Bashe Hasomeki

NTIGAHELA

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
362
254
HOUSE NEGRO vs FIELD NEGRO

Mwanzoni mwa miaka ya 1960, mpigania haki, uhuru na heshima ya mtu mweusi ndani ya America hayati Malcolm X alitoa hotuba ya kihistoria na kukumbukwa.
Malcolm X alikuwa akiwatumia ujumbe Wamarekani weusi wa kipindi hicho ambao kwa sababu ya kunufaika kwa namna moja au nyingine na utawala wa kidhalimu wa kizungu unaokandamiza haki za mtu mweusi nchini humo walikuwa wakihujumu jitihada za weusi wenzao waliosimama kidete kutaka na kupewa heshima yao ya kiutu wanayostahiki kama binadamu katika nchi hiyo.

Malcolm X alikumbusha kisa cha watumwa wa aina mbili waliokuwepo kipindi cha utumwa,
1. Watumwa wa Ndani ya nyumba
2. Watumwa wa mashambani huko nje ya nyumba

Malcolm X akasema"WATUMWA WA NDANI YA NYUMBA" ( HOUSE NEGROES) waliishi ndani ya nyumba na bwana mkubwa, walikula chakula kizuri cha bwana mkubwa, Walimpenda bwana mkubwa kuliko hata bwana mkubwa anavyojipenda yeye, Ikitokea bwana mkubwa anaumwa huyu Mtumwa wa ndani ya nyumba atakuja kimbelembele huku anamwambia BOSI TUNAUMWA?, yaani kuumwa aumwe bosi lakini eti hata Mtumwa huyu anadai eti naye anaumwa!- Absurd

Kwa upande mwingine kuna watumwa wa upande wa pili, wale wa mashambani, hawa walinyanyapaliwa, waliteswa, walifokewa, walikula makombo hawa hawakumfagilia Bosi hata kidogo, hawa kama ikitokea moto umewaka unaunguza nyumba ya bosi, hawa wangeombea uje upepo mwingi zaidi nyumba Iungue lisibaki hata jivu.

Falsafa hii ya Malcolm X imenifikirisha juu ya tamko la Hussein Bashe juu ya Wazee wetu mzee Kinana na Mzee Makamba, Ukimsikiliza Hussein Bashe tamko lako limejaa hofu, unafiki, kujipendekeza na kwa kweli halina tofauti na tabia ya MTUMWA Wa Ndani ya Nyumba ( HOUSE NEGRO)

At the same time ukisoma tamko la Wazee wetu mzee Kinana na Makamba ni tamko la kijasiri la kishujaa na linalenga zaidi kusaidia kuweka breki kwenye tabia za siasa za Uzandiki, Chuki, Character assasination, Uonevu na tabia zote za siasa za kuraruana kwa sababu ya Ulafi wa madaraka na hofu ya kutaka shortcut ya kisiasa kwa kutumia STATE MACHINERY badala ya kutumia medani za kisiasa, Kwa kweli katika ile mifano ya MALCOLM X, Wazee wetu hawa wamekuwa kama yule FIELD NEGRO, Mtumwa wa nje ya nyumba asiyependa mambo ambayo Bwana mkubwa anafanya.

1 .Bashe ana tabia za kutoa kauli za kubomoa badala ya kujenga
Wakati ule wimbi la uonevu dhidi ya wapinzani halijaanza kasi sana nchini, Ni Hussein Bashe aliyetoa kauli za kuunga mkono siasa za fujo na vurugu, Huyu alisikika akitoa wito kwa wana CCM "Kurudisha Mapigo" kwa kuwapiga Wapinzani kama njia ya "Self defence", akaendelea kutamba kuwa hawna hofu ya kuwa na wasiwasi kwa sababu POLISI ni wao!, Hebu tazama kauli hii na mambo yaliyofuata nchini ya siasa za kibabe na uonevu uliokithiri dhidi ya wapinzani nchini. Bashe hajawahi kuomba msamaha kwa kauli hii na sijui kwa nini watu wasimuone yuko responsible kwa matendo ya kikatili yaliyowafika wapinzani nchini.
Lakini leo hii ambapo Wazee wetu Mzee makamba na mzee Kinana wametoka mbele, kuonyesha kukerwa na tabia za siasa chafu, za kizandiki ni Bashe yule yule anayetokea na kujaribu kuitia matobo kazi hii ya Wazee wetu hawa ambao kwa sababu ya busara zao wanajua kuwa tabia hii ya siasa chafu ikiachwa then itapelekea watu kuumizwa zaidi na zaidi na kupelekea uvunjifu mkubwa wa amani nchini. Badala ya huyu kijana kuangali BIG PICTURE yeye anakuja na hoja zake za shallow
shallow kuhusu tamko la wazee. HIVI BASHE ANADHANI ANAIJUA CCM KULIKO MZEE KINANA?

2. Bashe na Kambi yake bado wana hangover ya Uchaguzi wa 2015
Hasira na kinyogo cha mtu wao kukatwa mwaka 2015 bado kingali ndani ya mitima ya watu wa timu yao, Safari ya Matumaini ilisitishwa wakiwa ndani ya CCM, kisha ikasitishwa wakiwa nje ya CCM. Na hii kazi ya kumkata mtu wao iliyofanywa kwa maslahi mapana ya nchi yetu hawakuipenda, walishatumia fedha nyingi, walishapanga timu zao, lakini akina mzee Kinana walisimama kwa maslahi mapana ya nchi. Bashe na timu yao wanaona sasa ni muda muafaka kulipiza kisasi juu wazee wetu hawa, Ndiyo maana ni majuzi tu Bashe alitoa kauli nyingine kwenye mitandao ya jamii kauli isiyo ya staha kumlaumu Mwenyekiti mmoja mstaafu wakati alipotoa ujumbe wa kumpokea tena EL, Na leo Bashe huyohuyo anatumia nafasi hii "KUMPIGA" mzee Kinana kama namna ya kulipiza kisasi kwa "Mtu wake kukatwa"

3. Bashe anataka kununua "loyalty“
Bashe anajua kuwa hata yeye hakubaliki sana na kambi ya bwana mkubwa, kauli kadhaa za mafumbo zimeshatolewa juu ya watu wanaoweza kukatwa mwaka 2020, Hata Musiba naye amemuweka kwenye list, sasa huyu kijana nahisi anaona kuwa by all means kama hakujitokeza na Kuvaa koti kubwa zaidi la kijani kuliko wenzie, au kuimba kwa sauti kubwa zaidi kuwa 2020 ni Magufuli tu, au asipoonyesha kuunga mkono Juhudi kwa kasi mara kumi zaidi ya wanaunga mkono basi hawezi kuaminika hata afanyeje. Hiki alichofanya juzi kinaweza kumsogeza karibu kwenye meza ya "wakubwa", lakini itabidi afanye zaidi, asifu zaidi, anyooshee vidole zaidi wanaosimama ndani ya CCM kupinga Siasa za kizandiki, za hovyo, za majitaka na siasa za kishamba

4. Bashe na Katiba ya CCM
Huyu kijana anawasema wazee wetu mzee Kinana na Mzee Makamba eti tamko lao wanamlenga Raisi Magufuli, kwanza lazima aelewe kwamba kama kuna mtu ambaye angependa Raisi Magufuli afanikiwe ni hawa Wazee, Kwanza walimpigania, wakamuunga mkono na wakamnadi mbele ya wananchi na wakampa msaada wote wa kichama mpaka akawa hapa alipo, kwa hiyo kufanikiwa kwa raisi Magufuli kunawapa hawa wazee pride kuwa kazi waliyoifanya inaleta matunda.
Pili Mzee Makamba mwanae ni Waziri, Raisi Magufuli ni Mwajiri wa mwanae, kampa ajira mwanae kwa hiyo angekuwa the last person kutaka "Tajiri huyu mwema kwa mwanae aanguke".
Hawa wazee hakuna hata mmoja anayetaka raisi Magufuli ashindwe, bali wanataka NCHI IENDESHWE KWA SIASA SAFI NA UONGOZI BORA!. Hakuna excuse ya kufanya siasa za chuki, visasi, uonevu kwa namna yoyote ile!. Wakati Mwalimu Nyerere anaikosoa serikali ya Mwinyi haimaanishi kuwa hata yeye zamani alikuwa hafanyi makosa, hapana!, Ukiona tatizo lazima uliseme hata kama huko zamani na wewe umewahi kufanya makosa, Kukemea mambo ya ajabuajabu NDO MATURITY HIYO!.
Lakini at the same time Bashe anawesema wazee hawa, kuwa hawakufuata kanuni na katiba ya Chama katika tamko lao, hata hivyo na yeye Bashe katika tamko lake hilohilo anafanya kosa la kikatiba ANATANGAZA KUUNGA MKONO MGOMBEA FULANI AMBAYE BADO HAJAPITISHWA NA VIKAO VYA CHAMA!. Raisi Magufuli yes ni rais wa nchi na ni mwenyekiti wa chama, lakini kuwa huko raisi na mwenyekiti wa chama hakumuweki juu ya chama, CHAMA BADO HAKIJATOA RUHUSA YA MTU KUTANGAZA NIA KWA HIYO YOYOTE ANAYEEONYESHA KUTANGAZA KUUNGA MKONO MTU FULANI AWE MGOMBEA WA CHAMA "IWE MVUA, IWE JUA" MTU HUYO ANATENGENEZA MAKUNDI NDANI YA CHAMA NA NI KINYUME CHA KANUNI ZA CHAMA!. Raisi Magufuli bado hajapitishwa na Chama kugombea 2020 kwa hiyo siyo sahihi kutangaza kuwa ndiye Mgombea iwe Jua iwe mvua. Bashe toa boriti kwenye jicho lako kabla ya kutoa kibanzi katika jicho la Wazee!

5. Mwisho, Mzee Makamba na Mzee Kinana wamesimama katika muda na wakti muhimu katika historia ya nchi yetu
kutamka waliyoyatamka kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yetu, wangetaka kukaa kimya wangekaa kimya kwa sababu hakuna mtu serious ambaye anamchukulia huyu Musiba serious. Ila kilicho serious siyo huyu Musiba, bali kile kilichopo nyuma yake, ni dhahiri kilicho nyuma ya Musiba ni tufani zaidi, Maumivu zaidi, hofu zaidi kwa hiyo hii hali ilipaswa ikomeshwe. Na hawa wazee wetu ni Masjasiri, Wamepikwa kiuongozi, Wamepikwa Kijeshi, Wanajua Propaganda ni zipi na wanajua chenye hatari kwa Taifa ni kipi. HAWA WAZEE WAMESEMEA WENGI la sivyo ambacho kingefuata huenda ni kibaya zaidi kwa mustakbali wa nchi yetu. Mimi nawapongeza sana hawa wazee.

Katika Sakata hili linaloendelea nchini Tutakwenda kuwajua zaidi ndani ya CCM ni akina nani ni MAHOUSE NEGROES na MAFIELD NEGROES NI akina nani!
 
Eti wazee wetu, naona walivyosemwa nawe imekuwa kama mahouse negroes ! Punguzeni umimi na usisi!!
 
Tangu enzi za wakongwe wa siasa za muundo wa jamhuri, shirikisho, falme na nyinginezo, wale akina Julius Caesar, jenerali Pompeii, Cecero na Carrius inatambulika ktk siasa na kupigania guvu za kidola lazima kuwe na character assassination, na propaganda.

Pia inatambulika mwenye nguvu iwe ya kijeshi au yaani alie shika dola lazima aitumie kujidhatiti asipokonywe udhibiti.

Hizi kelele zote za kumshambulia Mh. Magufuli ni muendelezo tu wa harakati za kisiasa za kutaka aondolewe udhibiti wa dola. Nayeye atakuwa mwanasiasa wa ajabu aache kuitumia hiyo nguvu kuhakikisha anakuwa na udhibiti utakaomuwezesha kumalizia muda wake kikatiba.

Sio kweli kwamba yote anayo tuhumiwa au kutukanwa anakosea. Wanao fanya hivyo ni kama na wao wanafanya character assassination kuhalalisha harakati zao kumtoa kwenye udhibiti wa dola.

Sasa wakizidiwa wasilielie kutafuta huruma kwa wananchi bali wapambane kujibu mapigo. Kama hawawezi basi watulie wakubali yaishe.
 
HOUSE NEGRO vs FIELD NEGRO

Mwanzoni mwa miaka ya 1960, mpigania haki, uhuru na heshima ya mtu mweusi ndani ya America hayati Malcolm X alitoa hotuba ya kihistoria na kukumbukwa.
Malcolm X alikuwa akiwatumia ujumbe Wamarekani weusi wa kipindi hicho ambao kwa sababu ya kunufaika kwa namna moja au nyingine na utawala wa kidhalimu wa kizungu unaokandamiza haki za mtu mweusi nchini humo walikuwa wakihujumu jitihada za weusi wenzao waliosimama kidete kutaka na kupewa heshima yao ya kiutu wanayostahiki kama binadamu katika nchi hiyo.

Malcolm X alikumbusha kisa cha watumwa wa aina mbili waliokuwepo kipindi cha utumwa,
1. Watumwa wa Ndani ya nyumba
2. Watumwa wa mashambani huko nje ya nyumba

Malcolm X akasema"WATUMWA WA NDANI YA NYUMBA" ( HOUSE NEGROES) waliishi ndani ya nyumba na bwana mkubwa, walikula chakula kizuri cha bwana mkubwa, Walimpenda bwana mkubwa kuliko hata bwana mkubwa anavyojipenda yeye, Ikitokea bwana mkubwa anaumwa huyu Mtumwa wa ndani ya nyumba atakuja kimbelembele huku anamwambia BOSI TUNAUMWA?, yaani kuumwa aumwe bosi lakini eti hata Mtumwa huyu anadai eti naye anaumwa!- Absurd

Kwa upande mwingine kuna watumwa wa upande wa pili, wale wa mashambani, hawa walinyanyapaliwa, waliteswa, walifokewa, walikula makombo hawa hawakumfagilia Bosi hata kidogo, hawa kama ikitokea moto umewaka unaunguza nyumba ya bosi, hawa wangeombea uje upepo mwingi zaidi nyumba Iungue lisibaki hata jivu.

Falsafa hii ya Malcolm X imenifikirisha juu ya tamko la Hussein Bashe juu ya Wazee wetu mzee Kinana na Mzee Makamba, Ukimsikiliza Hussein Bashe tamko lako limejaa hofu, unafiki, kujipendekeza na kwa kweli halina tofauti na tabia ya MTUMWA Wa Ndani ya Nyumba ( HOUSE NEGRO)

At the same time ukisoma tamko la Wazee wetu mzee Kinana na Makamba ni tamko la kijasiri la kishujaa na linalenga zaidi kusaidia kuweka breki kwenye tabia za siasa za Uzandiki, Chuki, Character assasination, Uonevu na tabia zote za siasa za kuraruana kwa sababu ya Ulafi wa madaraka na hofu ya kutaka shortcut ya kisiasa kwa kutumia STATE MACHINERY badala ya kutumia medani za kisiasa, Kwa kweli katika ile mifano ya MALCOLM X, Wazee wetu hawa wamekuwa kama yule FIELD NEGRO, Mtumwa wa nje ya nyumba asiyependa mambo ambayo Bwana mkubwa anafanya.

1 .Bashe ana tabia za kutoa kauli za kubomoa badala ya kujenga
Wakati ule wimbi la uonevu dhidi ya wapinzani halijaanza kasi sana nchini, Ni Hussein Bashe aliyetoa kauli za kuunga mkono siasa za fujo na vurugu, Huyu alisikika akitoa wito kwa wana CCM "Kurudisha Mapigo" kwa kuwapiga Wapinzani kama njia ya "Self defence", akaendelea kutamba kuwa hawna hofu ya kuwa na wasiwasi kwa sababu POLISI ni wao!, Hebu tazama kauli hii na mambo yaliyofuata nchini ya siasa za kibabe na uonevu uliokithiri dhidi ya wapinzani nchini. Bashe hajawahi kuomba msamaha kwa kauli hii na sijui kwa nini watu wasimuone yuko responsible kwa matendo ya kikatili yaliyowafika wapinzani nchini.
Lakini leo hii ambapo Wazee wetu Mzee makamba na mzee Kinana wametoka mbele, kuonyesha kukerwa na tabia za siasa chafu, za kizandiki ni Bashe yule yule anayetokea na kujaribu kuitia matobo kazi hii ya Wazee wetu hawa ambao kwa sababu ya busara zao wanajua kuwa tabia hii ya siasa chafu ikiachwa then itapelekea watu kuumizwa zaidi na zaidi na kupelekea uvunjifu mkubwa wa amani nchini. Badala ya huyu kijana kuangali BIG PICTURE yeye anakuja na hoja zake za shallow
shallow kuhusu tamko la wazee. HIVI BASHE ANADHANI ANAIJUA CCM KULIKO MZEE KINANA?

2. Bashe na Kambi yake bado wana hangover ya Uchaguzi wa 2015
Hasira na kinyogo cha mtu wao kukatwa mwaka 2015 bado kingali ndani ya mitima ya watu wa timu yao, Safari ya Matumaini ilisitishwa wakiwa ndani ya CCM, kisha ikasitishwa wakiwa nje ya CCM. Na hii kazi ya kumkata mtu wao iliyofanywa kwa maslahi mapana ya nchi yetu hawakuipenda, walishatumia fedha nyingi, walishapanga timu zao, lakini akina mzee Kinana walisimama kwa maslahi mapana ya nchi. Bashe na timu yao wanaona sasa ni muda muafaka kulipiza kisasi juu wazee wetu hawa, Ndiyo maana ni majuzi tu Bashe alitoa kauli nyingine kwenye mitandao ya jamii kauli isiyo ya staha kumlaumu Mwenyekiti mmoja mstaafu wakati alipotoa ujumbe wa kumpokea tena EL, Na leo Bashe huyohuyo anatumia nafasi hii "KUMPIGA" mzee Kinana kama namna ya kulipiza kisasi kwa "Mtu wake kukatwa"

3. Bashe anataka kununua "loyalty“
Bashe anajua kuwa hata yeye hakubaliki sana na kambi ya bwana mkubwa, kauli kadhaa za mafumbo zimeshatolewa juu ya watu wanaoweza kukatwa mwaka 2020, Hata Musiba naye amemuweka kwenye list, sasa huyu kijana nahisi anaona kuwa by all means kama hakujitokeza na Kuvaa koti kubwa zaidi la kijani kuliko wenzie, au kuimba kwa sauti kubwa zaidi kuwa 2020 ni Magufuli tu, au asipoonyesha kuunga mkono Juhudi kwa kasi mara kumi zaidi ya wanaunga mkono basi hawezi kuaminika hata afanyeje. Hiki alichofanya juzi kinaweza kumsogeza karibu kwenye meza ya "wakubwa", lakini itabidi afanye zaidi, asifu zaidi, anyooshee vidole zaidi wanaosimama ndani ya CCM kupinga Siasa za kizandiki, za hovyo, za majitaka na siasa za kishamba

4. Bashe na Katiba ya CCM
Huyu kijana anawasema wazee wetu mzee Kinana na Mzee Makamba eti tamko lao wanamlenga Raisi Magufuli, kwanza lazima aelewe kwamba kama kuna mtu ambaye angependa Raisi Magufuli afanikiwe ni hawa Wazee, Kwanza walimpigania, wakamuunga mkono na wakamnadi mbele ya wananchi na wakampa msaada wote wa kichama mpaka akawa hapa alipo, kwa hiyo kufanikiwa kwa raisi Magufuli kunawapa hawa wazee pride kuwa kazi waliyoifanya inaleta matunda.
Pili Mzee Makamba mwanae ni Waziri, Raisi Magufuli ni Mwajiri wa mwanae, kampa ajira mwanae kwa hiyo angekuwa the last person kutaka "Tajiri huyu mwema kwa mwanae aanguke".
Hawa wazee hakuna hata mmoja anayetaka raisi Magufuli ashindwe, bali wanataka NCHI IENDESHWE KWA SIASA SAFI NA UONGOZI BORA!. Hakuna excuse ya kufanya siasa za chuki, visasi, uonevu kwa namna yoyote ile!. Wakati Mwalimu Nyerere anaikosoa serikali ya Mwinyi haimaanishi kuwa hata yeye zamani alikuwa hafanyi makosa, hapana!, Ukiona tatizo lazima uliseme hata kama huko zamani na wewe umewahi kufanya makosa, Kukemea mambo ya ajabuajabu NDO MATURITY HIYO!.
Lakini at the same time Bashe anawesema wazee hawa, kuwa hawakufuata kanuni na katiba ya Chama katika tamko lao, hata hivyo na yeye Bashe katika tamko lake hilohilo anafanya kosa la kikatiba ANATANGAZA KUUNGA MKONO MGOMBEA FULANI AMBAYE BADO HAJAPITISHWA NA VIKAO VYA CHAMA!. Raisi Magufuli yes ni rais wa nchi na ni mwenyekiti wa chama, lakini kuwa huko raisi na mwenyekiti wa chama hakumuweki juu ya chama, CHAMA BADO HAKIJATOA RUHUSA YA MTU KUTANGAZA NIA KWA HIYO YOYOTE ANAYEEONYESHA KUTANGAZA KUUNGA MKONO MTU FULANI AWE MGOMBEA WA CHAMA "IWE MVUA, IWE JUA" MTU HUYO ANATENGENEZA MAKUNDI NDANI YA CHAMA NA NI KINYUME CHA KANUNI ZA CHAMA!. Raisi Magufuli bado hajapitishwa na Chama kugombea 2020 kwa hiyo siyo sahihi kutangaza kuwa ndiye Mgombea iwe Jua iwe mvua. Bashe toa boriti kwenye jicho lako kabla ya kutoa kibanzi katika jicho la Wazee!

5. Mwisho, Mzee Makamba na Mzee Kinana wamesimama katika muda na wakti muhimu katika historia ya nchi yetu
kutamka waliyoyatamka kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yetu, wangetaka kukaa kimya wangekaa kimya kwa sababu hakuna mtu serious ambaye anamchukulia huyu Musiba serious. Ila kilicho serious siyo huyu Musiba, bali kile kilichopo nyuma yake, ni dhahiri kilicho nyuma ya Musiba ni tufani zaidi, Maumivu zaidi, hofu zaidi kwa hiyo hii hali ilipaswa ikomeshwe. Na hawa wazee wetu ni Masjasiri, Wamepikwa kiuongozi, Wamepikwa Kijeshi, Wanajua Propaganda ni zipi na wanajua chenye hatari kwa Taifa ni kipi. HAWA WAZEE WAMESEMEA WENGI la sivyo ambacho kingefuata huenda ni kibaya zaidi kwa mustakbali wa nchi yetu. Mimi nawapongeza sana hawa wazee.

Katika Sakata hili linaloendelea nchini Tutakwenda kuwajua zaidi ndani ya CCM ni akina nani ni MAHOUSE NEGROES na MAFIELD NEGROES NI akina nani!

Huu uzi utaungwa mkono na upande fulani.

Ivi yale makubaliano kati ya Acacia na Barrick yanasemaje?
 
Najitahidi kumuelewa Bashe mzee wa kung'ata na kupuliza.
Body language inasoma usaliti alienation huku kauli ikijinasibu ni mtu sahihi
 
Back
Top Bottom