Barua yangu kwa waajiriwa wote

Barua yangu kwa waajiriwa wote

Jaalut

Member
Joined
Jan 18, 2020
Posts
72
Reaction score
245
Tar 11/05/2020
S.l.p 255
Jamiiforums

Kwenu waajiriwa, mimi ni mzima wa afya sijui kwa upande wenu.

Lengo la barua hii ni kutaka kuwaambia ukweli mchungu ambao hutopenda kuusikia, lakini tambua hata sindano inauma lakini ni dawa kwa wagonjwa.

Kama kila siku unatega alarm ili uamke mapema uwahi kazini, na ukifika kazini unapangiwa cha kufanya, na huwezi kuondoka kazini mpaka muda uliopangiwa na boss wako ufike, samahani naomba utambue kwamba wewe ni MTUMWA WA FIKRA.

Ndio, wewe ni mtumwa wa fikra kwa kuwa unahangaikia kufanikisha ndoto za mtu mwingine, sasa vipi kuhusu ndoto zako?

Hivi hujisikii vibaya ukitaka kwenda msibani kumzika ndugu yako mpaka uombe ruhusa kwa boss, na ikitokea amekukatalia itakubidi usiende msibani hata kama aliyekufa ni Mama yako.

Ukweli usioujua ni kuwa "AJIRA NI SULUHISHO LA MUDA MFUPI KWA TATIZO LA KUDUMU" maana hata ukistaafu ni lazma maisha yaendelee, yaani ni lazma ule, unywe na uumwe pia, sasa je kama unategemea ajira tu unafikiri utaishije?

Waajiriwa wengi wanaogopa kujiajiri kwa kuwa wanaona kujiajiri ni hatari sana kwa afya za pesa zao, ila hawajui kuwa kusubiri mpaka ustaafu ndo ujiajiri ni hatari zaidi kwao.

Muda mzuri wa kujiajiri ni sasa hivi wakati bado kijana na unalipwa mshahara, hata ikitokea umepata hasara kwenye biashara bado utafidia katika mshahara unaopokea kila mwezi, wakati huo huo utakuwa unajifunza kutokana na makosa mbalimbali yaliyosababisha upate hasara.

Kumbuka huwezi kuwarithisha kizazi chako ajira ila unaweza kuwarithisha biashara zako.

Tafakari, chukua hatua

Wako katika kujenga taifa
Prazora Wirepa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba nikulize swali samahani kama ntakuwa nimekuudhi. Mimi si mwajiriwa nimejiajiri mwenyewe ila nimeajiri watu. Kwa kauli yako akisoma mfanyakazi wangu anaweza kuacha kazi naye akajiajiri mwenyewe. Sasa tukijiajiri wote nani atakuwa ameajiriwa?

Lazima kuwa na mgawanyiko wa kazi na unalipwa kulingana na maslahi unayoyafanyia kazi. Haimanishi kwa kuwa ni muajiriwa lazima utakuwa na maisha mabivu na ukiwa serious na kazi yako hata ikiwa binafsi huwezi ifungu utapoteza vitu vingi ikiwemo wateja.

Utakuwa na hela nyingi sana mzee unazungumza kwa dharau?
 
Kila jamii inahitaji walimu,wanajeshi,wauguzi,madaktari,maaskari na kada nyingine ili iweze kustablelize maisha....mkuu kuajiriwa ni utumwa lkn pia fikiria ukifungua kampun utahitaji watu wa kukufanyia kazi uwalipe....hivyo ndivyo maisha yalivyo wengine watajiajir na wengine wataajiri..........Ila na mm nachukia kuajiriwa...life is about choices!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukijiajiri wote nani atafanya kazi ambazo si za mwajiri?
Si kila aliyeajiriwa amepanga kufail kama unavyofikr,tupo waajiriwa wengi tu tunafanya mambo makubwa kuliko unavyofkr
Kuajiriwa sio dhambi, ila kutegemea ajira peke yake ni kosa kubwa.

Ukisoma uzi vizuri kuna kipande nimesisitiza kuwa waajiriwa wajaribu kujiajiri kipindi bado wapo kwenye ajira zao, wasisubiri mpaka wastaafu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naomba nikulize swali samahani kama ntakuwa nimekuudhi. Mimi si mwajiriwa nimejiajiri mwenyewe ila nimeajiri atu. Kwa kauli yako akisoma mfanyakazi wangu anaweza kuacha kazi nae akajiajiri mwenyewe...
Soma uzi wangu vizuri kiongozi.

Halafu mimi sina dharau, ila nimeandika ukweli mchungu ambao watu wengi hawapendi kuambiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Soma uzi wangu vizuri kiongozi...

Halafu mimi sina dharau, ila nimeandika ukweli mchungu ambao watu wengi hawapendi kuambiwa

Sent using Jamii Forums mobile app

Sasa kila mtu akiwa ameajiajiri tunaweza ishije mie nimesoma ila wewe binafsi unaweza dharau kazi ila ukidharau kwa waajiriwa wote unakuwa umekosea. Chukia wewe kama wewe kwani wenzako wanasomesha wanakula na wanafanya maendeleo makubwa kwa sababu ya kuajiriwa.

Haiwezekani kila mtu akajiajiri mwingine anaweza soma uzi wako akajiaminisha aache kazi akajiajiri akafeli utakuwa umempotosha sana. Kuajiriwa na kujiajiri yote sawa maana kuna watu wavivu hawataki kazi wanazurura. .
 
POLE SANA, HAKUNA TOFAUTI YA MWAJIRIWA NA MWAJIRI kuna vitu huajavifahamu, kitu muhimu hapo ni aidha kuwa MJASIRIAKAZI (Intrapreneur) au MJASRIAMALI(Entrepreneur) basi wote hawa huwa na uwezo wa mali mkubwa tokana na tabia zao.

Utumwa uko pale pale, aidha utakuwa mtumwa kwa wateja wako , bank, serikali KODI yoote ni UTUMWA TU Na wote ni maBOSS wako tu kama mwajiriwa

Kwa hakika na uzoefu wangu KUJIARI ndio utumwa mbaya sana, hujawahi ona tajiri anajinyonga wafanyakazi tena wake wanamshangaa ?

MSIDANGANYWE kama mnavyodanganya watu eti collage drop out wanatajirika na watu wanaamini hilo, HIZI NI FIKRA ZA KIMASKINI TU NA HAZITAKUSAIDIA

‘Motivational Speaker’ wanaweza kuharibu maisha ya waajiriwa - JamiiForums
 
Kuajiriwa sio dhambi, ila kutegemea ajira peke yake ni kosa kubwa.

Ukisoma uzi vizuri kuna kipande nimesisitiza kuwa waajiriwa wajaribu kujiajiri kipindi bado wapo kwenye ajira zao, wasisubiri mpaka wastaafu

Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wore wakijiajiri nani atafundisha wanao,nani atatengeneza hizo bidhaa unazoziuza, nani atakulinda dhidi ya maadui,nani atakutibu utakapo umwa wewe na familia yako? na mambo mengi.

Maisha lazima yawe na mgawanyo was majukumu,ndio maana mkeo kazi yake kukupikia wewe na wewe kutafuta hela ya ugali na mboga,tatizo Mkubwa la nchi za kiafrika Hanna mgawanyo sawia Katika keki ya Taifa ndio maana unaona watumishi wanahangaika.

Haya hivyo wahenga waliosema mshika mbili moja humponyoka hawakuwa wajinga,biashara yoyote ni usimamizi huwezi kuwa mtumishi at the same time use mfanyabishara mahili lazima utapwaya sehemu moja.
 
Nijikite hapo kwenye UHURU

Ndugu zangu wengi wamejiajiri katika biashara za maduka na vitu vidogo vidogo. Ila ikitokea amekufa mtu, Yaani wanakuwa wagumu Sana kutoka na kwenda msibani. Yaani wamekuwa watumwa wa biashar yao.

Imagine mtu anadaiwa na benk na tarehe zimefika, then unamwambia mtu kafa ( ndugu wa muhimu) sumbawanga uko na yeye yuko dar unafikiri ataenda mapema? Wengi wanaenda kwa kuchelewa Sana au wanaahirisha kabisa kwa visingizio mbalimbali.

Pia wengine wakifanikiwa kufika msibani hujikuta wanaondoka baada ya muda mfupi ili kuwahi biashara yake.

Upande mwingine, ushawi kufanya kazi ya kumshawishi mteja aingie kwenye duka lako wakati yapo mengine meengi yanayouza bidhaa hiyo hiyo. Pale ndipo utagundua kuwa mfanyabiashara Ni mtumwa wa mteja wake.

Kwa ufupi, mjasilia Mali Ni mtumwa kwa mteja, benki n.k

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kila mtu akiwa ameajiajiri tunaweza ishije mie nimesoma ila wewe binafsi unaweza dharau kazi ila ukidharau kwa waajiriwa wote unakuwa umekosea. Chukia wewe kama wewe kwani wenzako wanasomesha wanakula na wanafanya maendeleo makubwa kwa sababu ya kuajiriwa.

Haiwezekani kila mtu akajiajiri mwingine anaweza soma uzi wako akajiaminisha aache kazi akajiajiri akafeli utakuwa umempotosha sana. Kuajiriwa na kujiajiri yote sawa maana kuna watu wavivu hawataki kazi wanazurura. .
Kumbuka ajira ni suluhisho la muda kwa tatizo la kudumu.

Narudia, "kuajiriwa sio dhambi, ila kutegemea ajira peke yake ni kosa kubwa"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
POLE SANA, HAKUNA TOFAUTI YA MWAJIRIWA NA MWAJIRI kuna vitu huajavifahamu, kitu muhimu hapo ni aidha kuwa MJASIRIAKAZI (Intrapreneur) au MJASRIAMALI(Entrepreneur) basi wote hawa huwa na uwezo wa mali mkubwa tokana na tabia zao...
Ni utoto kufananisha utumwa wa muajiriwa kwa boss wake, na utumwa wa mjasiriamali kwa mteja wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijikite hapo kwenye UHURU

Ndugu zangu wengi wamejiajiri katika biashara za maduka na vitu vidogo vidogo. Ila ikitokea amekufa mtu, Yaani wanakuwa wagumu Sana kutoka na kwenda msibani. Yaani wamekuwa watumwa wa biashar yao...
Kuhusu suala la msiba nimetolea kama mfano tu, na nimekusudia Hasa misiba inayomgusa mtu moja kwa moja kama misiba ya wazazi na ndugu wa damu.

Ila ukiachana na msiba kiuhalisia kuna dharura nyingi ambazo anazipata muajiriwa, kuna kuumwa, kuuguza, na kadhalika, lakini dharura zote hizi atahitaji ruhusa ya boss wake kwanza



Sent using Jamii Forums mobile app
 
kila mtu yuko sahihi kutokana na mazingira na changamoto anazozipitia katika maisha yake hatujui wew mtoa mada umepitia nini katika maisha yako mpaka umefikia kuamua mahamuzi ya kujiajiri mwenyewe hupo sahihiii sana na wala usione walio ajiriwa wana matatizo ya kutokuwaza vizuri katika maisha yao.

ila twende mbele tuludi nyuma asilimia kubwa ya vijana wakibongo tunategemea ajira ili tuweze kujipatia mtaji wa biashara ila kumbuka mtoa mada kuna baadhi ya ajira ukipata unatulia tuli na kuanza kucheka mwenyewe kwa kile unacho kipata bila kutililika na jasho jingi ndg.
 
Ni utoto kufananisha utumwa wa muajiriwa kwa boss wake, na utumwa wa mjasiriamali kwa mteja wake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe pia unamawazo ya kitoto mbona. Umesema muajiriwa anapofanya kazi ya bosi Basi anamfaidisha bosi, Sasa mshahara anaolipwa unamfaidisha Nani?

Hivi mkuu ushawahi kuwa muajiriwa na Kisha ukajiajili? Tupe experience kidogo ya aina ya kazi uliyokuwa umeajiriwa na kazi unayofanya sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuhusu suala la msiba nimetolea kama mfano tu, na nimekusudia Hasa misiba inayomgusa mtu moja kwa moja kama misiba ya wazazi na ndugu wa damu...
Samahani unazungumzia ajira za aina gani mkuu?

Kama Ni serikalini, dharura zote ulizoweka hapo muajiriwa anachotakiwa Ni kutoa taarifa tu.

Pia hiyo ya msiba, hebu tuambie Ni lini muajiriwa wa serikali alikataliwa kwenda kumzika baba, mama, mke, mtoto, dada, Kaka, n.k.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom