Bashungwa aungana na wananchi Kagera kumkaribisha nyumbani Kardinali Rugambwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,897
941
Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ameungana na wananchi wa wilaya ya Karagwe na Mkoa Kagera katika hafla ya kumpongeza na kumkaribisha nyumbani Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa, baada ya kuteuliwa na kusimikwa rasmi na Baba Mtakatifu Francisko kuwa Kardinali.

Hafla hiyo ilifanyika Disemba 28, 2023 nyumba alipozaliwa katika kijiji cha Kasheshe, Nyaishozi wilayani Karagwe mkoani Kagera na kuhudhuria na viongozi mbalimbali wa wa Dini na Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Fatma Mwassa, ambapo pamoja na mambo mengine Waziri Bashungwa alitoa salamu za pongezi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Kardinali Rugambwa.

"Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anaungana na Watanzania kuendelea kumpongeza Kardinali kwa heshima hii ambayo nchi yetu tumeipata, amenipa dhamana ya Wizara ya Ujenzi na baada ya kuona mawasiliano barabara ya kuja hapa Kasheshe yalivyokuwa, sisi tulijiongeza ili tusimuangushe Rais tukatengeneza barabara ili wageni watakaotoka sehemu mbalimbali wafike hapa kwa urahisi kwa kumpongeza Kadinali"- alisema Bashungwa.

Bashungwa alitoa wito kwa Watanzania wote kuendelea kumuombea Kardinali Rugambwa kheri, afya njema, na mafanikio katika utumishi wake.

Kwa Upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Fatma Mwassa alisema Mkoa wa Kagera una bahati sana kwani umeweza kumtoa Kardinali na hiyo ni heshima ya kipekee ambayo itasaidia mkoa wa Kagera kuwa na wacha Mungu na kuepuka yote yaliyokatazwa kwenye maandiko matakatifu.

"Tuepuke yote yaliyokatazwa ikiwemo uzinzi, kula rushwa, wizi, roho mbaya na uuaji. Tuishi kwa upendo na kutenda yale yanayompendeza Mungu na tukitenda hivyo tutakuwa tumemfurahisha Mungu na tutakuwa tumemfuharisha Kadinali wetu Rugambwa" - alisema RC Mwassa.

Naye, Mwadhama Protase Kardinali Rugambwa aliwashukuru wananchi wa Kagera kwa kumpokea na kuwasihi Watanzania kuendelea kumtegemea Mungu kwa kila jambo ili waweze kuvuna mema.

"Tubaki tumejiaminisha kwa Mwenyezi Mungu na akiwa pamoja nasi tunaamini kabisa tunaweza kuyafanya mengi sana katika maisha yetu. Niwasihi tuzidi kumtegemea Mungu ndiye anayetufanya tuendelee kuwepo na ndiye anayefanya tuyapate mengi kupitia kwa wengine ambao ni yeye mwenyewe kawaweka" - alisema Kardinali Rugambwa.

WhatsApp Image 2023-12-29 at 12.55.27.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-29 at 12.55.28.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-29 at 12.55.28(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-12-29 at 12.55.29.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-29 at 12.55.29(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-12-29 at 12.55.30.jpeg
WhatsApp Image 2023-12-29 at 12.55.30(1).jpeg
 
Back
Top Bottom