Barua yangu kwako

Tanayzer

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
3,009
7,309
To the beautiful flower....

Ninatumai umzima wa afya....Ni kipindi kirefu kimepita, toka uamue kwenda mbali na kuacha moyo nahisia kwenye majonzi, umeacha roho ndani ya moto pengine umeacha mwili umeondoka na roho yangu.....

Najiuliza, nini kilifanya unikimbie??, na nadhani hali yangu haikuwa nzuri, labda ndo chanzo.... Huenda ulipenda pesa,zawadi, hata kile kidogo nilichokupa ukaona hakifai na kuamua kunitoa moyoni mwako na kuzima ndoto yangu ya kuja kuishi nawe....
Labda pengine marafiki zako walikushawishi uachane namm, kwa kuwa sijawahi onekana kama nina future mbele ya marafiki zako...
Pegine ni utoto alifanya udate na wavaa vizuri na wenye hadhi zao na kuona mtoto wa mkulima sina cha kukupa maishani....

Moyo unamsiba bado na kichwa hakiwezi kaa sawa,...

Natumaini unaendelea vizuri. Ila huku umeacha mtu nusu, furaha na mazoea uliyonizoesha vimegeuka mzigo mkali uliomshinda babu mwenye mzigo wa kuni kupanda mlima.....

Najaribu kukusahau ila siwezi,najaribu penda naishia kuumiza wasio na hatia.najaribu kaa bila upendo nakuwa mpweke zaidi ya ukiwa wa yatima asie na wazazi wote, ila naimani ipo siku nitapata kitu cha muhimu na nitakuwa na uwezo wa kukuafford labda sahizi wewe ni too expensive kwangu na you are too far from my poor reach.....

All the lord love and protection be upon you......
@By Tanayzer lamo
 
Kuna Mtu anaitwa Publius of Syrus (Ancient Rome Slave) aliwahi Kusema Love is the Source of Idle Anxiety, Pole sana Mkuu
Shukrani mkuu mchana nitajitahidi nionekane mjanja ila muda kama huu narudi kuwa yatima tena....I miss her now tungeweza tumiana text hata 80 za kuambiana nani aanze kulala....
 
Mimi kwenye mapenzi huwa sina kitu kukaa pembeni na kulalama au kuhadisia masela. Nikipigwa na chini nahakikisha nachukuwa chombo kuliko kile, hasa wakati kama huu Instagram sijui Facebook zimerahisisha kazi.

Sio kama zile enzi za babu zangu mpaka upite na demu mpya kwao yule wa zamani. Huweka pic za mpenzi mpya wa zamani anaanza mafumbo mwenyewe akijileta wala sina pozi nakula halafu nampiga chini ili iwe nimemuacha sio nimeachwa.😂😂

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
ila naimani ipo siku nitapata kitu cha muhimu na nitakuwa na uwezo wa kukuafford labda sahizi wewe ni too expensive kwangu na you are too far from my poor reach

Kama umelijua hili upo kwenye hatua nzuri, endelea kupambana mkuu..

Mpe hela
Mpe hela
Narudia Mpe hea
Nasisitiza mpe hela
 
To the beautiful flower....

Ninatumai umzima wa afya....Ni kipindi kirefu kimepita, toka uamue kwenda mbali na kuacha moyo nahisia kwenye majonzi, umeacha roho ndani ya moto pengine umeacha mwili umeondoka na roho yangu.....

Najiuliza, nini kilifanya unikimbie??, na nadhani hali yangu haikuwa nzuri, labda ndo chanzo.... Huenda ulipenda pesa,zawadi, hata kile kidogo nilichokupa ukaona hakifai na kuamua kunitoa moyoni mwako na kuzima ndoto yangu ya kuja kuishi nawe....
Labda pengine marafiki zako walikushawishi uachane namm, kwa kuwa sijawahi onekana kama nina future mbele ya marafiki zako...
Pegine ni utoto alifanya udate na wavaa vizuri na wenye hadhi zao na kuona mtoto wa mkulima sina cha kukupa maishani....

Moyo unamsiba bado na kichwa hakiwezi kaa sawa,...

Natumaini unaendelea vizuri. Ila huku umeacha mtu nusu, furaha na mazoea uliyonizoesha vimegeuka mzigo mkali uliomshinda babu mwenye mzigo wa kuni kupanda mlima.....

Najaribu kukusahau ila siwezi,najaribu penda naishia kuumiza wasio na hatia.najaribu kaa bila upendo nakuwa mpweke zaidi ya ukiwa wa yatima asie na wazazi wote, ila naimani ipo siku nitapata kitu cha muhimu na nitakuwa na uwezo wa kukuafford labda sahizi wewe ni too expensive kwangu na you are too far from my poor reach.....

All the lord love and protection be upon you......
@By Tanayzer lamo
Pole sana ndugu....
 
Listen up man, flowers grow everywhere. If you stop living in your sad memories, you might even find a huge garden with all the best flowers in it.

By the way, i hate flowers. Their beauty will deceive you, only to fade when you pluck them and they'll never bloom again.
 
Pole kibuti kinauma, kinauma mno.....yani usipokua mkakamavu kibuti kinaweza kukuacha wodini break drip ya glucose.

Ukiona dalili za kuachika heri uwahi ujiache mwenyewe na vicheko juu, ukisubiri kuachwa unahisi kama moyo umeacha mwili. Nilipigwa vibuti viwili enzi hizo SITASAHAU!!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom