Standards Person
JF-Expert Member
- Apr 22, 2021
- 673
- 859
Mh. Rais ninakusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Hongera sana kwa kazi nzuri ya kulijenga taifa. Ninaandika hapa maana ulikiri kwamba unapitia mitandao ya kijamii.Pia kwakua umejipambanua kwamba ni mpenda haki na hutaki makusanyo ya uonevu na mabavu.
Wananchi wa Tanga mjini wanajambo lao na jambo hilo ni kilio dhidi ya mkurugenzi wa jiji Daudi Mayeji. Amefanya uonevu mkubwa sana kwa wananchi. Amepora viwanja vya watu. Watu wamekufa kwa presha na mkuu wa wilaya aliambiwa kwenye mkutano. Je, hata waliopoteza mali zao wakirudishiwa vipi hao waliopoteza wazazi wao? Zimebomolewa nyumba za watu maeneo ya masiwani hata kabla ya mahakama kutoa tamko. Maeneo ya kichangani,amboni na kasera ni vilio.
Wenye hela ndio wamepewa viwanja na wasiokua na uwezo wanaitwa wavamizi. Mtu anamiliki kiwanja chake kihalali na ameingiza hadi maji lakini mipango miji wanauzatu hawaangalii eti kwakua wametumwa na mteule wa Rais. Wananchi wamelalamika mpaka kwa mkuu wa mkoa na katibu tawala lakini hakuna hatua inayochukuliwa dhidi ya mkurugenzi huyo. Kuna jamaa wa ardhi anaitwa Tony ni mkorofi mlarushwa na mwizi wa viwanja vya watu. Maskini akilalamika anaambiwa kalete uthibitisho na akionesha wanachukua wanapoteza kisha unashangaa eneo linajengwa na tajiri.
Mh.Rais malalamiko yalifika hata kwa mwenyekiti wa CCM mkoa ndugu Shekifu. Lakini mkurugenzi huyo hasikii la mtu eti yeye ni mteule wa Rais. Viwanja vimeuzwa na wamepelekewa hela mkononi wala sio kwa kulipia benki.
Takukuru nao ndio hivyo tena,ingawaje bosi wao alisimamishwa sababu siijui lakini bado mambo hayajakaa sawa. Kilichopo nikwamba akija mtumishi yoyote anawahi kulambishwa ili atulie.
Ummy Mwalimu analijua sana hili, Jafo anajua habari za huyo jamaa yake Daudi. Lukuvi alikuja maji yakawa kina kirefu yakamshinda akaondoka. Wananguvu ya ziada wanatumia lakini kwa kua tunayasema haya basi nguvu hiyo iende zake na wanaotaka kuwachunguza watumeni watafika na kuondoka salama.
Ummy alikua anaogopa kwani alihofia labda kuenguliwa kwenye uchaguzi. Sasa amekua Tamisemi anasimamisha wakurugenzi halmashauri nyingine yakwake anaiacha.hatendi haki tena anakuaibisha mh Rais.
Mh. Rais Tanga hawatendewi haki kwani walioletwa hawapo kwaajili ya wanatanga na wanaotakiwa kuwasemea wanatanga wameungana na wanyanyanyi.
Mh. Rais itazame Tanga kuanzia juu hadi chini na mchunguze mkurugenzi wako ni mbadhirifu hakuna shaka. Wamekaa hapa muda mrefu wanapigatu dili hata wakija na hakuna wa kuripoti haya mambo ipasavyo kwani waandishi wa habari Tanga hawapo huru
Mh. Rais kipimo cha uadilifu kwa Ummy nihuyo mkurugenzi wake, japo wanajuana lakini asipompumzisha akapisha uchunguzi hata wale wawili mh. Rais amuru tu warudishwe.