Nice story Mentor!!ni somo zuri kwa watu wanaoendekeza uzinzi na kutoka nje ya ndoa hata kwa sisi ambao hatujaingia kwenye ndoa,majaribu na misukosuko wanayopitia wanandoa ni foundation nzuri ya kujenga uhusiano madhubuti na imara kwasababu unachallenge subira na uvumilivu wao,pamoja na kujiifunza mapungufu ya wenza hao!
- Ustahamilivu na kusameheana ni mambo muhimu sana kwenye mahusiano yoyote. mwallu has a big heart and true love it takes a lot of courage to go through what she did and still hold on and stay strong...ijapokuwa Mentor alinogewa na kusahau hata kwanini alimuoa yule alomuoa na si huyo mlimbwende mwengine!TAMAA MBELE MAUTI NYUMA!!Ni vyema tukajifunza jinsi ya kudhibiti tamaa zetu za kimwili!
- Ndugu sio watu wakutegemea 100% ukiwa na matatizo ndio unaona utu wa watu.. Ndio maana wazungu wanasema familiy ni wife,husband and children hao wengine ni relatives.
- Ulifanya jambo la maana kuandika ile barua ya wosia..cause you can never predict the future so we should always be prepared for anything..like having enough savings now while we flourishh..
- Felix is a true friend,sio sifa kuwa na marafiki chungu nzima,binafsi bora niwe na rafiki mmoja tu ambae namuamini na najua ni rafiki wa kweli AKUFAAYE KWA DHIKI NDIO RAFIKI
Thank you so much kwa kuwa mkweli . Wanawake ni viumbe tofauti sana Eeee Mungu wabariki wanawake wote na uwaongezee moyo wa kusamehe na uvumilivu zaidi.
Thanks kwa ku appreciate who we are (Women)..we tend to forgive so easily
Heveni is such a bad girl....am sure she will fix it by tomorrow...
hii story inafanana na wimbo mmoja huwa nausikisikia kaimba mwanamke sijui anaitwa nani....wimbo mrefu sana,kwenye AUDI yule dada aliimba VOGUE....
...Very true Mkuu Mentor halafu penzi likakolea kupita kiasi...Ukiwaambia watu nilikutana na mupenzi wangu wa moyo Bar wanakuangalia kama hawakuelewi vile.....Chezeya Penzi weye!!!! Una kipaji kikubwa sana Mkuu cha uandishi, usinisahau kunipatia copy utakapoamua kuandika kitabu chako cha kwanza.
Story inafanana kabisa na wimbo wa bahati bukuku usikilize utaskia yote hayo aliyesema anaenda nje ya nchi alikuwa anaenda kuangalia mpira ila hongera mtoa mada kwa kuweza kuielezea vizuri
Siku ya kufa nyani miti yote haikubali idandiwe
nimeipenda
Mwisho imedhihirisha kuwa kimfaacho mtu chake
mwekundu ssssshhhhhhh.... #kimyakimyaMentor you are so strategic like PK!!mwallu sijui kama atakataa tena hapo ,kwa sababu kapata bonge la bwana!!
Mentor hii Kweli ni story na kwa Kweli ina kila sababu ya kuwa kwenye hili jukwaa na sitakuwa na la kuongeza maana AshaDii kashamaliza yote
Ndoa na iheshimiwe na watu wote na kumpata mke mwema na atakayekupenda haswa katika kipindi kigumu na cha shida ni jambo jema sana
Naona unapredict kitu kitakachotokea baada ya miaka miwili ya ndoa yako ila angalia yasikupate Kama haya uliyoyaandika mkuu Mentor
Siku ya kufa nyani miti yote haikubali idandiwe
Thank you so much kwa kuwa mkweli . Wanawake ni viumbe tofauti sana Eeee Mungu wabariki wanawake wote na uwaongezee moyo wa kusamehe na uvumilivu zaidi.
Nimecheka hapo ulipokutana na panga la huyo Mkurya....
Ko mkeo alikusamehe yakaisha....Zulekha nae aliishia wapi na mumewe.......
Hakukuwa na haja ya kuquote hadithi yote tena...
Uko serious kabisa mkuu?
Hebu fanya haraka kuomba radhi kabla hayajakukuta...
Babu DC!!
Mleta uzi uache tabia za KDF wa westgate ...kwa ufupi story ni kutoka kwenye wimbo wa Bahati Bukuku ...
Jamani haya mambo mengine kama utani vile lkn kwenye jamii yamekuwepo sana. Hili ni fundisho kwa wanaume wasio waaminifu kwenye ndoa zao na pia thamani ya mke ni kubwa mno yaweza shinda hata thamani ya ndugu. Lakini nani anajali alarm za aina hii kila mara zinagonga hakuna anaetaka kusikia. Pia najiuliza hivi Mentor ungekuta mwallu kafanya hayo je ungemsaidia kweli. Mwanamke ana role kubwa sana kwenye familia. Halafu jamani mahusiano ya kale haifai kuyachokoza kwani bond zingine huwa ni ngumu kuziharibu cha msingi ni kukaa mbali nazo na ikiwezekana kuacha kabisa mawasiliano wala kujua kinachojili ulikotoka wewe songa mbele usitazame nyuma.
Mkuu Mentor sitaki kuwa biased na sitaki kuonekana napendelea upande wowote ila ningekuwa sina hiyo ningesema sisi wanaume tuna sijui kimdudu kinatekenya mara kwa mara. Maana unaweza ukawa na mwanamke amekamilika kila idara na anakupenda sana na anakupa kila unachokihitaji ila bado macho yetu yanatambaa kuangalia kila ndege arukaye twamtaka
Haijalishi tuko kwenye ndoa wala single au bachelor mzoefu ila hatuishi tamaa. Hatujali maumivu wanayopata wenzetu wakati wanapogundua kuwa tunacheat tena na vitu ambavyo havina Hata uzuri wa wake zetu. Hatuoni Kama tunawaumiza wenzetu ila huwa tunajifikiria wenyewe na tamaa zetu. Na mwanaume mwenzako akiwa na kitu kizuri bado tunakionea wivu natamani ningekuwa nacho mimi na sio yule yaani BAK akiwa na kitu kizuri Mr Rocky roho inadunda kwa nini nisingekuwa nacho mimi. Nitatafuta kila njia nikipate au Hata kuwa nacho one night stand ndo hayo ya Mtambuzi na mke wa mjeda
Muhimu ni kuwa heshimu ndoa yako na heshimu hisia za mwenzako jiweke kwenye moyo wake anavyoumia atakaposikia au kujua kuwa unamsaliti
Mentor ulikuwa na kila kitu Kutoka kwa mwallu ila tamaa zikakufanya utamani vya nje na kukumbushia vya zamani ambavyo ushaviacha tangu umetoa kiapo cha kuwa na huyu peke yake. Kumbe kiapo kile ulikuwa ni upepo tuu upite hukumaanisha ni mbaya sana.
Mentor, it is a great story, I have enjoyed reading it. Hongera sana, kuna mengi ya kujifunza hapa.
Hii story inafundisha haya:-
1. Ni muhimu sana kupatia kuoa mwanamke ambaye kweli anafaa kuwa mke. Ni mwanamke mwerevu na mwenye busara pekee anaweza pita kwenye mtihani huu kama alivyoweza kufanya Mwallu, ki ukweli; wengine wangeweza kuacha Mentor ujifie after all anakuwa na hasira kuwa umemsaliti.
2. Sijui watu huwa wanatumia vigezo gani kudhania mwanamke na mwanaume ni sawa. Wanaume wanao tembea na wake za watu wana risk kubwa sana, tena hasa kama hayo mahusiano ni long term, kheri hata wale ambao wanakuwa wamegusa siku moja na kupotea kabisa (sina maana kuwa ni acceptable). Mke wa mtu ni sumu jamaniii... Kaka/baba zetu yapaswa muwe waoga katika hilo. Ni hatari!
3. Wazazi wana umuhimu katika maamuzi yetu ya kila siku. Lakini unapokuwa ni mtu mzima inapaswa kuji emancipate kuwa na uwezo wa kuchagua na kusimamia maamuzi yako. Pengine huyo shombe shombe angefanikiwa kuolewa na wewe asingekusaliti kwa mwanaume mwingine maana inaonyesha wazi (tokana na story uliyotoa) alikuwa anakupenda.
4. Wanaume acheni kupenda dezo na kutaka mteremko. Unatoka na mke wa mtu, huoni aibu jamani hata nafsi kukusuta kwenda kulala kitanda alicho nunua mwanaume mwenzio na kwenda kuvitumia vitu vyake hapo nyumbani? Unaridhika na kujiachia kabisa kana kwamba ni kwako? In such cases ni kheri wale wenye uwezo mtoke nje ya mji kabisa (narudia sina mana kuwa na support - naelezea facts).
5. Wanawake ni muhimu kutambua na kujua thamani ya mume. Hata kama humpendi hata kama hakuridhishi si haki kabisa kumdhalilisha kwa kutembea na mwanaume mwingine tena kwenye nyumba ambayo kakujengea/pangia yeye na mnaishi naye.
6. Kwa wanandoa... Ndoa si mteremko. Na ndoa huimarika zaidi tokana hasa na misuko suko muipatayo na mkafaulu kupitia hayo majaribu. Kwa stori kama hii, naamini kwa kiasi kikubwa Mentor ni lazima ashike adabu, awe mpole, aongeze mapenzi na kujikita katika kuhakikisha anamfurahisha mkewe. Maana Mentor kapata bahati ya kuelewa na kuona ni to what length mkewe anampenda, kumthamini na kuwajibika kama mke mwema.
7. Kwa mwanamke yeyote yule katika ndoa ni muhimu akatambua umuhimu wa kuacha walau kanafasi kadogo sana katika imani ya kuwa mumeo anaweza kukuangusha ama kukuumiza kwa namna moja ama nyingine. Hili husaidia pale matatizo kama haya yakitokea unakuwa una nguvu ya maamuzi sahihi wakati wa kutafakari tukio. Mwallu alizimia, kwa mwingine magonjwa kama pressure yanaweza ibukia hapo hapo sababu tu uliweka imani yako yote hapo. Nisinukuliwe vibaya kuwa wanaume hawaaminiki: ila naomba nieleweke kuwa ni rahisi kuumizwa nae hasa kama unampenda na pengine hata kama na yeye pia anakupenda.
Pamoja Saana.
Yani we Mentor wewe. Yani mi na wewe tunahitaji kuwa na serıous talks.
BTW huyo dokta kama mkeo angekuwa Heaven on earth sidhani kama angetoka salama. LOL
Siku zote nlijua mwallu ni sista wa Paroko.... kumbe kijana hatare sana weye