Barua ya wazi kwa Rais kuhusu ujenzi wa barabara ya Msongola

Nendubotho Sunguya

Senior Member
Oct 9, 2019
126
112
Tumeamua kuchanga kutengeneza barabara ya Msongola iwe kiwango cha lami tusaidiane kuisambaza hii barua ifikie watu wote hasa mh Rais John Joseph Magufuli

NEEMA JOHN MOLLEL

KITONGA-MSONGOLA,

0746715216.

DAR-ES-SALAAM.​

RASI WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,

DAR-ES-SALAAM.

YAH: KUCHANGIA UJENZI WA BARABARA YA MSONGOLA ILALA DAR ES SALAAM IWE KIWANGO CHA LAMI.

Tafadhali rejea kichwa cha habari hapo juu. Barua hii nimeielekeza ikulu kwa sababu ndio sehemu ya juu inayotuunganisha pamoja na viongozi wengine wote ikiwemo mkuu wa mkoa, mkuu wa wilaya ya temeke na Ilala ambazo zinaunganishwa na barabara hii, lakini kikubwa kwa wananchi wanaoishi Msongola, Kitonga, Mbande, Kisewe pamoja na wanaopita njia hii kwenda Chanika na Mvuti, pamoja na wafanya biashara wote waletao bidhaa zao maeneo tajwa hapo juu.

Rais wetu mpendwa John Pombe Magufuli, sisi wananchi wa Kitonga, Mbande, Msongola na Kisewe na maeneo mengi yanayoungwa na barabara hii tunapata tabu sana na hii barabara kwa nyakati zote, kipindi cha jua ni makorongo na vumbi zito na kipindi cha mvua ni madimbwi pamoja na tope lisiloolezeka. Ni tabu isiyoelezeka. Kuna mama alishawahi jifungua barabarani kwa kushindwa kufika hosipitali kwa wakati, nayo magari ni shida kufika huku hivyo kupekelea kuchelewa maeneo ya kazi na pia gharama kubwa ya usafiri.

Tunajua fika kwa sasa kuna miradi mingi ya maendeleo inayoendelea kujengwa ndio nikapata wazo hili la kuchangia kiasi tutakachofikisha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii kwa hiyari. Nilitaka kutafuta namna ya kuendesha mikutano ya hadhara tutafute namna ya kuchangisha pesa hizo maana kwa hali ya barabara hii hakuna mwananchi atakayekataa kujitoa kwa namna atakayoweza, kabla ya hapo nimeona niandike barua hii ya wazi tuisambaze kwenye vyombo vya habari ili kuwapa taarifa wananchi ili tupate muongozo wako maana kwa mimi peke yangu bila msaada taarifa haitasambaa vizuri.

Mheshimiwa Rais kama tunachangia maharusi mamilioni ya pesa na barabara tutaweza tena kwa moyo wote, hivyo tunakuomba utupe muongozo lakini kikubwa tunaomba Baraka zako na sapoti kutoka kwako, Maana tunajua ni pesa nyingi inahitajika kwenye ujenzi wa kilomita chache tu lakini kwa kipande hichi ambacho kwa makadirio ni kama kilomita sita hivi, hata tukipunguza kilomita moja tutakua tumepunguza adha tunayopata.

Nimejaribu kuongea na baadhi ya wananchi wenzangu wanaonaje kama tukijichanga kwa ajili ya ujenzi wa barabara kila mmoja anasema yupo tayari hata kushika sururu, maana huku tukiona mvua tunawaza barabara itapitika? Wakati wenzetu wanawaza wakalime na kuifurahia mvua.

Barua hii pia imfikie mkuu wa mkoa Paul Mkonda, mkuu wa wilaya ya Ilala pamoja na mbunge wa Jimbo hili la Ukonga ambako barabara hii ipo.Tunaomba muongozo waheshimiwa hii barabara tangu enzi na enzi ni korofi.

Mwisho kabisa barua hii ifikie vyombo vyote vya habari, magazeti, televisheni na mitandao yote ya kijamii, tunaomba mtusaidie kusambaza barua hii kwa watanzania wote kwani tunaitaji sapoti ya kila mtanzania, tutatangaza tarehe rasmi ya kuanza mikutano na harambee mbalimbali kama tukipata Baraka kutoka kwa viongozi wetu hasa Rais wetu John Joseph Pombe Magufuli
 

Attachments

  • NEEMA JOHN MOLLEL.docx
    16.1 KB · Views: 3
  • NEEMA_JOHN_MOLLEL.pdf
    7.7 KB · Views: 1
  • 20191122_072822.jpg
    20191122_072822.jpg
    200.9 KB · Views: 4
Hongereni , nadhani itamfikia mh Rais

Ni msikivu atawachangia zaidi kukamilisha hiyo Barabara


Maendeleo hayana vyama
 
Hali ilivyo kwa sasa barabara yetu ya mbande msongola.
 

Attachments

  • 20191122_072822.jpg
    20191122_072822.jpg
    200.9 KB · Views: 4
  • 20191122_072819.jpg
    20191122_072819.jpg
    229.5 KB · Views: 4
Yote haya chanzo chake ni ujenzi holela...

Wananchi wanaenda kujenga maeneo serikali imepanga kuyaendeleza miaka 20 /30 mbele...
 
Yote haya chanzo chake ni ujenzi holela...

Wananchi wanaenda kujenga maeneo serikali imepanga kuyaendeleza miaka 20 /30 mbele...
Eneo la barabara wala halijaguswa kabisaaa.
Na hifadhi ya barabara ni kubwa sana.tatizo hii barabara magari yanapita mengi na watu ni wengi ila barabara ni mbovuuu hakuna mfano.
 
Maana yangu mmejenga mahali ambapo mpango wa maendeleo wa serikali pengine bado kufika...

Mtaishia kutengenezewa barabara kwa kiwango cha changarawe/udongo
Eneo la barabara wala halijaguswa kabisaaa.
Na hifadhi ya barabara ni kubwa sana.tatizo hii barabara magari yanapita mengi na watu ni wengi ila barabara ni mbovuuu hakuna mfano.
 
Haya ndio maendeleo.Sio ule ulimbukeni wa kupukutisha hela kwa send off na harusi za anasa kama mazuzu na kuacha kuchangia mambo yenye tija kama hili.Hongera dada Neema.
 
Maana yangu mmejenga mahali ambapo mpango wa maendeleo wa serikali pengine bado kufika...

Mtaishia kutengenezewa barabara kwa kiwango cha changarawe/udongo
Ni kilometa chache tu kutoka chamazi complex ilipo.kwa kifupi hii barabara ina historia.wengine wanadai ni pesa zilipigwa enzi za JK.
ni barabara ya kwenda chanika eneo la mjini kabisa.ni barabara yenye wakazi lukuki
Sio makazi mapya.
Tangu enzi za mapa wanapiga danadana kuotengeneza na wakazi walikua wengi tu
 
Back
Top Bottom