Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,441
- 5,238
Mbunge wa Nzega Mjini ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amemuomba Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan akifanikiwa kushinda na kuwa Rais wa Tanzania kwa awamu nyingine aidhinishe kugawanywa kwa Mkoa wa Tabora ili upatikane Mkoa mwingine wa Nzega kutokana na ukubwa wa Mkoa huo
.Akiongea leo September 10, 2025 wakati wa kampeni Nzega Mjini, Bashe amesema “Sisi hapa ombi letu kwako Mgombea, Watu wa Bukene ili aende kwenye Makao Makuu ya Halmashari ya Nzega Vijijini anasafiri zaidi ya KM 220, Mgombea ombi langu kwako katika kipindi chako cha pili nakuomba Rais tufikirie kuwepo na Halmashauri ya Bukene na Halmshauri ya Ndara, na nakutoa hofu kuhusu uwezo na rasilimali za kuendesha Halmashauri hizo hakuna tatizo”
“Tunaomba Mkoa huu ugawanywe kwasababu ndio Mkoa mkubwa kuliko Mikoa yote Tanzania, hii itakuwa kumbukumbuku kwasababu hili tumelilia kwa muda mrefu, na GDP ya Mkoa huu usiwe hofu nayo wala haitokuwa mzigo kwa Serikali”
Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema amelipokea na atalifanyia kazi ombi la Mbunge huyo la kuidhinisha kugawanywa kwa Mkoa wa Tabora ili upatikane Mkoa mwingine wa Nzega kwakuwa Mkoa wa Tabora ni mkubwa.
Dkt. Samia amesema ““Yote nayabeba na nakwenda kuyafanyia kazi, na mwenyewe anajua ndio maana kaniambia usijibu hapa lakini yabebe ukayafanyie kazi, kwahiyo la Halmshauri, la Campus ya UDSM kujengwa Nzega, na hili la Mkoa nakwenda kulifanyia kazi kwa undani zaidi”