Bashiru Vs Membe: CCM yatoa msimamo wake kuhusu suala hilo

😀😀😀😀😀
 
Hayo maelezo mengine mengi ni chini yanachosha tu ila kichwa tu cha habari kinajitosheleza kbs kuwa Mh. Rais alibugi au tuseme kuna kachuki kauchaguzi uliopita wa timu A na B kutokana na mparangano wakati wa kuwania nafasi hii adhimu.
Kuna uwezekano pia mkuu alipima maji kama huyu nguli wa kidiplomasia anaweza kupokea na kutekeleza zile zinazoitwa amri toka juu, wakapata mashaka na kumuacha.
Huenda pia kulikuwa na hofu kuwa huyu jamaa ni mashuhuri duniana kidiplomasia na ana akili nyingi na mbinu kwahiyo ni hatari kwa akili kidogo wakaona isiwe tabu wakamtosa.
Inawezekana pia walimhofia kwakuwa timu yake ndani ya chama na serikali ingalipo na inanguvu kwahiyo kumpatia nafasi ndani ya serikali yake ni kuimarisha/kutia nguvu zaidi timu yake na kuhatarisha/kudhoofisha utendaji wa serikali ya awamu hii kama itatokea wangetofautiana ktk maamuzi flaniflani ndani ya serikali. Hofu ya timu JK kuendelea kuwepo serikalini pia inaweza kuwa sababu za kumtosa.
 
Kwahiyo mnataka chadema wakavamie magereza wamkomboe Mbowe!, waandamane kwa kitu kilichopo mahakamani?

Ccm ni mzigo kabisa, hamjaribu kutumia hata 0.2 ya ubongo kufukiri.

Mbafu!
 
Naona unachanganya mambo, kuwa na taarifa sahihi na kuchukua maamuzi sahihi ni mambo mawili tofauti. Kwani hao wanaovuta sigara ni kwamba hawana taarifa sahihi kwamba zina madhara?
Hahahahahah sijui umeandika nini.
 
Chadema wako bize kumpotosha Membe kama walivyompotosha Lowasa.

Mahaba ya Chadema kwa Membe yanasitajaabisha , badala ya kumlilia Mbowe yupo gerezani wako bize kumlilia mwana ccm Membe!!!!

Apotoshwe kwani yeye mtoto mdogo? Hayo mambo yenu wenyewe CCM yamalizeni wenyewe. keshawashika kende mnabaki kulia lia.
 
Kwani keshkokutwa hawezi kupewa dhamana!?oohh maskini amekwisha
 
Pamoja na yote hayo 2020 magufuli ccm hana chake mchuano utakuwa lissu(cdm) na Membe(ccm)
 
Jamaa kajifanya mjanja na kusahau kwamba;mjanja hajinyoi.
Tuone chamelon amnyonyoe atie akili
 
Na misukule mwaka huu inaipambwa kwa kila rangi. Membe hata ule uwaziri wa mambo ya nje alikuwa hafai. Alibebwa tu kwenye ule utawala ulikuwa umejaa vilaza kama kina Masha, Ngeleja nk

Asante kwa Kuchangia siku njema!
 
hivi kwani Membe si mwanachama wa kawaida tu upande ule
 
Kada wa CCM na aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe aliyekuwa mtia nia wa urais kupitia CCM mwaka 2015, akiwa anahojiwa na ITV, mwaka 2013 alidai kwamba, yeye ana maadui 11 na kwamba ikifika mwaka 2016, wataihama Nchi.

Membe aliitoa kauli hiyo akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na kwa nafasi yake hiyo, isiyomhusisha na masuala ya ndani ya Nchi, tulitegemea ndiye Waziri wa kwanza ambaye atakuwa na maadui wachache sana nchini, achilia mbali kutokuwa nao kabisa kwani Wizara yake ina-deal zaidi na masuala ya nje ya Nchi.

Hata bungeni, Wizara ya Mambo ya Nje, ni mojawapo ya Wizara chache sana nchini ambazo huwa hazikumbani na maswali magumu bungeni na hupitishwa haraka haraka bila ugumu wowote kutoka kwa Wabunge. Ni kama ilivyo pia kwa Wizara ya Ulinzi.

Sasa, swali linakuja: Kwa kazi gani alizozifanya Bernard Membe katika uwaziri ubunge na wake toka mwaka 2000 hadi 2013, ambao ulimsababishia yeye kuwa na maadui wa mpaka kuweza kutajwa hadi kwenye Tv? Basi hata angekuwa adui 1, maadui yaani wote hao hadi11? Basi napo ungemalizana nao humu humu ndani, yaani unataka hadi wakimbilie Kenya? Ni adhabu gani uliwapangia kuwafanyia hadi uwatake wakimbilie Kenya - ulitaka kuwaua?

Kaulii hiyo ya Membe aliyoitoa kwa umma wa Watanzania ilitaka umma umuone Membe ni strong kuliko Kikwete aliyeonekana dhaifu ama? Je, hao aliowataja ni maadui wa Taifa ama ni maadui wa Membe?

Kwa statement hiyo ya Membe, nini cha kumshauri Rais Magufuli dhidi ya Membe? Na yeye Rais amfukuzie mbali ama?

Je Rais Magufuli amtake Membe kama "anaguna anyooshe mikono ajifanye kama anajukuna?

Je, Membe ndiye anayesifiwa kwa utendaji wa Sera za Mambo ya nje? Soma hapo chini.

Mh Bernard Membe, Ulishafuta kauli hii Kuhusu Rajoelina - JamiiForums

Bernard Membe: Nina maadui 11, ikifika 2016 watakimbilia Kenya! - JamiiForums
 
Rais Dk. John Pombe Magufuli, hana kinyongo chochote na Viongozi wenzake ndani ya CCM na ndani ya Serikali na ndani ya Dola lakini wao wanamhujumu kwa nia zao mbaya. Wengi walipewa nafasi huko nyuma walishindwa ku-deliver, amekuja mwenzao wanaanza kumuonea wivu.

Magufuli pitia hiki Kitabu cha The Prince cha Karne ya 16 kutoka kwa gwiji la Kitaliano, Niccolo Machiavelli, upate ushauri namna ya ku-deal na adversaries wako.

Machiavelli's The Prince
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…