Mkuu tunashukuru kusikia msimamo wako na kuwa muwazi hapa JF, lakini inanishangaza sana kuona wewe kama mmoja wa vijana tunaokutegemea, imekuwaje kuwa mstari wa mbele kushikamana na Rostam hasa wakati anajiuzuru kama sii kujenga majungu zaidi! Na hizi habari za rangi na Ukabila yamekukuta ukigombea Ubunge, leo bila kujifunza unakuwa mbele wakati chama chako kimekwisha amua kujivua magamba na Rostam ambaye hakubaliki unamtandikia red carpet!..
Huoni kama unazidi kujipotezea nafasi ya kuaminiwa na wananchi, pamoja na yote ndani ya CCM watakuona wewe mnafiki? Mkuu Siasa ni mchezo mchafu inatakiwa uwe makini sana na sii kuonyesha emotions zako mahala ambapo viongozi wako wamefikia maamuzi ya kumwondoa. Rostam kaondolewa madarakani, alipewa barua na makamu mwenyekiti mzee Msekwa, hizi habari za kujiuzuru ni staha tu alopewa lakini lugha ilikuwa wazi kwamba asipojiuzuru chama kitamwondoa! haya wewe ndio kwanza huelewi!