Zitto aache janja yake! Anatupiga tu wananchi changa la macho. Hii Kigoma Development Initiative(KDI) ni NGO yake mwenyewe! So hizo allowance zinamrudia yeye mwenyewe!
Yaani hata mtu akifanya jambo jema still anatiliwa shaka!!
Mbona Watanzania hatuna jema!!
BINAFSI NATOA PONGEZI ZANGU STAHILI.......(ANGALIZO) KAMA ALIPOELEKEZA ZIPELEKWE KWELI IKAWA NI NGO YAKE BINAFSI (hiyo ni sarkasi katuchezea) SI SAHIHI SANA.....! BALI NINGEMWELEWA ANGEPELEKA KATIKA TAASISI AMBAZO HANA MKONO WAKE KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE!
TUHESHIMU MCHANGO WAKE NA PIA LOLOTE AMBALO AENDA KINYUME TUWE KINYUME NALO
Mkuu Kimbunga ningependa km makamanda wote wange muunga mkono zitto, kwa mujibu wa Zitto Kabwe ile Barua ni yake binafsi, ameiandika kuelezea dhamila yake ya kutochukua posho!
Mkuu hivi huoni kama hapa kuna tatizo? Hapa inaonekana kama Zitto yupo peke yake wakati huo ni msimamo wa Chama.
Kweli kabisa!! Na hicho ndichi Zitto alichofanya. Halafu hpa ndani mijitu inampongeza tu bila hata kuthink bigHivi Zitto huwa hachangii hiyo KDI? Huwa anachangia kutoka wapi. Si ni kutokana na mapato yake yakiwemo ya posho? Sasa kama ameamua posho ziende kwenye mfuko anaouongoza kuna jipya hapa? Hii ni sawa na kusema msinilipe cash ila niwekeeni kwenye account yangu ya bank!!!
mwanzo mzuri lakini linatakiwa shinikizo kwa wabunge wengine kufanya hivyo
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, ameiandikia barua Ofisi ya Bunge kuiomba isimamishe kumlipa posho zake zinazotokana na vikao vya Bunge kuanzia juzi. Zitto ametoa ombi hilo kwa barua rasmi aliyoiwakilisha kwa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah Juni 7 mwaka huu.
Watu bana eti angeimarisha chama. Kwani kwa kutumia KDI CDM haiwezi kuimarika. Sometime tuweke siasa pembeni. Wana CDM wanaweza kumarisha CDM hata nje ya CDM. kuna mambo mengi ya kufanya nje ya siasa wapinzani wakifanya ni msumari kwa CCM.
Suala la posho ni suala Binafsi na hata chama bado wasingekubaliana wote. As an individual zito aana haki ya kujitolea kuonyesha njia kama wenzake wana sista sita basi yeye katangulia........... Ni kazi kwa wanaona inafaa nao wafuate njia na wakifika hata wabunge 10 utasikia hata bunge linafanya kuwa official
Zitto endelea lakini hizo pesa zi quantify zifanye nini sehemu gani .katika kila kikao cha bunge weka tangible output inayotakiwa kuonekana na uwachieved juu ya hizo pesa zako. La sivyo itakuwa ni siasa tu