Sanda Matuta
JF-Expert Member
- May 9, 2007
- 949
- 142
MF/NA: 836'04 Johnson Nguza (Papii Kocha)
Gereza Kuu Ukonga
S.L.P 9091
Dar es Salaam
Mh. Rais Jamuhuri ya Muungano Tanzania
YAH: MAOMBI YA KUPEWA MSAADA (MSAMAHA) WA KUFUTIWA ADHABU YA KIFUNGO NILIYOPEWA NA MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU.
Husika na somo hilo hapo juu. Mimi ni mfungwa katika gereza kuu Ukonga.
Kwa heshma na taadhima na kwa kutambua utu na huruma yako ya ki MUNGU ulionayo dhidi ya binadamu wenzako pamoja na mamlaka uliokabidhiwa na jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
Naanguka na kushika miguu yako mitukufu muheshimiwa rais. Na kuomba msaada (msamaha) kwako muheshimiwa rais
Kwa njia hii ya maandishi kusudi niweze kuondolewa adhabu ya kifungo cha maisha gerezani, niliyohukumiwa na mahakama tajwa hapo juu.
Mh.Rais mimi nimefungwa nikiwa bado kijana mwenye umri mdogo. Mpaka sasa natambua wazi hatima pamoja na dhamana ya maisha yangu ipo katika mikono yako mitukufu Mh. Rais.
Naomba huruma yako muheshimiwa Rais maana mimi ni mtoto wako ninaehitaji huruma yako wewe mzazi.
Natumaini kauli yako ya mwisho ndio itakayoleta pumzi ya uhai nafsini mwangu
Nakutakia kazi njema, afya njema na maisha marefu.
Mungu akubariki!
Wako mtiifu
NO:836'04
JOHNSON NGUZA (PAPII KOCHA)
Tahadhari:
Inaruhusiwa kuinakili hii story kama ilivyo ( i wont mind), ila sio vibaya pia mkitoa credit na sio kusema eti ni kutokana na vyanzo vyenu vya habari.
Walengwa mnajijua sio lazima nitaje majina (jaydee)
Hiyo sio lugha ya Papii Kocha na barua rasmi haiandikwi hivyo - Wewe Paka Jimmy hujui JD ako kwenye System Gani - Chunguza utagundua kitu
Inagusa!..
Lakini kwanini iwekwe kwa Jaydee kwanza?
Jaydee ana mawsasiliano gani na Ikulu, au MKULU wa nchi husoma sana blogu ya JD?
HAPO NIFAFANULIWE!
...Hivi huyo Papii amekwenda shule angalau hata darasa la 7? Barua haina kichwa, mwili wala mkia.....Mh! Huenda watu mnataka kutupisha baraza la kahawa tu humu....Hiyo sio lugha ya Papii Kocha na barua rasmi haiandikwi hivyo - Wewe Paka Jimmy hujui JD ako kwenye System Gani - Chunguza utagundua kitu
Hiyo sio lugha ya Papii Kocha na barua rasmi haiandikwi hivyo - Wewe Paka Jimmy hujui JD ako kwenye System Gani - Chunguza utagundua kitu
Lakini ameshasema ni barua ya MKUU sio ujumbeNadhani Jaydee alikwenda kumtembelea ndio akampa hiyo barua amsaidie kuifikisha kwa Mheshimiwa, ukiingia kwenye blog ya Jaydee utaiona imeandika kwa mkono, Jaydee akaipiga picha na kuiweka kwenye blog yake na baada ya kuona maandishi yanaonekana kwa mbali ndio akaamua kuiandika upya ili watu waweze kuisoma na walio karibu na Mh. Rais waweze kumfikishia ujumbe wakati yeye (Jaydee) anaendelea kutafuta taratibu za kumuona mh.Rais ampatie barua yake.
Lakini ameshasema ni barua ya MKUU sio ujumbe
Ingekuwa ujumbe wa mkuu ingeeleweka kuwa ameuweka pale ili watu wamfikishie ujumbe wake sasa barua??? Ilipaswa iende moja kwa moja kwa mheshimiwa na si kuitundika pale- je siku mheshimiwa akitoa msamaha kwa wafungwa na Papii akisamehewa ndo tujue kuwa amesamehewa kwa vile aliomba msamaha hadharani?
Hivi kesi ya kubaka watoto huwa inahitaji msamaha wa Raisi??? naomba kuelimishwaaa