Bashiru Ally ameongoza mazishi ya watoto walioungua moto huko Kyerwa Kagera kama nani?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,666
218,169
ITV imemuonyesha Katibu Mkuu wa CCM ndugu Bashiru Ally akitajwa kuwa mgeni rasmi kwenye mazishi ya watoto 10 waliozikwa leo huko Kagera, sina shida na mtu yoyote kuhudhuria mazishi yoyote popote lakini kumpa cheo cha kuongoza mazishi mtu asiye na cheo chochote kwenye Serikali yetu ni dharau kubwa sana kwa wananchi na marehemu wao.

Kuleta kampeni za kishamba kwenye misiba isiyo ya kisiasa haikubaliki na hali hii ikiachwa iko siku itakuja kuleta machafuko kwenye misiba na kuharibu shughuli za watu, fanyeni siasa zenu majukwaani.

Napinga CCM chama kilichokongoroka kujaribu kutumia majanga kujinadi, marehemu hao ambao walikuwa watoto hawakuwahi kuwa na kadi za CCM, za chipukizi wala za UVCCM, hii haikubaliki hata kidogo.
 
Kwa CCN kila kitu ni siasa.... Misiba na maafa kwa CCM ni mtaji wa kisiasa.

Hapo malengo yake ni kugombea ubunge 2025.
 
Aliendaa itifaki hiyo kawakosea sana wadau wa msiba. CCM kuongoza mazishi!? Ni sawa na kojo/mchanga ktk pilau.
 
Back
Top Bottom