Barua ya majibu ya Msekwa kuwajibu Kinana na Makamba hii hapa

Angekuwa mnafiki angepeleka barua kwa mkono? Ama kwenye lugha yenu hii ina maana gani? Au ulitaka aipeleke kwa Musiba? Ameipeleka kwa Katibu kwa Baraza kwa mkono. Sasa hapo unafiki uko wapi? Huyo unayetaka am-face una uhakika gani kuwa hajawahi kum-face. Ama ulitaka afanye hivyo kwenye TV?
Barua ya mzee Makamba na Kinana anaipeleka Nape?
 
Msekwa nadhani ndio kiongozi Mstaafu muoga kuliko wote , hana ujasiri wowote ule na wala hawezi kutenda haki kwenye sakata hili , hii ni kwa sababu hajawahi kujitegemea na hajawahi kuhangaikia maisha yake nje ya ccm , anaiabudu ccm kuliko Mungu , kwake " mwenye bia nyingi mezani " ndiye wake , hata mke aliyenaye alimpata kwenye jumuiya za chama .
Wewe ni mbuzi hujui hata taratibu zinaendaje akiliyako ni kutaka uvunjifu wa amani
 
Msekwa nadhani ndio kiongozi Mstaafu muoga kuliko wote , hana ujasiri wowote ule na wala hawezi kutenda haki kwenye sakata hili , hii ni kwa sababu hajawahi kujitegemea na hajawahi kuhangaikia maisha yake nje ya ccm , anaiabudu ccm kuliko Mungu , kwake " mwenye bia nyingi mezani " ndiye wake , hata mke aliyenaye alimpata kwenye jumuiya za chama .
ukatorik tu ha
Huku bavichaa wako bize na audio feki za ccmView attachment 1156857
CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KUPITIA KICHAA WAKE JPM CHAWAZULUMU/ KUWAPORA WAKULIMA KOROSHO ZAO HUKO KUSINI.
chashindwa kulipa!
chasiingizia ujenzi wa mataaluma ya reli
Hovyo wewe
 
Msekwa nadhani ndio kiongozi Mstaafu muoga kuliko wote , hana ujasiri wowote ule na wala hawezi kutenda haki kwenye sakata hili , hii ni kwa sababu hajawahi kujitegemea na hajawahi kuhangaikia maisha yake nje ya ccm , anaiabudu ccm kuliko Mungu , kwake " mwenye bia nyingi mezani " ndiye wake , hata mke aliyenaye alimpata kwenye jumuiya za chama .
Neno "uoga" unautafsiri vipi? Kuna siku aliyekuwa kocha wa arsenal mzee arsene Wenger aliwahi kuulizwa....akistaafu atafanya shughuli gani? Alijibu hawezi kufanya chochote zaidi ya soka hii ni kwa sababu ameishi na kukulia kwenye soka...je Wenger ni muoga wa maisha nje ya soka?

The same applies to mzee Msekwa...amekuwa ameishi na amezeekea CCM tangu iikiwa Tanu...je huo ndo uoga?

Msekwa kumuoa Anna Abdallah toka UWT kuna tatizo gani? Mara Nyingi watu wa Kada Fulani wanaoana wao kwa wao sababu kuu ni kukutana Mara kwa Mara kwenye shughuli zao.....je tumlaumu mlevi akimuoa barmaid?

Kaka rudi tena darasani na utafute tafsiri sahihi ya neno uoga....maana unapotosha watu.

Humu JF kina Kinana wakati wameshika hatamu walishambuliwa sana kuwa ni majangiri na waua tembo wetu....je Leo baada ya kustaafu ndo wamekuwa mashujaa na ujangiri wameacha?

WaTanzania acheni unafiki na kusukumwa sukumwa na upepo.
 
Wajipange kisawasawa, ni vyema wakae kimya. wakati mwingine ukimya unasaidia kuonyesha hekima zao, wala siyo lazima ukituhumiwa ujibu kama ni kuchafuka walishachafuka sana na wala hawachafuliwi na Msiba, hata wakiweka mkwala ndani ya chama tuko tayari kumsimamisha kama mgombea pekee na atapata kura za kutosha. Makamba kama mwasisi wa rushwa ndani ya chama ambaye kwa kiasi kikubwa alikiweka pabaya chama hicho bora angekaa kimya vinginevyo anamharibia hata kijana wake January anayeonekana walau kuwa na hekima kidogo kuliko Baba yake. Niombe JPM awapuuze hao naona ugonjwa wa kusahau umewaanza mapema.
 
Nimeanza kumwogopa sana Musiba inaelekea anachosema anauhakika nacho na maneno yake yana kishindo kikuu. Musiba amesema Vodacom ilikuwa ya CCM wakagawana na wenye share ndio hawa wanaotoa majibu kwa akina Kinana hatari.
 
Msekwa anatoa majibu ya awali kama nani?? Hapo ni kama keshavunja katiba, je kikao kikaja kuamua vingine itakuwaje?
Kama umesoma between the lines,kikao cha Baraza hakitakuja na maamuzi tofauti na haya.They are thrown under the bus sababu wanes jamani was “wapambane na hali zao”!kwamba kutakua kikao kingine ni geresha kuwafanya waendelee kungoja/au kununua muda wakati majibu yako tayari.usishangae hata kikao cha hilo baraza hakitakaa
 
BARUA YA MAJIBU YA AWALI.

Ndugu Abdulrahman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu;

Ndugu Yussuf Makamba, Katibu Mkuu wa CCM Mstaafu;

DAR ES SALAAM.

Tarehe15 Julai, 2019.

Nakiri kupokea barua yenu ya tarehe 15 07/ 2019 ambayo mliisaini wote wawili, na ikawasilishwa kwangu kwa mkono na Mhe. Nape Nnauye (Mb), jana tarehe 14/07/ 2019.

Baada ya kuisoma kwa makini, nimetambua kwamba malengo makuu ya barua hiyo, yalikuwa ni mawili yafuatayo:

(i) Kuwasilisha kwa pamoja malalamiko yenu dhidi ya mtu aitwaye Cypriian Musiba; ambaye “amekuwa akitoa maelezo yenye kuwatuhumu na kuwazushia uwongo ninyi, na viongozi wengine wastaafu wa CCM na wa Serikali waliostaafu na walioko madarakani, kwamba eti mnamhujumu Rais kutekeleza majukumu yake” (ukurasa wa kwanza, para ya pili).

(ii) Kuomba Baraza la Viongozi Wakuu Wastaafu wa CCM “walishughulikie jambo hili, kwa namna ambayo wazee wenyewe wataona kuwa inafaa”. (ukurasa wa pili, para ya mwisho).

Zaidi ya hayo, nimezingatia maelezo yenu ya kuwa “tuliamini kwamba, kama utaratibu wa CCM ulivyo, kazi ya kulinda heshima ya CCM ni pamoja na kukemea vikali, pale viongozi wake wakuu wa sasa na waliostaafu wanapochafuliwa. Kwa hiyo basi, tulitegemea wahusika ndani ya Chama watazikemea kauli zake , na kumuasa asitumie jina la Mwenyekiti wa CCM kuchafua na kudhalilisha watu, au kumchukulia hatua nyingine muafaka. Kwa bahati mbaya, hili halikufanyika”. (ukurasa wa kwanza, para ya tatu).

Kwa maelezo hayo, barua yenu inachukua sura ya “rufaa kwa Wazee” hawa, kutokana na kuona kwamba Chama “kimeshindwa kukemea vikali jambo hili”.

Majibu ya awali.

Kama mnavyofahamu, Baraza hili hufanya kazi kwa njia ya vikao rasmi, na kwamba Katibu peke yake hana mamlaka ya kutoa maamuzi yoyote. Kwa hiyo, nitawasilisha barua yenu kwa Wajumbe wa Baraza, ili kupata maelekezo yao juu ya nini kifanyike. Lakini wakati tunasubiri, naweza kutoa majibu ya awali, yakiwa ni ya kukumbushana mambo ya msingi yafuatayo ambayo yanapaswa kuzingatiwa, (ambayo mimi na ninyi tulisimamia utekelezaji wake, wakati tulipokuwa madarakani kama viongozi wakuu wa Chama):

(1) Wajibu wa kutii Katiba na Kanuni zilizopo.

Jambo la kwanza linahusu mamlaka ya kutenda kazi, au ‘ jurisdiction’, ya Baraza letu, kama yalivyowekwa na Katiba ya Chama, Kama mnavyojua, Katiba ya Chama cha Mapinduzi imekipangia kila Kikao cha Chama kazi zake mahsusi za kufanya. Na kazi mahsusi ya Baraza la Ushauri la Viongozi Wakuu Wastaafu wa CCM, zimetajwa na kuainiishwa katika Ibara ya 127 (3) ya Katiba hiyo, Toleo la 2012, kuwa ni “kutoa ushauri kwa Chama cha Mapinduzi, na kwa Serikali zinazoongozwa na Chama hicho”. Lakini kazi zile za kuangalia mwenendo wa wanachama na Viongozi wake, na kuchukua hatua stahiki pale inapobidi; hizo zimepangiwa vikao vingine vya Chama, vikao ambavyo ni vya utendaji (administration) ; kama ilivyoainishwa katika Ibara zinazohusu Vikao hivyo. Maana yake ni kwamba Kikatiba, Baraza la Ushauri halikupewa mamlaka, au ‘jurisdiction’, ya kutenda kazi hizo, ambazo ni za ki-uendeshaji. Badala yake, jukumu hilo limetolewa kwa vikao vingine, ambavyo ni vya viongozi walioko madarakani.

(2) Jambo la pili linahusu umuhimu wa kuzingatia miiko ya utoaji ushauri (ambayo ndiyo kazi mahsusi ya Baraza hili); ambayo ni hii ifuatayo:

(i) Kwamba ushauri huombwa. Ushauri kamwe hauwezi kushinikizwa kwa mshauriwa, au kutolewa kwake

kama amri ! Ndiyo kusema kwamba ushauri hauwezi kutolewa pale ambapo hauhitajiki. Na mwenye kuamua kuwapo kwa hitaji hilo, ni yule anayehitaji kupata ushauri, SIYO yule anayetaka kutoa ushauri.

(ii) Hata pale ushauri unapotolewa, tusisahau kwamba unaweza ama kukubaliwa; au kukataliwa. Pale unapokubaliwa, thamani yake inakuwa ni kubwa, kwa maana ya kuondoa tatizo lililokuwapo. Lakini pale ushauri unapokataliwa, thamani yake inakuwa ni sifuri kabisa, kwa maana ya kutatua tatizo lililopo.

(3) Jambo la tatu, ni kwamba jukumu la mtu yeyote aliyetuhumiwa la kusafisha jina lake, ni la mtuhumiwa mwenyewe.

Barua yenu imeeleza kwamba “Mlitafakari suala la kujitokeza hadharani ili kutoa yaliyo moyoni mwenu katika kujibu uwongo wake, kusafisha majina yetu, heshima yenu, na rekodi nzuri ya utumishi wenu, lakini mkaona kuwa ni vyema kwanza mkawasilisha malalamiko yenu kwenye Baraza la Ushauri la Viongozi Wakuu Wastaafu wa CCM, ili jambo hili lishughulikiwe”.

Sasa ki-utaratibu, siyo sahihi kujaribu kukwepa jukumu hilo la watuhumiwa wenyewe kujisafisha kwa kukanusha tuhuma zinzowahusu, na kujaribu kulihamishia jukumu hilo kwa watu wengine . Hii ni kwa sababu watuhumiwa wenyewe ndio wanaojua ukweli kuhusu tuhuma hizo, na kama kweli hazina msingi, ni wajibu wao kufichua ukweli wanaoujua.

Umuhimu wa jambo ili unatokana na kuwapo kwa dhana inayosema kwamba “silence means consent”; ambayo maana yake ni kwamba ‘ukinyamaza kimya bila kukanusha tuhuma zilizoelekezwa kwako, ukimya wako huo unachukuliwa kwamba umekiri ukweli wa tuhuma hizo’. Nafurahi, na kuwapongeza, kwamba tayari mumetekeleza wajibu huo kupitia vyombo vya habari.

TAHADHARI: Msiruhusu machungu ya tuhuma hizo yakawasahaulisha misingi hii, mkashawisika ‘kutafuta njia za mkato’ za kuyashughulikia, ambazo kumbe zinakiuka Katiba ya Chama chetu.

Madhumuni ya maelezo haya

Naomba ieleweke kwamba madhumuni ya kukumbushana juu ya mambo haya ya msingi , ni kuonesha tu ugumu uliopo wa ki-Katiba, kwa Baraza la Ushauri la Viongozi Wakuu Wastaafu wa CCM kushughulikia malalamiko yenu, kama mlivyoomba. Ugumu huo unatokana na kuzingatia kuwa:

kwanza, Katiba ya Chama haikutoa jukumu la kufanya kazi za ki-uendeshaji (administration) kama hii ya kusikiliza malalamiko yenu, kwa Baraza hili. Lakini pili, Baraza letu pia halikupewa mamlaka ya kusikiliza rufani zinazotolewa dhidi ya Chama, kama hii ya kwenu.

Ni muhimu vile vile, kuzingatia kwamba Baraza la Viongozi Wakuu Wastaafu wa CCM, ni chombo maalum cha Chama hicho , kilichoundwa na kupewa kazi maalum, iliyotajwa katika Katiba ya Chama. Baraza hili siyo kundi lolote tu la “wazee wa Chama” (kama yalivyo yale “Mabaraza ya wazee” mengine, yaliyotajwa katika Ibara ya 128 ya Katiba ya Chama), ambayo wajumbe wake wanatajwa kuwa ni “wazee wote wana-CCM, wenye umri kuanzia miaka sitini”; ambao, kwa kuwa hawakupangiwa jukumu lolote maalum, wanadhaniwa kuwa wanaweza kushiriki tu katika utekelezaji wa shughuli zozote za Chama “kwa kutumia busara za uzee wao, kama watakavyoona wao kuwa inafaa”!

Nahitimisha kwa kurudia kusema, kwamba haya ni majibu ya wali tu. Nawajibika kusubiri maelekezo ya wajumbe wa Baraza.

Pius Msekwa.

KATIBU, BARAZA LA USHAURI LA VIONGOZI WAKUU WASTAAFU WA CCM.
Kuchafuliwa ni kubambikiziwa mambo mabaya yasiyo kweli,sasa katika mazingira yao, kweli wamechafuliwa?Si kweli.Kama ni kweli wakanushe tuhuma za Mukama.
Na je,utendaji wa watuhumiwa ni mzuri kama wanavyodai?So far hakuna ushahidi huo.Kama nilivyosema wakanushe tuhuma za Mukama kama ni wasafi.Ila wawe makini,maana jamaa naona hazungumzi kutoka hewani,ana ushahidi wa kufa mtu.Naamini huyu bwana yuko ndani ya mfumo.Confidence aliyo nayo na taarifa alizonazo haiwezekani mtu wa kawaida kuzipata.
 
JK sio mtu wa kuvamia mambo kichwakichwa kama Makamba au Nape.

Hao watu uwezo wao ni mdogo kichwani zaidi ya mdomo mwingi.

Nashangaa Kinana kuingia mtego huu.

Membe pia anakuwa na papara sana. Sidhani kama alifanya hesabu zake viziei kukokotoa namna atakavyo fikia kilele cha mafanikio kisiasa kadiri ya ndoto zake.
yaani wewe ndo unaakili saaan kupita wao
 
Msome vizuri tena.
Hakuna mahali ametoa hitimisho au majibu ya mwisho.

Yeye kama katibu anao wajibu wa kuwajulisha wahusika kuwa amepokea barua yao, na kisha kutoa maoni yake au kukumbusha taratibu, kanuni, sheria na katiba vinasema nini na nani wa kutolea mahamuzi ya madai ya kwenye barua.

Asante Titicomb!
Majibu ya awali ya Msekwa yanaonyesha ukomavu na busara kubwa kushughulikia mambo mazito na ya msingi. Tufahamu kuwa hawa makatibu wastaafu, hususan Kinana kuwa ni watu wenye uelewa mpana sana. Kinana ndiye aliyeikoa CCM baada ya kuzama ikiwa chini ya Makamba na kukaribia kilindini chini ya Mukama. Ni vyema pia kukumbuka kuwa Kinana alihamua kujiuzulu nadhani kutoka kwenye sekretarieti ya wakati huo, kabla ya baadae JK kumuomba awe katibu mkuu. Walioona mbali, akiwemo Mhariri maarufu Kibanda, waliandika kuwa Kinana sio mtu wa kubeza baada tu ya kuchaguliwa kuwa katibu Mkuu. Itoshe tu kusema kuwa Kinana anayafahamu yote haya yaliyosemwa na Msekwa, lakini pia anayafahamu ambayo yangekuwa matokeo endapo barua yao ingewakilishwa kwenye sekretariati ya sasa.
Naamini, kwao hawakutegemea wala kuhitaji makubwa kuliko haya ya kuufahamisha umma juu yanayoendelea na pili, kutokubaliana kwao na sekretariati ya sasa kunyamazia watu kuchafuliwa na kutengeneza dhana inayoyofikiriwa kuwa wao wako nyuma ya huyu mpuliza mbiu.

Hii ni tathmini yangu kadri ya upeo wangu wa siasa za Tanzania.
 
Muoga kwakuwa hajatoa majibu sawa na matarajio yako?
Hekima huepusha mambo mengi sana wakati wote..
Mzee amejibu kihekima sio kimuhemko
Sio tuu kajibu kihekima bali pia ameonesha weledi katika kuilinda katiba na misingi ya chama. Mzee kichwa sana.
 
Neno "uoga" unautafsiri vipi? Kuna siku aliyekuwa kocha wa arsenal mzee arsene Wenger aliwahi kuulizwa....akistaafu atafanya shughuli gani? Alijibu hawezi kufanya chochote zaidi ya soka hii ni kwa sababu ameishi na kukulia kwenye soka...je Wenger ni muoga wa maisha nje ya soka?

The same applies to mzee Msekwa...amekuwa ameishi na amezeekea CCM tangu iikiwa Tanu...je huo ndo uoga?

Msekwa kumuoa Anna Abdallah toka UWT kuna tatizo gani? Mara Nyingi watu wa Kada Fulani wanaoana wao kwa wao sababu kuu ni kukutana Mara kwa Mara kwenye shughuli zao.....je tumlaumu mlevi akimuoa barmaid?

Kaka rudi tena darasani na utafute tafsiri sahihi ya neno uoga....maana unapotosha watu.

Humu JF kina Kinana wakati wameshika hatamu walishambuliwa sana kuwa ni majangiri na waua tembo wetu....je Leo baada ya kustaafu ndo wamekuwa mashujaa na ujangiri wameacha?

WaTanzania acheni unafiki na kusukumwa sukumwa na upepo.
Tunapozungumzia sakata hili ni lazima tujikite ndani ya sakata lenyewe hasa , yote niliyoandika kuhusu Msekwa haikuwa lawama , bali nilikuwa naionyesha dunia kwamba Msekwa hana uwezo wa kuwa msuluhishi kwenye jambo ambalo anao upande wake , hayuko neutral , ndio maana nikaweka mifano iliyotukuka ! ili uelewe namaanisha nini , halikuwa lengo langu kumuonea Wivu Mzee Msekwa kwa kupata mke ndani ya jumuiya ya ccm
 
Maajabu! Barua ya Msekwa imevuja kabla hata hajai-sign! Au wazee wa baraza la wazee huwa hawasign documents zao?

Hata hivyo nimeona tatizo la kisarufi ambayo si rahisi ifanywe na Mzee Msekwa ambaye amewahi kuandika hata vitabu:

'Ndugu Abdurahaman Kinana, Katibu Mkuu wa CCM mstaafu' badala ya .......Kinana, Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM. Hali kadhalika kwa mzee Makamba. Hii kitu inaitwa 'CCM mstaafu' sijui nini.....maana ni kuwa CCM ilishastaafu. Nachelea kusema hii barua si genuine kwa sababu haina sahihi ya mwandishi lakini pia tatizo la sarufi inaonesha imeandikwa na Bashite classic.
Haya ndio makosa ya kisarufi? Ok hiyo barua ni feki na mzee msekwa anawaunga mkono kina Kinana.

Haya furahi sasa
 
Msekwa nadhani ndio kiongozi Mstaafu muoga kuliko wote , hana ujasiri wowote ule na wala hawezi kutenda haki kwenye sakata hili , hii ni kwa sababu hajawahi kujitegemea na hajawahi kuhangaikia maisha yake nje ya ccm , anaiabudu ccm kuliko Mungu , kwake " mwenye bia nyingi mezani " ndiye wake , hata mke aliyenaye alimpata kwenye jumuiya za chama .
Uwiii
 
Back
Top Bottom