Barua ya wazi kwa Mh. Rais Samia

Standards Person

JF-Expert Member
Apr 22, 2021
673
859
Mh. Rais ninakusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,

Hongera sana kwa kazi nzuri ya kulijenga taifa. Ninaandika hapa maana ulikiri kwamba unapitia mitandao ya kijamii.Pia kwakua umejipambanua kwamba ni mpenda haki na hutaki makusanyo ya uonevu na mabavu.

Wananchi wa Tanga mjini wanajambo lao na jambo hilo ni kilio dhidi ya mkurugenzi wa jiji Daudi Mayeji. Amefanya uonevu mkubwa sana kwa wananchi. Amepora viwanja vya watu. Watu wamekufa kwa presha na mkuu wa wilaya aliambiwa kwenye mkutano. Je, hata waliopoteza mali zao wakirudishiwa vipi hao waliopoteza wazazi wao? Zimebomolewa nyumba za watu maeneo ya masiwani hata kabla ya mahakama kutoa tamko. Maeneo ya kichangani,amboni na kasera ni vilio.

Wenye hela ndio wamepewa viwanja na wasiokua na uwezo wanaitwa wavamizi. Mtu anamiliki kiwanja chake kihalali na ameingiza hadi maji lakini mipango miji wanauzatu hawaangalii eti kwakua wametumwa na mteule wa Rais. Wananchi wamelalamika mpaka kwa mkuu wa mkoa na katibu tawala lakini hakuna hatua inayochukuliwa dhidi ya mkurugenzi huyo. Kuna jamaa wa ardhi anaitwa Tony ni mkorofi mlarushwa na mwizi wa viwanja vya watu. Maskini akilalamika anaambiwa kalete uthibitisho na akionesha wanachukua wanapoteza kisha unashangaa eneo linajengwa na tajiri.

Mh.Rais malalamiko yalifika hata kwa mwenyekiti wa CCM mkoa ndugu Shekifu. Lakini mkurugenzi huyo hasikii la mtu eti yeye ni mteule wa Rais. Viwanja vimeuzwa na wamepelekewa hela mkononi wala sio kwa kulipia benki.

Takukuru nao ndio hivyo tena,ingawaje bosi wao alisimamishwa sababu siijui lakini bado mambo hayajakaa sawa. Kilichopo nikwamba akija mtumishi yoyote anawahi kulambishwa ili atulie.

Ummy Mwalimu analijua sana hili, Jafo anajua habari za huyo jamaa yake Daudi. Lukuvi alikuja maji yakawa kina kirefu yakamshinda akaondoka. Wananguvu ya ziada wanatumia lakini kwa kua tunayasema haya basi nguvu hiyo iende zake na wanaotaka kuwachunguza watumeni watafika na kuondoka salama.

Ummy alikua anaogopa kwani alihofia labda kuenguliwa kwenye uchaguzi. Sasa amekua Tamisemi anasimamisha wakurugenzi halmashauri nyingine yakwake anaiacha.hatendi haki tena anakuaibisha mh Rais.

Mh. Rais Tanga hawatendewi haki kwani walioletwa hawapo kwaajili ya wanatanga na wanaotakiwa kuwasemea wanatanga wameungana na wanyanyanyi.

Mh. Rais itazame Tanga kuanzia juu hadi chini na mchunguze mkurugenzi wako ni mbadhirifu hakuna shaka. Wamekaa hapa muda mrefu wanapigatu dili hata wakija na hakuna wa kuripoti haya mambo ipasavyo kwani waandishi wa habari Tanga hawapo huru
Mh. Rais kipimo cha uadilifu kwa Ummy nihuyo mkurugenzi wake, japo wanajuana lakini asipompumzisha akapisha uchunguzi hata wale wawili mh. Rais amuru tu warudishwe.
 
Yasiwe majungu mkuu,wamesikia ni watu makini,
Sio majungu mkuu,tena yapo mambo kibao anayowatendea raia sijayaweka hapa. Namvutia pumzi Ummy aaipochukua hatua wiki ijayo nitaenselea kumdokeza mh.Rais uozo wa huyo mkurugenzi.

Alisha lalamikiwa muda mrefu sana huyo sema ana nguvu zake za kuyazima mambo. Nitaendelea kuelezea wizi ubabe ultoaji rushwa wake hadharani.

Kama Ummy anachukua maoni ya wananchi kutoka halmashauri nyingine kwanini kwenye halmashauri yake hachukui maoni?
Akiendelea kua kimya utatolewa ufafanuzi zaidi nikwanini hamshuhulikii. Watu wakae mkao wa kula
 
Sio majungu mkuu,tena yapo mambo kibao anayowatendea raia sijayaweka hapa. Namvutia pumzi Ummy aaipochukua hatua wiki ijayo nitaenselea kumdokeza mh.Rais uozo wa huyo mkurugenzi.

Alisha lalamikiwa muda mrefu sana huyo sema ana nguvu zake za kuyazima mambo. Nitaendelea kuelezea wizi ubabe ultoaji rushwa wake hadharani.

Kama Ummy anachukua maoni ya wananchi kutoka halmashauri nyingine kwanini kwenye halmashauri yake hachukui maoni?
Akiendelea kua kimya utatolewa ufafanuzi zaidi nikwanini hamshuhulikii. Watu wakae mkao wa kula
Naona kaanza na Bumbuli🏌🏌🏌
 
Naona kaanza na Bumbuli🏌🏌🏌
Hapo hajaanza nao,amewataka wajitathmini. Sasa hapo ndipo unapojua kwamba bado anaishi ulimwengu tusioutaka. Mtu anazembea unamwambia ajitathmini. Yaani simuombei Ummy mabaya lakini anguko lake naliona Tamisemi. Ujamaa mwingi kazini. Tanga pameoza na kama anabisha achukue maiki aseme mkurugenzi wa Tanga hana shida. Wanaojua shida ilipo wataonesha. Kila aina ya rushwa unayoijua Tanga imeshamiri kwenye halmashauri ya Tanga. Hapa hatujaelezea watu kufukuzwa kazi ili wake zao washuhulikiwe vizuri. Yaani Ummy wewe....mchekee huyo halafu shuhulikia wengine
 
Sidhani kama ukiachia mbali hao wenye migogoro ya viwanja na ambao hawajawahi kwenda kwa DC kama waliobaki wanamjua DC. RC anaonekana kwenye gari akipita au wakija viongozi wa kitaifa.
Rais apeleke watu Tanga wenye uchungu na watu wa Tanga
 
Tanga Tanga Tanga kunani paleeeee eeee mbona kila kitu pale kimekuufa
Ndio itazidi kudidimia kwani Ummy amewekwa na huyo Daudi. Daudi nae leo ananyenyekea kwa Ummy asitumbuke.
Hata imeonekana mkurugenzi huyo kushiriki kwenye upokeaji wa mashine za wavuvi. Mkurugenzi huyo Ummy hamtoi bali wanatanga wasubirietu huruma ya mh. Rais
 
Wakurugenzi sii ndio walikuwa mastermind wa kuiba kura za uchaguzi kwenye maeneo yao,.
Ummy=mkurugenzi=tanga mjini
Sio kwamba ummy hafahamu ilo tatizo pengine ametulia kulipa fadhila
 
Wakurugenzi sii ndio walikuwa mastermind wa kuiba kura za uchaguzi kwenye maeneo yao,.
Ummy=mkurugenzi=tanga mjini
Sio kwamba ummy hafahamu ilo tatizo pengine ametulia kulipa fadhila
Ummy anajua kabisa watumishi ambao wake zao wamechukuliwa na wanaume hao walipoleta ukali nyumbani wakabebeshwa kesi na wamefukuzwa kazi. Yeye kama mbunge anajua. Kwakua Ummy ameungana na huyo mtenda dhambi ninamuombea nae aondolewe maana anafanya upendeleo.
Mh. Rais ajue kwamba watu wameporwa wake zao na kazi wamefukuzwa.
Pia ajue kwamba hao wanawake wanakula keki ya taifa isivyo halali maana niwabadhirifu kwenye idara zao na mkurugenzi hana ubavu wa kuwauliza.
 
Back
Top Bottom