Barua ya wazi kwa Rais kuhusu korosho

sharifusaid

Senior Member
Jan 24, 2015
107
63
BARUA YA WAZI KWA MH. RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, JOHN POMBE MAGUFULI KUHUSU OPARATION KOROSHO 2018.
NA RAMA ALLY NAHONHO, Mkulima na mtoto wa mkulima wa korosho.
Mheshimiwa rais, kwanza kabisa nikupe pole kwa kazi ngumu ya kuwatumikia wananchi hasa wanyonge. Natambua kazi hii ni ngumu na wewe binafsi umewahi kukiri hilo hadharani mara kadhaa.
Aidha, nikushukuru wewe binafsi kwa kukubali serikali unayoiongoza kununua korosho zote kwa msimu huu wa mauzo baada ya matarajio ya uuzaji wa korosho kutokidhi kiu ya wakulima na hali halisi ya gharama za uendeshaji wa zao hili muhimu kwa maendeleo ya viwanda na ujenzi wa TANZANIA ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Korosho inachangia sana fedha za kigeni kwa taifa letu. Kwa mfano, kwa miaka mitano ya karibu, korosho ilichangia kama ifuatavyo.
2013/14 dola million 133.4, mwaka 2014/15 dola million 252.8, mwaka 2015/16 dola million 186.5, mwaka 2016/17 dola million 342.6 na mwaka jana dola million 585.5 na kuwa zao linaloongoza TANZANIA kwa kuliingizia TAIFA fedha nyingi za kigeni.
Hivyo, uamuzi wako huu unalenga pamoja na mambo mengine, kulinda thamani ya zao la korosho sokoni na kuwalinda wazalishaji wake ili kusudi miaka ijayo, waendelee kuzalisha.
Uamuzi huu, sio tu unakutambulisha wewe binafsi na serikali yako kama serikali ya wanyonge, lakini pia inatuma salaam kote duniani kuwa, TANZANIA si shamba la bibi la kuchuma na kuwaonea wakulima masikini.
Mheshimiwa Rais, wakati unatangaza uamuzi ule, jukumu la kuratibu na kununua korosho liliwekwa chini ya bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko kwa kushirikiana taasisi zingine 10 na zote zipo field.

HALI YA UNUNUZI ILIVYO HADI SASA.
Mheshimiwa Rais, mikoa saba inayolima korosho, ikiongozwa na MTWARA NA LINDI, ilitarajia mwaka huu wa kilimo 2018/19 tukusanye tani 275,191 na kilo 300 za korosho huku mkoa wa mtwara pekee ukitarajia kukusanya tani 148,000.
Aidha, hadi kufikia tarehe 26/11/2018, korosho ambazo zimeshakusanywa na kutunzwa maghala makuu ni tani 143,245 na kilo 572.
Hii ina maana kuwa, korosho zaidi ya tani laki moja bado zipo majumbani, mashambani au kwenye vyama vya ushirika.
Mheshimiwa rais, mchakato huu wa ununuzi hadi sasa umekwama na hauleti matumaini kabisa ya kukamilika ulipaji au kama utakamilika, basi ni kwa kuchelewa sana hali inayotishia usalama wa watu wetu na uzalishaji kwa msimu wa mazao ujao.

Aidha, kwa wakulima umeongeza njaa, mateso na sonona kwa sababu zifuatazo.
TEAM ZA UHAKIKI KUWA NA KASI NDOGO YA UHAKIKI NA ULIPAJI.

Mheshimiwa Rais, pamoja na kutambua umuhim wa uhakiki wa taarifa za wakulima, lakini zoezi hilo limekuwa na kasi ndogo ambayo kama haitaongezwa, mwisho waske utakuwa mbaya sana.

Kwa mfano, kwa mikoa ya lindi, mtwara na ruvuma, timu 11 za uhakiki zenye watu kati ya watatu na sita zimeundwa.

Tukichukua wastani wa juu kabisa wa watu sita kwa timu moja, ina maana kwamba, tuna wahakiki 66 tu mikoa yote mitatu.

Kwa korosho zilizopo maghala makuu pekee kama ilivyoanishwa huko juu, tunahitaji kila mtu mmoja ahakiki kilo 2,170,387 sawa na tani 2170 na kilo 387.

Kwa sabau hii, ndio maana kwa mikoa hii mitatu, hadi kufikia tarehe 26/11/2018, ni tani 4017 na kilo 551 tu ndio zimehakikiwa (siku 18) sawa na asilimia 2.8046 ya korosho zote zinazohitaji kuhakikiwa ambazo zipo maghala makuu.

Hapa sijajumlisha zile tani laki moja ambazo bado hazijakusanywa hadi sasa.
Hii maana yake ni nini ?

Tunahitaji siku 642 sawa na mwaka mmoja na miezi nane kukamilisha zoezi la uhakiki tu.

Ni sawa na kusema, zoezi litakamilika mwaka 2020 mwezi wa saba kwa kasi ya sasa.

KASI YA ULIPAJI KUTORIDHISHA.

Mheshimiwa rais, kwa makusanyo ambayo tayari yapo ghala kuu (achana na tani laki moja ambazo hazijakusanywa na zimekwama majumbani, shambani na kwenye vyama vya msingi), ambazo ni sawa na tani 143,245 ; kwa bei ya 3300 tu ambayo inatakiwa iende kwa mkulima (143,245x1000x3300) ni sawa na billion 472.709.

Kiasi ambacho hadi kufikia tarehe 29/11/2018 kwa mujibu wa waziri Hasunga kilicholipwa ni billion 22 tu sawa na asilimia 4.7 tu ya pesa yote inayotakiwa kulipwa kwa korosho zilizopo maghala makuu tu.

Ukijumlisha na zile ambazo hazijakusanywa, idadi ya tani ni (275,191.3x1000x3300) sawa na billion 908.131. ukichukua pesa iliyolipwa hadi kufikia tarehe 29/11/2018 ya billion 22, ni sawa na asilimia 2.4.

Kwa utaratibu huu, kama siku 18 tumelipa billion 22 tu, ina maana kuwa, ili kila mkulima alipwe, tunahitaji siku 642 sawa na mwaka mmoja na miezi saba.

Waziri jana tarehe 29/11/2018 aliwaambia wakulima kuwa, anatarajia kuongeza kasi ya ulipaji hadi kufikia billion 4 kwa siku sawa na billion 120 kwa mwezi.

Ukichukua makadirio ya makusanyo kama ilivyoanishwa huko juu ya tani 275,191.3 zenye thamani ya shilingi billion 908.131 kwa bei ya 3300 kwa kilo, tunahitaji miezi saba na siku 15 kukamilisha zoezi.

Hii ni sawa na kusema, kama kweli kauli ya waziri itatekelezwa, zoezi litakamilika mwaka 2019 mwezi wa sita… (miezi mitatu kabla ya msimu mpya wa uvunaji kuanza).

UHAKIKI KUCHUKUA SURA MPYA AMBAYO WEWE BINAFSI HUKUELEKEZA NA KULETA SINTOFAHAMU.

Mheshimiwa Rais, inawezekana kabisa baadhi ya watendaji wako wakataka kukukwamisha kwenye mchakato huu wa ununuzi.

Zoezi la uhakiki, lililenga hasa kubaini endapo taarifa za mkulima za mauzo ya korosho chamani ni sahihi na zile zilizopo kwenye orodha ya malipo.

Aidha, lililenga kuhakikisha mtu anayelipwa ni yule tu aliyeuza korosho.
Lakini cha kusikitisha, watendaji wako uliowatuma, wamekuja na aina mpya ya uhakiki ambayo hatujui hasa dhamira yake ni nini.
Kwa mfano ;
Mtu mwenye uzalishaji unaoanza na kilo 1501 kulazimika kuonesha shamba na kutolipwa kwa hatua ya awali. Hii inashangaza kidogo. Ni ama wahakiki hawajui korosho au wameamua kutouliza au wamekuja na agenda ya kuwafilisi wakulima. Mheshimiwa rais, hekari moja ya korosho kitaalam ina mikorosho 25 na mkorosho mmoja mkubwa unaweza kukupa gunia moja, lenye ujazo wa kilo 100.
Tuchukue watani wa kilo hamsini tu kwa mkorosho. Mtu mwenye hekari moja, anaweza kuzalisha kilo 1250.
Wazee wetu huku mtwara, wanamili hekari kuanzia 10 hadi 100. Hii ina maana kuwa, wazee wetu wanaweza kuzalisha tani kuanzia 12 hadi 100 sawa na kilo 12000 na kuendelea.

Mifano ipo mingi sana ;
Nanyamba tunao akina mzee mauji, akina mzee mdoba, mzee tall na wengine. hawa wanakusanya hadi tani 50 kwa mwaka.

Inasikitisha sana wahakiki wanapogeuza mavuno manono kuwa uhaini.
Wazee wetu wanaovuna kiasi kikubwa cha korosho wanalazimika kukaguliliwa mashamba yao.

Hawa wanachukuliwa orodha yao (wanaoanzia kilo 1501) na kutakiwa kuambatana na wahakiki hadi shambani.

Tunajiuliza, lengo hasa ni nini ?
Serikali haitaki watu wawe na korosho za kutosha ?
Kuzalisha sana imekuwa nongwa hadi wasulubiwe na kutakiwa kukaguliwa mashamba ?
Kwa wahakiki wale 66, zoezi hili litachukua muda gani ?
Uliwaagiza washinde mashambani au wanunue korosho ?
Baadhi yao wanadai wanazuia kangomba, hivi kweli kangomba anazuiliwa kwa kukagua shamba ?
Mkoa wa mtwara kwa mfano, kila mtu karibia analo shamba, hadi kupelekea mkoa kukosa kabisa misitu. Hivi kweli watatembelea mashamba yote ?

Mheshimiwa rais, kangomba inachukiwa na kila mpenda maendeleo. Lakini mbinu ya kuhakiki mashamba haitazuia kangomba.
Tunashauri serikali kama ina dhamira ya kukomesha kangomba ifanye yafuatayo.

Serikali itoe mikopo nafuu na kwa wakati kwa wakulima ili kuwezesha zoezi la palizi
Serikali igawe pembejeo na viuatilifu kwa wakati
Serikali ihakikishe wanunuzi kwa misimu ijayo inalipa korosho kwa wakati ili kuwezesha zoezi la uendeshaji wa kilimo na ukusanyaji
Serikali iweke bima ya bei ili kulinda anguko la bei ya korosho.
Kama haya yatafanyika, kangomba itajifia yenyewe.

Kama haya hayatafanyika,hata kama polisi watasambazwa kila nyumba kulinda, wakulima watauza tu kangomba kwa sababu ya njaa, gharama za uendeshaji, palizi na viuatilifu. Mtu hawezi kukaa miezi mitatu hajalipwa na mtoto anaumwa au ndani hakuna chakula akaacha wanawe wafe wakati kangomba wananunua. Watauziana hata chooni na watalindana.

Mheshimiwa rais, zoezi hili la ukaguzi wa mashamba ni la ajabu na halina matokeo yanayotarajiwa.

ATHARI ZA UCHELEWESHWAJI WA MAKUSANYO, UHAKIKI NA ULIPAJI.

MAKUSANYO.
Kama ambavyo nimeanisha hapo juu, zoezi la makusanyo kwas asa limekwama kwa sababu hakuna maghala ya kuhifadhi na yaliyopo yamejaa, hivyo, korosho ani laki moja hazijakusanywa hadi sasa.
Hii ina hatari sana hasa msimu huu wa mvua unaoanza.
Korosho zitanyeshewa na hazitakuwa na ubora na hivyo serikali kupata hasara.

UHAKIKI NA ULIPAJI.
Athari za kuchelewa uhakiki sio tu kunachelewesha ulipaji, lakini pia, inaibua taharuki na kuchochea uvunjifu wa aman iwa watu wetu. Mtu mwenye njaa hana dhamana na anaweza kufanya uhalifu ili kujikimu.
Aidha, zoezi la uhakiki limechukua sura mpya inayoleta mashaka ya watu kudhulumiwa mali zao (korosho).

Kucheleweshwa kwa ulipaji kumeongeza sana ukali wa maisha na inatishia uzalishaji kwa msimu unaofata.

HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
Kufuatia maelezo hapo juu, nashauri yafuatayo yafanyike.

Timu za uhakiki ziongezwe ikiwezekana mara tatu yake. Timu 11 za sasa ziongezeke ziwe 33 ili kuongeza kasi ya uhakiki. Makatibu wa AMCOS wanaweza kuwa msada hapa kwa kuwa kwanza ndio wenye wakulima lakini pia, ni wazoefu.
Uhakiki wa mashamba ukomeshwe mara moja kwani hauna tija na unalenga kuwatesa wazalishaji wakubwa.
Watu wenye kilo kuanzia 1501 kwa cheti kimoja ambao kwas asa ndio wanaohakikiwa mashamba yao waanze kulipwa bila ubaguzi kama ambavyo mh. Rais ulielekeza kwa sababu inayofanana na hapo juu.
Mheshimiwa rais, kwa kuwa uwezo wetu wa uhifadhi wa korosho ni mdogo (tunaweza kuhifadhi tani 150,000 tu) huku makusanyo yakiwa tani 275,000, huku uwezo wa viwanda vyetu (binafsi na vya umma) kwenye ubanguaji ni tani 11,142 (utilized capacity ya viwanda vyote nchini) sawa na asilimia 26 tu ya installed capacity ya tani 42,200 ; nashauri kwa faida ya taifa letu, serikali iridhie wateja 7 walojitokeza kununua korosho serikalini ikiwemo makampuni ya ndani na nje ya nchi. Hawa wapewe kiasi kinachozidi (bakaa) huku tukisubiri ukarabati wa miundombinu kwenye viwanda vya ndani na kuanza mara moja zoezi la kubangua na kuziongeza thamani korosho zetu.

Mwisho, nikuombe tena kwa unyenyekevu mkubwa uendelee kutupigania.
Sisi wakulima tuna imani kubwa sana na wewe na tunaamini kupitia barua hii ya wazi kwako, na kupitia forums zingine ikiwemo timu yako ya wataalam, changamoto zitapatiwa ufumbuzi.
 
Kuna ulazima wa kutambua kwamba mambo ya biashara hayaendi kwa UBABE bali kwa maelewano kati ya muuzaji na mnunuzi; bila ya makubaliano hakuna biashara!!!
 
Wacha waisome naambaa eeeeeh!

Waisome naambaa eee

Sisi wacha mbeeele kwa mbeleeeeee

Hatunywi suumuu,hatujinyongiiiiiiii

Sisi wacha mbele kwa mbeleeeeeeeeee!!!!!!
 
Kweli Dunia ina Mambo... Kumbe huko Ntwara ni Vituko na Viroja tu.. Bora Jana kuliko leo
 
Swala la Bima kwa wakulima ni muhimu sana kwa wakulima korosho na wakulima wengine wote.

Sababu bei za mazao huwa zinapanda na kushuka.

sharifusaid, umeandika na kushauri vizuri sana, matatizo, athari zake, mapendekezo jinsi ya kutatua matatizo. Natumaini ushauri wako utafanyiwa kazi.
 
Wewe utakuwa umetumwa, ni kibaraka wa wazungu. Sisi tunatembea vifua mbere wewe unaleta majungu
 
Sasa aingilie mara ngapi jamani kwani hao anaoteua kumsaidia ni MATAAHIRA? Hivi nchi hii sasa hivi zao linalolimwa ni korosho peke yake au wakulima wa mazao mengine hatuna changamoto hadi nguvu zote za serikali zielekee kwenye korosho? Iundwe wizara ya korosho basi kama hili zao lina upekee kushinda mengine ili wizara ya kilimo itukumbuke na sisi tunaolima mazao mengine. Korosho, korosho kuja kutahamaki michezo tu kama michezo mingine ya siasa.
 
Hongera sana mkuu kwa Uzi nzuri na wenye mashiko naamini mkuu atalifanyia kazi hili

Nimesoma hii barua na mwisho machozi yamenitoka.
Biashara na siasa ni kama ardhi na mbingu.
Kamwe haviwezi kukutana.
Ok poleni sana ndugu zetu wana ntwara.
 
Kwa sisi tunao peleka biashara huko tunasoma namba vibaya labla ukopeshe malipo mwakani
 
Bwana NAPE hakuna cha pole na kazi wala nini, iyo ilikuwa incriment yetu watumishi imeenda kununua korosho, tulieni ivyo ivyo, naomba wahakiki wa punguzwe kutoka 66 mpaka 10 kubana matumizi
 
Back
Top Bottom