Bashe na kundi lake wanaigharimu CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bashe na kundi lake wanaigharimu CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OTIS, Aug 23, 2012.

 1. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kijana huyu na kundi lake amekuwa mstari wa mbele kukihujumu Chama cha mapinduzi kwa siasa zao za chuki na kutafuta ugomvi.

  Ni jambo la ajabu na la kusikitisha sana kwani kijana huyu ana sifa ya kusaka ugomvi na inaonekana hadi kwenye utendaji wake kwenye akiongoza Habari Corporation.

  Makala mbalimbali ambazo zimekuwa zinatolewa na magazeti ya habari corporation zimekuwa zinalenga kumhujumu Mhe Rais na viongozi waadilifu ndani ya chama na serikali.

  Ikumbukwe kwamba Rostam na vijana wake kina Bashe ndio walimpiga marufuku Nape asikanyage Igunga wakati wa uchaguzi mdogo kwani wao wanaendekeza ugomvi na wana CCM zaidi badala ya kuleta maendeleo ya nchi hii.

  Natoa rai kwa serikali kufuatilia nyendo za kundi hili kwani latishia ustawi wa nchi hii kwani hata uraia wao unatiliwa shaka na mpaka kesho hatujapata uthibitisho wa uraia wao.

  Kuna umuhimu hili zoezi la vitambulisho vya taifa likatuondolea watu kama hawa nchini.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Kumbe hampendi kusemwa mnapofanya madudu eeh? Fungieni basi gazeti lao km kawaida!
  Ni ajabu na inafurahisha sn ninapoona ccm wanapolia kilio cha mbwa mdomo juu!
   
 3. t

  tenende JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mnapobanwa mnakimbilia kusema mtu si raia!..
   
 4. C

  Concrete JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Anachochewa na Chadema huyo.

  Chadema wamezidi uchochezi dhidi ya serikali yetu pendwa, walianza kupitia kwa madaktari, walimu, wastaafu, Mwanahalisi, Vita dhidi ya Malawi, kugomea sensa na sasa Bashe.
   
 5. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Mchawi anapokata roho ulopokalopoka kila aina ya neno!!amini,usiamini,ccm imefika mwisho,mwacheni bashe na fisadi lake rostam ccm imenyanyasa sana wakulima na wafanyakazi kama madaktari,walimu n.k na mbaya zaidi walimu sasa wanawafudisha watoto haki na kuwaelimisha juu upumbavu unaofanywa na serekali ya magamba ncha kama haina rais,,yaani ni dhaifu yupoyupo tu!msitafute mchawi wakati huu,wananchi tumeamua kuwa chukia hasa dhaifu.
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,265
  Trophy Points: 280
  Kamati kuu ya CCM ilisema siyo raia wakamkata jina, lakini Laurence Masha aliyekuwa na dhamana ya kutangaza kama mtu ni raia au siyo raia aliutangazia umma wa Tanzania kwamba Bashe ni raia halali, sasa wewe unaweweseka na nini? na bado hilo Gazeti la Rai na Mtanzania litawanyoosha mpaka mnyooke na siri ya kulifungia Mwanahalisi imeshafichuka.
   
 7. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  pia wanatia chuki mawizarani, na ktk mashirika ya uma, ona kagasheki na mwakyembe wnavyo simamisha wakurugenzi kazi, CHADEMA wapo nyuma hapo. baya zaidi ni hili la udini wa CHADEMA wakaingilia uhuru wa mahakama, ili Costa mahalu na mwenzie Grace wakaachiwa huru. aggggggggggggggh, kwakweli sasa wamezidi, maana hata malipo ya makarani wa sensa wameyatia doa
   
 8. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 24,952
  Likes Received: 37,491
  Trophy Points: 280
  Sasa hivi ndio mnawaona hawafai wakati bosi wao ndio alimfadhili mgombea wenu kwenye uchaguzi mkuu.Hata kwenye uchaguzi mdogo wa igunga si ndio yeye anaedaiwa kugharamia helikopta.

  Bora mkae kimya maana mnatuboa.
   
 9. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  mbona NAPE naye sio raia..we umewahi kusikia jina la NAPE wapi tanzania..huyu ni mtu wa timbuktu huyu na ushahidi tunao
   
 10. papason

  papason JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Wacheni wamagamba wamalizane wao wenyewe, sis tutawa tandika pigo la mwisho 2015!
   
 11. M

  MTK JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2012
  Joined: Apr 19, 2012
  Messages: 6,960
  Likes Received: 2,837
  Trophy Points: 280
  OTIS

  Be fair please and remember what goes around comes around!! Je, wewe unakubaliana na jinsi Bashe alivyotendewa katika kinyanganyiro cha uchaguzi 2010 kule Nzega hadi kuambiwa sio raia? Je, hiyo ilikuwa halali?

  If he is hitting back kutokana na anayoyajua yamekaa ndivyo sivyo ndani ya CCM ni haki yake na usimtuhumu kuwa anahujumu chama! Kina Makamba waliojaribu kumfutia uraia wake wewe unawaitaje?

  Hivi wewe unamwona Nape ni mtu wa maana? Hebu fanya home work yako vizuri ndio uongee hadharani and avoid being judgemental in the absence of detailed facts; No research no right to speak!
   
 12. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,148
  Likes Received: 1,242
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu mwadilifu ndani ya Chama na Serikali? Acha uzushi wewe na kulalamika wewe, sema wote mnagombea maslahi yenu binafsi tu.

  Sema anatishia Ustawi wa CCM na wala sio nchi. Mkishikwa kwenye nyeti mnakimbilia kwenye Uraia na kupeleka watu msitu wa Pande.
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2012
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  Nasikia rostam ni msukuma na bashe ni mnyamwezi.............wenzetu bado wanaidharau rangi yao na kuwatukuza waarabu na wasomali kuwa ni watz.........
   
 14. c

  chachu Senior Member

  #14
  Aug 23, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 140
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Haki ya mtu haipotei na mfa maji haachi kutapatapa
   
 15. M

  Molemo JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Huu ni ujinga mtupu.Bashe move on......
   
 16. only83

  only83 JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Hivi Bashe kumbe sio raia.
   
 17. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  OTIS

  Hii ndiyo raha ya Siasa za makundi. Bashe ni kambi ya EL na RA, na Beno Malisa amejiunga tayari. Ndoa ya Beno na rafiki mpendwa na familia yake ilishavunjika na ile nyumba iliyonunuliwa kupitia mgongo wa Beno alishairudisha!!! Tunajua mengi, basi tunakaa kimya!! Imagine unanunua asset ili kuficha uhalisia unaandika jina la rafiki. Na urafiki ukivunjika unamdai, haki ya nani sirudishi!!!

  Mafisadi nyie wote tu maana ukikubali kumtumikia fisadi na wewe ni fisadi maana mtoa rushwa na mpokeaji wote ni wahalifu.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #18
  Aug 23, 2012
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Alisafishwa ni raia ila yuko ile kambi nyingine.
   
 19. U

  Unstoppable JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mwenyekiti ni Kikwete, alafu huyo huyo wanalalamika anahujumiwa na mtu mdogo kama Bashe? Basi si aachie ngazi amwachie mtu shupavu anayejua kuongoza chama? Kama kila wakati tu yeye wanachezea rafu; basi ni wazi hana support kwenye chama au ni dhaifu asiyejua lakufanya; aachie wanaoweza hiyo kazi. Kazi huwezi bado unang'ang'ania unategemea wanachama wako wafanyaje sasa?
   
 20. M

  Mfukunyuzi Senior Member

  #20
  Aug 23, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 127
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wewe ni mbumbumbu na haujielewi kabisa
   
Loading...