Barua kwako Rais Samia Suluhu Hassan

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
16,365
12,823
Madam President,naomba nikusalimie kwa salam ambayo umeipendelea Sana wewe mwenyewe kuwa NAKUSALIM KWA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,NA KAZ IENDELEE.

First and foremost,naomba nichukue nafas hii kukupa pole zangu nyingi sana KWA kifo cha aliekuwa RAIS wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Hayati John Joseph Magufuli, pole Sana Madam President, hakika hayakuwa haya maisha ya dunian, ila ni kitu Cha kupita tuh, na mbora miongon mwetu kwenye macho ya Mwenyezmungu ni yule ambae ni mchamungu.

Nakupa pole na kukuombea Sana,kwani umepokea kijiti Cha uongoz katika kipindi kigumu Sana, ambacho Taifa lilikuwa kwenye mtanziko, na mgawanyiko mkubwa Sana ambao kila mwananchi mwenye uelewa amekuwa anauona, siyo wafanyabiashara, wafanyakaz, wakulima na hata wajasariamali wakubwa na wadogo,bila kusahau wanasiasa na vyombo vya habari.

Pamoja na changamoto zilizopo mbele yako Wananchi wenye nia njema na Taifa hili tupo pamoja nawewe na siku zote tutakuombea KWA Mola akusimamie katika shughuli zako za kuliongoza Taifa.

Leo,nitaenda kwenye kipengele nyeti Sana,ambacho kinakuhusu wewe kuunda serikali yako madam president.

Nakupa pole Sana,katika mtihan mkubwa ambao utakutana nao ni jicho la waz waz la kuangaliwa KWA UDINI katika uteuzi wako,mama hii ni cancer ambayo sidhan kama utafanikiwa kuipata tiba yake zaid zaid ya kupiga moyo konde,kusimama kwenye haki,usawa na kuangalia weledi wa nani unamuhitaj katika kujenga serikali yako.

Kipindi ambacho Mh Jakaya Kikwete akiwa MADARAKANI,pamoja na kwamba kwenye serikali yake alikuwa fair kwenye teuzi zake na kuunda serikali yake,hakuachwa salama kuandamwa KWA waraka mbali mbali kumtuhum kuwa amekuwa akifanya teuzi zake KWA upendeleo wa kiiman,pamoja na ukweli kwamba katika teuzi hizo nafas nyingi alizitoa KWA haki na kuwapa nafasi nyingi ndug zetu hawa hawa christians bado ilionekana kuwa ana elements za udini.

Hali kama hiyo ya malalamiko hatukuiona Kabisa kutoka kwao katika utawala wa mkapa wala Magufuli pamoja na kwamba ukweli upo waz kuwa walipewa Sana wao nafas,hukuwahi kuwaskia waislam wakilalamika kuhusu teuzi hizo,na hata pale inapotokea baadhi wakihoji majibu yanayokuja ni kwamba waislam mtulie na hamna elimu,hiyo ni kasumba ambayo imejengeka kwa muda mrefu Sana, na haijengi kama Taifa.

Last week, ulifanya uteuzi ambao katika uteuzi huo yalionekana majina ya waislam kama wanne katika watu nane nadhan uliowateua ikazuka taharuki kwenye mitandao ya jamii, instagram, Twitter na hata huku JamiiForum kuwa eti awamu hii wavaa makubazi na barakashia ni awam yao, maneno ya chuki na kuudhi kabisa, na unaweza dhan huyo anaetoa mada kama hizo ni minority lakin amin kwamba anawakilisha views za wengi Sana ambao hawana tuh ujasir wa kusimama na kuongea chuki kama hizo.

Unafanya Tena uteuzi juz hapa,katika teuzi hizo hakuna jina hata moja la Muislam,wao wote wapo kimya Na hakuna taharuki yoyote iliyozuka na hujaskia malalamiko yoyote hata kutoka kwa waislam, siyo kama waislam hatuoni hilo,tunaona ila tunaingiwa na hali ya iman na kuchukulia kuwa kasumba ambayo hata tufanye nini hawa ndugu zetu hawawez kuiondoa fikran mwao,nadhan ni kasumba ambayo imegongwa muhuri ndani ya mioyo yao na wao nahis wanarithisha kizaz baada ya kizaz, it's sad.

Katika kukupa pole juu ya hilo rai yetu ni kukuomba,kwanza Simama kwenye haki,usiangalie udini,usiangalie ukanda wala ukabila,

Mkristo akiwa na qualifications na ukaridhika nae mpe nafas kwani huyo ni mtanzania, Muislam akiwa na qualifications na ukaridhika nae mpe nafas kwani huyo ni mtanzania pia.

Pamoja na kwamba ndan ya hii serikali wamejaa wao ila wakionekana waislam kadhaa tuh sehemu flan utaskia taasisi flan kuna udini, neno hilo udini limewekwa hapo Ili kukandamiza haki za watanzania hawa ambao ni Waislam wasionekane kwa namna yeyote katika hizo positions za uteuzi na utumishi hususan katika sekta ya umma.

Madam president, kuwa huru kumchagua team yako, hata kama wapo waislam wengi ambao unaona wako smart na competent kufanya nao kazi, usiache kuwapa nafas eti kwa kuhofia kuwa watapiga kelele za udini, hawa hawakuanza leo na hawatokuja kumaliza leo, ni muda SASA umefika kujifunza kuish nao kama walivyo na hiyo kasumba yao.

VYOVYOTE VILE IWAVYO MADAM PRESIDENT, WE SHALL STAND BEHIND YOU, KWA HILA NA CHUKI WATAZAOZIANZISHA KATIKA KUKUONDOA KWENYE MSTARI WA WEWE KUTENDA HAKI NA KUONGOZA TAIFA HILI.

RAMADHAAN KAREEM MADAM PRESIDENT.
 
Mkuu naungana na wewe kwa 100%.

Pia napenda kuongezea, sio tu wafuasi wa Christians ndio watalalamika na kupiga kelele za UDINi kwenye TEUZI. La hasha, ategemee pia waraka wa viongozi wao na waraka wa aina hiyo utapata 'airtime' kubwa ili kufanikisha ajenda yao.

Mwisho; asimame kwenye khaki, na asijaribu hata siku moja kuwajibu au kutumia Taasisi/Baraza la Dini kuwajibu ikitokea siku amealikwa na wala asimuagize Waziri Mkuu kutumia misikiti kujibu kitu chochote kinachohusiana na UDINI.
 
Mkuu naungana na wewe kwa 100%.

Pia napenda kuongezea, sio tu wafuasi wa Christians ndio watalalamika na kupiga kelele za UDINi kwenye TEUZI. La hasha, ategemee pia waraka wa viongozi wao na waraka wa aina hiyo utapata 'airtime' kubwa ili kufanikisha ajenda yao...
Umeongea sahihi Sana mkuu,

Madam president,asimame kwenye haki na usawa,siku zote hataweza pendwa na watu wote,

Jesus himself wapo ambao hawamkupenda even though he was just preaching a word of god,sembuse yeye?madam president
 
Hivi uislamu au ukristo unatambulika kwa Majina au KWA KUYAFUATA NA KUYAISHI MAFUNDISHO YA DINI\IMANI HUSIKA?!
 
Hivi uislamu au ukristo unatambulika kwa Majina au KWA KUYAFUATA NA KUYAISHI MAFUNDISHO YA DINI\IMANI HUSIKA?!

Umeongea point, utaweza kumtambua Muislam au mkristo kwanza KWA JINA lake, baada ya hapo ndipo utaujua uhakika wake kuwa ni muumin kweli wa hiyo dini au la, that's why hawa ndug zetu walipoona majina tuh yenye muelekeo wa arabic kwenye huo uteuzi wakaconclude kuwa ni Waislam wameanza kupendelewa.
 
Weww mwenyewe mdini, sifa za kumshauri Samia unazitoa wapi?

Ofcoz I am a Muslim that's why unaniita mdini,ushawahi sikia mkristo anaitwa mdini?

Si ndiyo KWA maana hata madam president SAMIA mnaanza kumtazama KWA jicho la udini now,but Magufuli hamkumtazama KWA jicho la udini kipindi kile,yes I know Mimi ni mdin,and I am proud of that
 
Back
Top Bottom