Barua ya wazi kwako Mwalimu

Ms Yahaya

Member
Apr 14, 2022
6
12
Kwako Mwalimu.


Mwalimu, nakumbuka siku ya kwanza tulikutana shuleni kwako. Nikiwa kama mzazi niliyeingiwa na usasa na kuachana na mila za kale za kumfungia mwanangu wa kike ndani, nikaona nikukabidhi wewe mwalimu.

Nilifanya hivyo nikitegemea kuwa mwanangu angepata malezi bora katika mikono yako mwalimu. Ni mikono hiyo niliyoiamini na kuitegema bila kuwa na chembe ya dosari. Aaah! Mwalimu kumbe lilikuwa kosa kubwa sana nililolifanya bila kujua.

Wakati nyumbani kwangu nikimfundisha mwanangu jinsi ya kuwaepuka watu mafedhuri kama nyie, nikimlinda kwa hali zote hata kuweka zaidi ukaribu naye. Kumbe wewe mwalimu ulikuwa ukimfundisha namna ya kukwepa kila mtego nitakao uweka, ulimfundisha namna ya kuruka viunzi vyote nilivyomuwekea.

Nakumbuka siku ya kwanza mwanangu kunieleza habari zako na kufikisha malalamiko kwako ulidai mwanangu hataki kufanya kazi unazompa, hataki kukusikiliza, hana adabu ndo maana anakuwekea visingizio!!.

Bila kujua wala kufikilia nikaamini kile ulichonieleza wewe! Na adhabu akapata kutoka kwako namimi nikamuongezea nyingine na fimbo za kutosha nikakupa ruhusa umpe utakavyo. Aahg! Mwalimu.

Nilijua nakata mizizi ya kiburi na dharau alizokuwa nazo mwanangu kama ulivyonieleza kumbe napalilia magugu. Na sasa yamestawi vyema siwezi hata kukatisha katikati ya shamba langu.

Hivi unadhani nisingeweza kumfunza kile alichotakiwa kuapata shuleni!? ni kwakuwa tu nilitaka mwanangu awe katika mfumo unaotambulika ili hapo baadae niweze kunufaika.

umefanya udhalimu wooote ukaona haitoshi na mimba ukampa!! bado hilo likinifikilisha ukaona uikatae kabisaa! mwalimu ni wapi tunaelekea.

Naskia una mke na watoto wawili. hivi! ulishawahi kukaa chini na ukafikilia hichi ulichokitenda siku kikimpata mwanao utajiskiaje!!?
na vipi mkeo unamuangaliaje kwanza!! kwa macho mawili!? moja!? au kwa kutumia kisogo!?

Najua sina pa kukupeleka kutokana na mifumo ya kihuni mliyojiwekea lakini amini amini nakwambia hili chozi halitapotea bure. ni aidha hapahapa tulipane basi likishindikana hilo hata kule tutakapofikia baada ya kufukiwa katika nyumba zetu za milele nako utalipa tu! nasema utalipa tu!!

Eeh! Mwalimu!!!.
 
Ukitoa udaktari kazi ya Ualimu ndio kazi ngumu mno hata pakupeleka malalamiko wanakosa

Mitego mingi

Lawama nyingi na zinatoka kila kona

Wanafanyishwa kazi kuliko uhalisia malipo yao huku wakiwafariji na posho

Mwalimu ni mhimu kwenye jamiii

Ila alifanya haya nadhani aliyafanya nje ya ualimu wake hatua zifute mkondo wake
 
Back
Top Bottom