Barua ya wazi kwa Askofu Mkuu Mhashamu Nyaisonga: Je, Mungu amekoma kuwa mtetezi wa wanaoonewa?

Zakaria Lang'o

JF-Expert Member
Apr 2, 2012
2,593
2,767
Askofu Mkuu, Mheshamu Nyaisonga. Hii ni barua yangu ya wazi kwako ikiwa imebeba kichwa cha habari tajwa.

Napenda kujitambulisha kwako kama raia wa kawaida ambaye ninajali sana jinsi ninyi viongozi wetu mnavyoshiriki masuala ya kila siku ya Taifa letu.

Jana nimesoma juu ya mahubiri yako kwa waumini wa Kanisa Katoliki ukiwalaumu Viongozi wa Vyama vya Upinzani kususia uchaguzi wa serikali za mitaa.

Nimeshangaa na kusikitika sana. nimejiuliza maswali mengi juu ya mitazamo ya watumishi wa Mungu juu ya Demokrasia na uendeshaji wa nchi yetu.

Mahali pengi katika Biblia Mungu amejipambanua kama "Mungu wa wanaoonewa" Biblia imejazwa aya zinazozungumzia suala la Mungu kusimama pamoja na wanaonyanyaswa na kuonewa kiasi kwamba sioni haja ya kuyanukuu maana unayafahamu.

Sasa mshangao wangu kwako ni kuwa kwa idadi ya malaki ya wagombea wa upinzani walioondolewa na wasimamizi wa uchaguzi hata bila kutolewa sababu za msingi, wewe unaona wakosaji ni Wapinzani?

Hivi umewahi kujiuliza juu ya sababu za Rais Magufuli kuwaita Ikulu watendaji ambao ni Wasimamizi wasaidizi katika uchaguzi wa serikali za mitaa na mara waliporudi wakayafanya waliyoyafanya kwa kuwapitisha wagombea wote wa CCM na kutowateua wagombea karibu wote wa Upinzani bila kueleza sababu toshelevu?

Askofu Nyaisonga, hebu nikupe mfano huu hapa: hivi iwapo wewe na Paroko mkiwa wageni wangu, nikawakaribisha sebuleni; mara nikamwita mwanangu mdogo chumbani na kumnong'oneza jambo; akirudi sebuleni akaanza kuwaporomoshea matusi ninyi wageni wangu, nani atalaumiwa, kati ya mimi mzazi, yule mtoto au ni ninyi wageni mlinitembelea?

Je, katika hali ya kawida iwapo mimi mzazi wa yule mtoto sitatoka hadharani kumkemea na kumchukulia hatua kwa kuwatukana wageni wangu, je, wewe Askofu uliye chini ya dari yangu utachukua hatua gani katika mazingira yale?

Utabaki pale sebuleni ukisubiri ukarimu wangu ilihali ukidhalilishwa na mtoto ambaye anaonyesha utovu wa nidhamu uliobarikiwa na mimi baba yake?

Mhe. Askofu, viongozi hasa Kiongozi wetu Mkuu ameonyesha dhahiri chuki dhidi ya Demokrasia ya Vyama vingi. Amewafanya Viongozi wa Upinzani kuwa ni adui zake. Anawatendea vibaya kila apatapo nafasi.

Na sasa kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu ubaguzi wa kiitikadi umeshushwa toka juu hadi huku chini kwenye vijiji, vitongoji na mitaa. Chuki ni kubwa sana maana wananchi wengi wanaiheshimu demokrasia ya vyama vingi.

Mhe. Askofu sasa tuiangalie Katiba ambayo ni Msahafu wa kuongoza nchi yetu. Rais anapochaguliwa kabla ya yote huapa kuilinda Katiba ya nchi huku akimuomba Mungu wake amsaidie.

Miongoni mwa mambo muhimu ni kuwa Rais akishaapa kwa Katiba basi anakuwa ndiye mlezi wa Vyama vyote vikiwemo vya Upinzani.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaweka bayana jambo hili katika msingi wake ulio kwenye utangulizi kwamba: KWAKUWA SISI wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki udugu na amani.

Mhe, misingi ya SISI wananchi (WE the people - citizens) wa Tanzania ni:- i) UHURU ii) HAKI iii) UDUGU na iv) AMANI

Kwa hakika hii ndiyo misingi inayotufanya kuwa watu huru (citizens)katika Taifa huru. Si Taifa huru tu, bali pia linalofuata mfumo wa kidemokrasia ambao umewekewa sheria ya katiba iliyoanzisha vyama vingi vya siasa.

Utekelezaji wa misingi inajengwa katika mihimili mitatu mikuu:-

i)Serikali ii) Bunge iii) Mahakama

Madhumuni ya vyombo tajwa hapo juu ni kuhakikisha kuwa Tanzania inajengwa kwa misingi ya uhuru, haki, udugu, na amani; kwa serikali kufuata barabara ya demokrasia (Democratic road)

Mhe, Ibara ya 8 (1.): (a), (b) na (c) inasisitiza juu ya “Ukuu wa watu (“ the supremecy of the people (citizens))” katika ujenzi wa Taifa lao.

“(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Nchi inayofuata misingi ya demokrasia na haki ya kijamii, na kwa hiyo

(a) wananchi ndio msingi wa mamlaka yote, na Serikali itapata madaraka na mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii;

(b) lengo kuu la serikali litakuwa ni ustawi wa wananchi;

(c) Serikali itawajibika kwa wananchi;

Ibara ya 9.

Kwa hiyo, Mamlaka ya Nchi na vyombo vyake vyote vinawajibika kuelekeza sera na shughuli zake zote katika lengo la kuhakikisha:

(a) kwamba utu na haki nyinginezo zote za binadamu zinaheshimiwa na kuthaminiwa;

(b) kwamba sheria za nchi zinalindwa na kutekelezwa;

(c) kwamba shughuli za Serikali zinatekelezwa kwa njia ambazo zitahakikisha kwamba utajiri wa Taifa unaendelezwa, unahifadhiwa na unatumiwa kwa manufaa ya wananchi wote kwa jumla na pia kuzuia mtu kumyonya mtu mwingine;

(d) kwamba maendeleo ya uchumi wa Taifa yanakuzwa na kupangwa kwa ulinganifu na kwa pamoja;

(e) kwamba kila mtu mwenye uwezo wa kufanya kazi anafanya kazi, na kazi maana yake ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu riziki yake;

(f) kwamba heshima ya binadamu inahifadhiwa na kudumishwa kwa kufuata Kanuni za Tangazo la Dunia kuhusu Haki za Binadamu;

(g)kwamba Serikali na vyombo vyake vyote vya umma vinatoa nafasi zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini au hali ya mtu;

(h) kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu au upendeleo zinaondolewa nchini;

(i) kwamba matumizi ya utajiri wa Taifa yanatilia mkazo maendeleo ya wananchi na hasa zaidi yanaelekezwa kwenye jitihada ya kuondosha umaskini, ujinga na maradhi;

(j) kwamba shughuli za uchumi haziendeshwi kwa njia zinazoweza kusababisha limbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;

(k) kwamba nchi inatawaliwa kwa kufuata misingi ya demokrasia na ujamaa.”

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Juu ya

Haki na Usawa:

Ibara ya 12:” (1)binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa.

(2) kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.”

Ibara ya 13: “(1) watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ya ubaguzi.”

Mhe. Askofu, Ibara ya 146 (1) inatamka wazi juu ya serikali za mitaa kuchaguliwa na wananchi wa wa maeneo husika katika uchaguzi wa kidemokrasia ili kujiendeshea mambo yao maendeleo.

Kwa muktadha huu MHe. Askofu unapata wapi mamlaka na uhalali wa kuitetea serikali inayovunja Katiba wazi wazi na kueneza chuki na ubaguzi katika jamii kwa sababu ya uroho wa madaraka!!!?

Hata hivyo haishangazi maana ndiyo kawaida ya Kanisa Katoliki la Tanzania kwamba anapotawala Rais Mkatoliki huhesabiwa kuwa ni malaika hata kama atafanya mambo yanayomkera Muumba wa Mbingu na Nchi.

Haishangazi pia kuwa kule Rwanda Kanisa Katoliki lilisimama na wauaji wa Halaiki tena baadhi ya Maaskofu na Mapadre wakiwa mstari wa mbele katika kuwauwa waumini waliokimbilia Makanisani. Ushahidi huu hapa:

Pope apologises for church's role in Rwanda genocide

Catholic church was accused of being close to Hutu-led government in 1994 when 800,000 mostly Tutsis were killed.

20 Mar 2017

Several Catholic priests as well as nuns were charged with participating in the 1994 genocide [Reuters]

Several Catholic priests as well as nuns were charged with participating in the 1994 genocide [Reuters]

Pope Francis has pleaded for forgiveness for "the sins and failings of the Church and its members" implicated in the 1994 Rwanda genocide that killed about 800,000 people.

The pontiff "conveyed his profound sadness, and that of the Holy See and of the Church, for the genocide against the Tutsi", the Vatican said in a statement following a meeting on Monday between Francis and Rwandan President Paul Kagame.

"He implored anew God's forgiveness for the sins and failings of the Church and its members, among whom priests, and religious men and women who succumbed to hatred and violence, betraying their own evangelical mission," it said.

A number of churches became scenes of mass killings during the 100-day rampage, as Hutu militiamen found people seeking refuge there, sometimes turned over by priests, with no way out.

TIMELINE: How Rwanda's genocide unfolded

Francis' pardon plea followed a request from Rwanda in November for the Vatican to apologise for the church's role in the massacres.

Since the genocide, whose victims were mostly from the Tutsi minority, the Catholic Church has been accused of being close to the Hutu government in power in 1994.

Francis, 80, said he hoped "this humble recognition of the failings of that period, which, unfortunately, disfigured the face of the church, may contribute to a 'purification of memory'" and promote "renewed trust".

Rwanda's government indicated it felt the apology did not go far enough, saying the local church was still complicit in protecting the perpetrators of the genocide.

f66454dba91540ba80cc2428e6a25602_18.jpg
Pope Francis poses with Rwandan President Paul Kagame and his wife Jeannette during a private meeting at

Mwalimu Nyerere aliwahi kusema: "Kuogopwa ni sifa na ada ya madikteta, viongozi halisi hawapendi kuishiriki sifa hii. Kujenga mazoea ya kutii viongozi hata katika mambo haramu ni dalili ya woga, ni kukaribisha udikteta."
Kazi kwako Askofu Nyaisonga.Bwana awe nawe.
 
Kawakamata huyu askofu anaakili sana huwezi kujilinganisha naye maana mmezoea kuongozwa na zero mbowe

Mkatubu huu ujinga /dhambi ya kukataa kila kitu na mnakula ruzuku za bura

Asante nyaisonga kwa kukata kichwa cha faraoh


State agent
 
Mimi binafsi mara ya mwisho kuheshimu masikofu na mapadiri wa kanisa katoliki, ilikua mwaka 1994 wakati wa mauwaji ya kimbali Rwanda.

Maaskofu wa kiHutu walihimiza wafuasi wao kuua waTusi wakikatoliki na wahutu wenye msimamo wa kati masikini wengi waumini wakikatoliki walikimbilia Miskitini kujihifadhi ili wasifanyie huo unyama na wakatoliki wenzao, karibu wa Tusi 800,000 wa liuawa, Tangia hapo siheshimu kiongozi wa hiyo dini ni wanafki sana, na wako kidunia zaidi kwa kupitia mgogo wa Dini
 
Tumwache askofu, tusimshambulie kwa kusema ukweli

Anayewaamini maaskofu hawa hana tofauti na mtu anayemtii shetani. Hao viongozi wa RC ni wale wanaotengeneza barabara ya watu kwenda kumwaga damu. Ni viongozi mufulisi na wachafu kupata kutokea ndani ya dini hii. Naona nchi hii ikipelekwa kumwaga damu kwa ndimi za hao viongozi wa RC.
 
Kawakamata huyu askofu anaakili sana huwezi kujilinganisha naye maana mmezoea kuongozwa na zero mbowe

Mkatubu huu ujinga /dhambi ya kukataa kila kitu na mnakula ruzuku za bura

Asante nyaisonga kwa kukata kichwa cha faraoh


State agent

Huyo sio askofu bali ni ibilisi na ni sehemu ya manabii wa uwongo zama hizi za kuelekea mwisho wa dunia. Waumini wa RC sasa ni wakati wa kupaza sauti kwa viongozi wanaocha kusimamia haki na kumtumikia shetani na fahari zake.
 
Wapinzani wengi si wakatoliki na ukikutana na mkatoliki mpinzani basi Ni yule ambaye hata jumuiya huwa haendi na hapokei hata komunyo na mbishi kutoa sadaka na zaka za kanisa

Kwa mwenendo huo wa viongozi wa RC kwenda kanisani ni sawa na kushiriki ibada ya mizimu, na kutoa sadaka ni sawa na kutoa pesa kwa mapepo a.k.a chuma ulete. Kwa maneno marahisi waumini wanaowaamini viongozi wa aina hiyo wana matatizo
 
Huyo sio askofu bali ni ibilisi na ni sehemu ya manabii wa uwongo zama hizi za kuelekea mwisho wa dunia. Waumini wa RC sasa ni wakati wa kupaza sauti kwa viongozi wanaocha kusimamia haki na kumtumikia shetani na fahari zake.
Unaona upinzani mumejaa si.wapinga CCM tu lakini na wapinga ukatoliki.Mumejificha vyama vya upinzani agenda yenu ikiwa kupinga ukatoliki na Bakwata
 
Unaona upinzani mumejaa si.wapinga CCM tu lakini na wapinga ukatoliki.Mumejificha vyama vya upinzani agenda yenu ikiwa kupinga ukatoliki na Bakwata

Ni hivi hata ukitaka kuhamisha mada bado hutaweza maana tuko vizuri. Askofu sio ukatoliki bali ni cheo ndani ya ukatoliki, kwa hiyo sio ajabu cheo ndani ya ukatoliki kukaliwa na ibilisi kama huyo askofu. Narudia tena, huyo askofu ni wale mashetani waliopata vyeo ndani ya kanisa katoliki fullstop.
 
Back
Top Bottom