Barua kwa Mke Wangu...

Barua kwa Mke Wangu...

Mentor

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2008
Posts
20,334
Reaction score
23,940
...A Letter to My Wife...


28[SUP]th[/SUP] January 2019, Monday

Ni miaka miwili sasa imepita tangu tufunge ndoa na mke wangu, Asante. Binti mrembo na mcha Mungu. Mahali tulipokutana mimi na yeye ni hadithi ambayo nitaomba kuwasimulia siku nyingine. Ni katika zile sehemu ambazo mtu kamwe usingetegemea/tarajia kumpata binti mwenye haiba kama zake (We found love in a hopeless place…Rihanna Cc: BAK).

Kama nilivyokwisha eleza hapo mwanzo, zaidi ya urembo wake,ambao hauringii wala kuutumia vibaya kama wengine, ni binti mmoja mpole ajabu, anajua kujali na anajituma. Ni mchango mkubwa katika maisha yangu kwani hapa nilipofika kama sio mawazo na changamoto zake basi sidhani kama hata robo yake ningefika. Ama hakika wahenga hawakukosea waliposema, ‘kosea njia utaelekezwa, ila ukikosea mke…’

Naam, ni siku tena ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwangu na pia kumbukumbu ya miaka miwili ya ndoa. Ndoa tuliyofunga January 28, 2017 siku ya Jumamosi..still fresh in my mind. Ni siku ambayo kwa kawaida ya watu walio katika ndoa, tena ya ‘Kikristo’ walitakiwa kuwa pamoja wakimshukuru Mungu kwa mbali alipowafikisha.

Haikuwa hivyo kwangu. Wiki mbili kabla ya siku hii nilikuwa nimeshapanga na Zulekha (shombeshombe again!damn me) kukutana. Zulekha aliwahi kuwa rafiki yangu wa kike tulipokuwa chuoni. Ni binti aliyelelewa katika maadili ya dini sana. Very strict na kwa hiyo mahusiano yoyote ya kimapenzi na mwanaume asiye wa Kiislamu yalikuwa mwiko/kiwicho/taboo kwao.

Ila ukweli ni kuwa mapenzi hayafungwi na dini, hivyo tuliendelea kuwasiliana na tupatapo nafasi kufanya yasotupasa kufanya japo kwa siri kubwa. Baada ya kumaliza chuo, Zulekha alichumbiwa na kuolewa na Mkurya mmoja mfanya biashara aishiye Kimanzichana. Tuliendelea kuwasiliana na mara moja moja kucheza mechi za wizi pindi ambapo mumewe yupo safarini. Nami miaka minane mbele nilibahatika kumpata huyu mke wangu ambaye leo tunatimiza miaka miwili ndani ya ndoa.

Alinipigia simu kunijulisha kuwa mumewe amesafiri kwenda Geneva hivyo kama ningeweza niende walau tukumbushie kwani ulikuwa ni muda mrefu sana umepita tangu tukutane. Nami bila kumuwaza mke wangu nikamkubalia na kumjulisha kuwa ningesafiri Jumapili ya tarehe 27 kwa kisingizio cha safar ya kikazi Mtwara.

Na hivyo ndivyo nilivyomuaga mke wangu kipenzi. Alisikitika kuwa nisingekuwepo siku ya kuadhimisha miaka miwili ndani ya ndoa yetu changa. Ilinibidi kutumia one of those magic words, “Sorry babes, I will make it up to you when I come back.” Alinisaidia kupaki na kunisindikiza hadi Mbagala rangi tatu nikapande basi ili yeye arudi na gari letu nyumbani, an Audi A3 sportback, one of my favorites.

Nilipanda basi la Hamanju kuelekea Mtwara ingawa kondakta alikuwa akifahamu kituo changu cha ukweli. Hivyo tulikubaliana nikampa alfu kumi anishushe kimanzichana kituoni ambapo nilimkuta Zulekha akiningoja kwa hamu ndani ya ki-vitz alichonunuliwa na mumewe.

Tulienda hadi kwake ambapo hatukupoteza muda na kuanza kulicheza game kwani tulikuwa na zaidi ya miezi tisa hatujawahi onana kabisa. Ulikuwa ni mtanange wa kukata na shoka na mtoto kutotumwa dukani kwa takribani dakika hamsini hivi ndipo kipenga cha kwanza kilipopulizwa kuashiria muda wa mapumziko.

Uchovu wa safari, mgongano wa mawazo kwa jinsi nilivyomuacha mke wangu, pamoja na uchovu wa mechi vilichangia kuingia katika dimbwi la usingizi ambao kwa mara ya kwanza nahisi siku hiyo sikukoroma. Nilikuja kustuka nasikia maumivu makali kwenye paji la uso. Kufumbua macho nilikutana na sura ya Mkurya mwenye hasira kali akiwa kashikilia panga mkononi. Hasira yake tu ilinitosha kuzimia kwa hofu ila nilijikaza na kutaka kunyanyuka ambapo alinizaba na ubapa nikajikuta nimejikunyata pembeni mwa kitanda.

Kumbe Mkurya yule alipoaga anaenda Geneva alimaanisha tu anaenda zake Arusha ila kilichonikera mimi ni tabia yake ya ‘kutokutanguliza koti nyumbani.’ Wakati nakua babu alituhadithia kuwa zamani walipokuwa wakirudi kutoka safari za mbali iliwabidi wafikapo kijiji kimoja kabla ya nyumbani kutanguliza koti lake kwa mkewe kupitia mmojawapo wa watoto wa kijiji hicho kuashiria kuwa mwenye ynumba yu karibu. Hii ilimpa mke nafasi ya kusafisha nyumba na kama kuna kidumu ndani kuhakikisha kinaondoka na mke kujiandaa kumpokea mumewe. Walijua hali kama hizo hazina budi kutokea, ila haikuwa sababu ya kumfuamia mkewe.

Babu alituambia zama zetu zimebadilika lakini kutanguliza koti ni muhimu ila kwa kipindi chetu kutanguliza koti ni sawa na kupiga simu siku moja kabla ya kufika, “Mke wangu, kesho natarajia kuondoka hapa Arusha saa mbili asubuhi kurudi nyumbani.” Inatosha! Ghafla kabla sijaweza kuzama zaidi kwenye mawazo mwanaume yule alinvamia na kuanza kunikata vibaya mikononi na panga lile la kichwani ndilo lilinipoteza fahamu kabisa.


Back at home, Msongola…

Mke wangu naye alipokea simu iliyomtaarifu kuwa mumewe yu mahututi Muhimbili kutoka kwa namba asiyoifahamu na kabla hajamuuliza ni nani simu ilikatwa. Alipata shida kufahamu kuwa nilipata ajali au ni nini hasa kwani kwa kawaida huwa ni mvivu kuangalia taarifa ya habari mpaka nimlazimishe. Hivyo hakufahamu kama jana yake kulitokea ajali yoyote au la.

Aliondoka haraka na kuja hospitali ambapo alipoulizia kuhusu mgonjwa aliyeletwa usiku wa kuamkia tarehe 28 kwa ajali hakuna aliyempatia jibu. Kwa haraka alimpigia simu dr. Kindonga na kumuuliza kama amepata taarifa zozote kuhusu mumewe. Dr. Kindonga naye alimjibu hana taarifa na hawezi kufuatilia kwani alikuwa akijiandaa na mitihani yake ya mwisho ya Masters.

Baada ya kuhangaika sana alifanikiwa kufika mapokezi ICU na kuwakuta manesi ambao waliona aibu hata kumweleza baada ya kuwatajia jina langu. Walimwambia tu, “Yupo ndani!” bila kutaja sababu ya mimi kuwepo huko.
Alifika ndani na kunikuta nimefungwa bandeji uso mzima…


Kuanzia hapa anasimulia mke wangu kipenzi: mwallu

Moyo ulinipasuka na kushindwa kuelewa ni nini hasa kilimpata mume wangu Mentor. Sikuweza kumuangalia hata mara mbili kwani machozi yalinitoka ghafla. Nilijikuta nikianguka chini na kupoteza fahamu. Nilishtuka niko mikononi mwa nesi aliyejitambulisha kwangu kama Samira. Alinitaka nikaze moyo nikajue jinsi ya kumtibu mume wangu kwani kwa hali aliyonayo alinihitaji nikiwa hai kuliko mfu. Baadaye nilikuja kugundua Samira alikuwa very sympathetic kwa kuwa hakuwa amefahamu nini hasa kilimsibu mume wangu.

Nilijikaza na kwenda mpaka kitanda alicholazwa Mentor. Zaidi ya macho yake na pua zilizotiwa mirija kila sehemu, huko kwingine kulikuwa kumezibwa kabisa. Daktari alikuja na kujitambulisha;

Dokta: “Habari dada, naitwa Dokta Chrispin”

Mimi: “Shikamoo dokta, naitwa Asante. Dokta nini kimempata mume wangu?”

Dr. Chrispin
(Akakohoa kwanza): “Mh! Dada (ingawa kwa vigezo vyote angetosha kuwa babu yangu!), pole sana. Mumeo alipatwa na ajali. Alifumaniwa na kupigwa ndo unamuona ha… ”

Dokta Chrispin hakumalizia sentensi ile nikazimia tena kwa mara ya pili (ingawa ilikuwa ni afadhali kwani nilikuwa nipige ukunga wa kufa mtu). Nilishtuka nipo ofisini kwa Dr. Chrspin nimelala kwenye examination bed yake. Alikuja kunipima mapigo ya moyo na kunibembeleza huku kanikumbatia kifuani mwake. Nililia sana na baada ya kutulia ndipo aliponimalizia mkasa wote. Sikuamini kama mume wangu Mentor angeweza kufanya vile. Sikuamini kama katika siku zote basi ingekuwa siku ya kumbukumbu ya ndoa yetu. Sikuamini hadi nilipooneshwa jalada la Polisi likielezea kila kitu kwa kinaga ubaga.

Dr. Chrispin alinitaka niende nyumbani nikaongee na ndugu na jamaa ili kupanga mipango ya matibabu kwani gharama zake zilikuwa kubwa kiasi kutokana na majeraha aliyoyapata hasa kichwani. Nilichukua nguo zake nikaziweka kwenye begi ambalo nilikuwa nimemsaidia kupaki asubuhi ya jana yake na kurudi nyumbani.

Nilianza kuwapigia simu kaka zake. Kaka yao wa kwanza Laurian alishtuka kwanza ila baada ya kumuhadithia mkasa wote alinijibu kuwa hawezi kutoa pesa kwa ajili ya upumbavu wa mtu mmoja na isitoshe anajenga. Familia yake haiwezi kuishi nyumba ya kupanga. Alimalizia kwa kusema, “Huyo mumeo nilishamuonya mara nyingi sasa basi umalaya wake usiniletee umaskini kwenye familia yangu.”

Kaka Kabezi, ambaye baada yake ndiye Mentor alizaliwa, alikuwa mtu wa pili kumjulisha. Yeye kwa kejeli kabisa aliniambia, “Shem, afe tu tukurithi!”

Nililia sana usiku ule nikashindwa hata kula wala kunywa chochote. Ni bahati tu mtoto wetu Cedric alikuwa kwa bibi yake.

Nilijaribu kuwapigia wifi zangu walau wao wangeweza kunisaidia kwani walionekana zaidi kumpenda kaka yao na walikuwa karibu naye kuliko kaka zao wengine. Mawifi nao hawakuwa msaada wowote kwangu.

Wifi mkubwa, Suraya, aliniambia hatoweza kunisaidia kwani anajiandaa kwenda nje ya nchi asubuhi kesho. Wifi anayefuatia, Dora, sista du kweli alinijibu hatoweza kutoa chochote ila ataleta chakula hospitali na kuanzia siku hiyo akawa hapokei tena simu yangu. Wifi mdogo, tena afisa wa Jeshi la Magereza, aliniambia yuko radhi kwenda kumlipia mfungwa atoke gerezani kuliko kutibu Malaya. Na Malaya huyu ni kaka yao, mume wangu. Moyo uliniuma sana nikakosa cha kufanya.

Marafiki zake; Willian, Alfred, Livingstone, Salvatory, Shabani, Peter, Aneth, Arnold, Dotto, Mary, Christine na wengine wengi wote walijifanya kuwa bize au hawana uwezo wa kumsaidia ilhali hao hao walikuwa marafiki wake wakubwa akiwa mzima.

Wengine kama kina Alfred na Willian walidiriki kunitongoza kabisa kwa ahadi za kunisaidia. Nilimlilia Mungu na kumuomba aniepushe na jaribu hili. Nilimuomba anioneshe mlango mwingine wa kutokea kwani niliamini upo. Ukweli nilishindwa kuomba muda mrefu kwani niliishia kulia na kulala hapo hapo nilipo.

Huku hospitali Dr. Chrispin akaanza kunisumbua nifanye haraka kwani nikichelewa sana mume wangu hatapona hata akifanyiwa hiyo operation. Ikanibidi kwenda kumlilia Dr. Chrispin.


1[SUP]st[/SUP] February 2019, Friday

Niliwahi hospitali kwenda kumhudumia mume wangu ambaye hadi wakati huo alikuwa amelazwa tu ICU bila matibabu yoyote ya ziada. Nilienda kumwangukia Dr. Chrispin kumuomba anisaidie. Nilikuwa nimekuja na ile Audi ya mume wangu nikamwambia dokta ikiwezekana achukue hiyo amtibu mume wangu na akipona tutamlipa fedha la asipopona basi aichukue gari hiyo. Dr. Chrispin alinijibu tu, “Dada, hizo gari zipo chache sana hapa nchini nitakuwa chambo cha kuibiwa na kuuwawa mimi.” Akakataa katukatu akaniambia; “Ila dada…ukinifikiria vyema nitakusaidia ” Hukuhitaji PhD kumuelewa mzee yule asiye na haya. Ila kwa muonekano pia wa sura yake alikuwa serious.

Nilirudi nyumbani kwa majonzi makubwa kwani dokta Chris ndo alikuwa tegemeo la mwisho katika matumaini yangu ya kumuokoa mume wangu kipenzi. Nilianza kutafuta ATM cards za mume wangu walau nikaangalie ana kiasi gani kimebaki benki na kama kinaweza kutosha kusaidia kulipia matibabu yake. Kumbe ndugu zake walipokuja kunisalimia waliondoka na kadi zote za benki. Ilikuwa ni kama wameshaamua ndugu yao afariki. Sikukuta chochote kwenye wallets zake ila wakati narudishia kadi nyingine kwenye wallet ndipo kikadondoka kikaratasi kilichokunjwa vizuri. Ilikuwa ni barua;

“Mke wangu kipenzi,

Kama unaisoma barua hii ni dhahiri kuna jambo baya limenikuta. Na zaidi sana najua litakuwa linahusika na umalaya wangu. Najua kuomba msamaha sitakuwa nimekusaidia kwa lolote. Ila ni ombi langu unisamehe, zaidi sana kwa mzigo ambao nitakuwa nimekutwisha.

Umalaya wangu umeniponza mke wangu na kamwe nisingependa kosa langu hilo liwe mzigo kwako mke wangu. Jitahidi kuwataarifu ndugu zangu watakusaidia. Kaka zangu na dada zangu pamoja na marafiki zangu. Kwa bahati nzuri unafahamiana nao vyema mke wangu.

Pia unaweza kuuza hiyo audi yangu itasaidia kwa gharama zozote hata ikitokea nimefariki. Tafadhali mke wangu, nyumba hiyo niliiandikisha kwa ownership ya mwanetu ili kwa vyovyote vile ndugu wasijaribu kukuibia. Usiiuze.
Mke wangu kipenzi (hata sidhani kama bado nastahili kukuita hivyo!), kama yote yakishindikana tafadhali usifanye jambo lolote zaidi ya hilo litakalokufanya ujutie maisha mbeleni. Ni heri uniache nife kwa dhambi zangu kuliko kutenda dhambi nyingine kuniokoa mimi. Najua ulivyo mzuri mke wangu, Asante. Watakutongoza wengi wakati huu wakijua una shida, tafadhali sana mke wangu usiwakubalie. Narudia tena, ‘Ni heri nife kwa dhambi zangu walau nitakuwa mfano wa kutoigwa kwa wengine wenye tabia kama yangu.’

Jambo la mwisho mke wangu. Yote hayo yakishindikana rudi kwa Mungu wako unayemuamini na uniombee mke wangu. Hiyo ilikuwa moja ya sababu iliyonivuta kwako. Mlilie yeye akusaidie kwani hawa wa duniani wote wakishindwa kusaidia basi ama kwa hakika Mungu yule niliyekufahamu ukimuamini atakusaidia.

Nisamehe tena mke wangu na niombee msamaha kwa mwanetu Cedric ikitokea nimefariki.

Wako,
Mentor.”

Ilimaliza barua hiyo na kunifanya nijisikie mnyonge kuliko alivyotarajia mume wangu.

Ila jambo moja katika ile barua lilinitia moyo, alipoongelea imani yangu. Nikajiuliza I wapi imani yangu? Nikajilaumu kwa kwenda kutafuta msaada kwa binadamu. Nakumbuka nilipiga magoti pale pale na kumlilia Mungu kuwa mimi mja wake sikustahili adhabu na aibu kama ile. Ni kweli mume wangu nampenda kama ahadi yetu ya ndoa ilivyosema, ‘kwenye shida na raha’ . Nikamwambia Mungu kama kweli yu pamoja nami basi katika jaribu lile anipe mlango wa kutokea.

Kwa mara ya kwanza siku ile tangu ajali ya mume wangu niliweza kuomba muda mrefu bila kulia. Nilijihisi kama naongea naye uso kwa uso. Naam, Mungu hakupi jaribu lililo juu ya imani yako wapendwa kwani katika ndugu na marafiki zake wote nilioongea nao nilimsahau Felix. Huyu aliwahi kufanya kazi na mume wangu wizara moja wakati wameanza kazi baada ya kumaliza chuo. Yeye alisikia kwa watu kuwa rafiki yake amepata ajali akaja moja kwa moja nyumbani na kuniuliza kama nina shida yoyote nikamueleza kila kitu ila ukweli ni kuwa moyoni nilikuwa na wasiwasi asijekuwa kama wenzake akaanza kunitongoza pia.

Felix aliniambia yeye kama yeye asingeweza kunisaidia ila kuna Msambaa mmoja, Iggy, anamfahamu anaweka bond magari kama niko tayari tukaweke bond Audi ya mume wangu nipewe pesa ya kumtibu. Nilikubali na siku hiyohiyo jioni mume wangu alifanyiwa operation na Dr. Chrispin. Ilimchukua miezi minne kupona kabisa na kurudi nyumbani. Gharama ambazo kwa hakika hatukuweza kulipa hivyo ilibidi walichukue gari lake pamoja na cellica niliyokuwa nimenunua mwaka 2013 kwa mkaka mmoja hivi. Ingawa ni kama alinihonga kwa bei aliyoniuzia.

Ama hakika mke wa mtu sumu wapendwa ila pia Mungu ni mweza wa yote.:amen: Sikujua kama mume wangu katika hali ile aliyokuwa nayo angeweza kupona na kama ningeweza kupata msaada wowote.


Wasalaam wapendwa,

Mentor & mwallu.
 
Last edited by a moderator:
Nimecheka hapo ulipokutana na panga la huyo Mkurya....

Ko mkeo alikusamehe yakaisha....Zulekha nae aliishia wapi na mumewe.......
 
Mentor, it is a great story, I have enjoyed reading it. Hongera sana, kuna mengi ya kujifunza hapa.

Hii story inafundisha haya:-

1. Ni muhimu sana kupatia kuoa mwanamke ambaye kweli anafaa kuwa mke. Ni mwanamke mwerevu na mwenye busara pekee anaweza pita kwenye mtihani huu kama alivyoweza kufanya Mwallu, ki ukweli; wengine wangeweza kuacha Mentor ujifie after all anakuwa na hasira kuwa umemsaliti.

2. Sijui watu huwa wanatumia vigezo gani kudhania mwanamke na mwanaume ni sawa. Wanaume wanao tembea na wake za watu wana risk kubwa sana, tena hasa kama hayo mahusiano ni long term, kheri hata wale ambao wanakuwa wamegusa siku moja na kupotea kabisa (sina maana kuwa ni acceptable). Mke wa mtu ni sumu jamaniii... Kaka/baba zetu yapaswa muwe waoga katika hilo. Ni hatari!

3. Wazazi wana umuhimu katika maamuzi yetu ya kila siku. Lakini unapokuwa ni mtu mzima inapaswa kuji emancipate kuwa na uwezo wa kuchagua na kusimamia maamuzi yako. Pengine huyo shombe shombe angefanikiwa kuolewa na wewe asingekusaliti kwa mwanaume mwingine maana inaonyesha wazi (tokana na story uliyotoa) alikuwa anakupenda.

4. Wanaume acheni kupenda dezo na kutaka mteremko. Unatoka na mke wa mtu, huoni aibu jamani hata nafsi kukusuta kwenda kulala kitanda alicho nunua mwanaume mwenzio na kwenda kuvitumia vitu vyake hapo nyumbani? Unaridhika na kujiachia kabisa kana kwamba ni kwako? In such cases ni kheri wale wenye uwezo mtoke nje ya mji kabisa (narudia sina mana kuwa na support - naelezea facts).

5. Wanawake ni muhimu kutambua na kujua thamani ya mume. Hata kama humpendi hata kama hakuridhishi si haki kabisa kumdhalilisha kwa kutembea na mwanaume mwingine tena kwenye nyumba ambayo kakujengea/pangia yeye na mnaishi naye.

6. Kwa wanandoa... Ndoa si mteremko. Na ndoa huimarika zaidi tokana hasa na misuko suko muipatayo na mkafaulu kupitia hayo majaribu. Kwa stori kama hii, naamini kwa kiasi kikubwa Mentor ni lazima ashike adabu, awe mpole, aongeze mapenzi na kujikita katika kuhakikisha anamfurahisha mkewe. Maana Mentor kapata bahati ya kuelewa na kuona ni to what length mkewe anampenda, kumthamini na kuwajibika kama mke mwema.

7. Kwa mwanamke yeyote yule katika ndoa ni muhimu akatambua umuhimu wa kuacha walau kanafasi kadogo sana katika imani ya kuwa mumeo anaweza kukuangusha ama kukuumiza kwa namna moja ama nyingine. Hili husaidia pale matatizo kama haya yakitokea unakuwa una nguvu ya maamuzi sahihi wakati wa kutafakari tukio. Mwallu alizimia, kwa mwingine magonjwa kama pressure yanaweza ibukia hapo hapo sababu tu uliweka imani yako yote hapo. Nisinukuliwe vibaya kuwa wanaume hawaaminiki: ila naomba nieleweke kuwa ni rahisi kuumizwa nae hasa kama unampenda na pengine hata kama na yeye pia anakupenda.


Pamoja Saana.
 
Aisee ni hadithi nzuri yenye mafundisho ndani yake mwenye masikio na asikie
 
Nimecheka hapo ulipokutana na panga la huyo Mkurya....

Ko mkeo alikusamehe yakaisha....Zulekha nae aliishia wapi na mumewe.......
Hahahahahahahaha jamani mambo mengine yanachekesha achene tu . Unajua mimi ninacheka pale manesi walipokua wanamwambia mlengwa kisa cha mumewe na mume kuzimika lol.
 
Hahahahahahahaha jamani mambo mengine yanachekesha achene tu . Unajua mimi ninacheka pale manesi walipokua wanamwambia mlengwa kisa cha mumewe na mume kuzimika lol.

hahaa bora hata wangemdanganya kwanza..we unadhani alipata ajali wakati


anaelekea Mtwara halafu unaambiwa ni kufumniwa..hapo waweza zimia tu
 
..asiyejua kusoma ni mjinga kabisaa akipata barua huitembeza kuwtwa hodo hodiiiiii tuseme barua ilitoka kwa "MENTOr"....
 
hahaa bora hata wangemdanganya kwanza..we unadhani alipata ajali wakati


anaelekea Mtwara halafu unaambiwa ni kufumniwa..hapo waweza zimia tu
Jamani haya mambo mengine kama utani vile lkn kwenye jamii yamekuwepo sana. Hili ni fundisho kwa wanaume wasio waaminifu kwenye ndoa zao na pia thamani ya mke ni kubwa mno yaweza shinda hata thamani ya ndugu. Lakini nani anajali alarm za aina hii kila mara zinagonga hakuna anaetaka kusikia. Pia najiuliza hivi Mentor ungekuta mwallu kafanya hayo je ungemsaidia kweli. Mwanamke ana role kubwa sana kwenye familia. Halafu jamani mahusiano ya kale haifai kuyachokoza kwani bond zingine huwa ni ngumu kuziharibu cha msingi ni kukaa mbali nazo na ikiwezekana kuacha kabisa mawasiliano wala kujua kinachojili ulikotoka wewe songa mbele usitazame nyuma.
 
Last edited by a moderator:
Mahir: Mento mke wa mtu sumu.
Mento: Aaaa, wapi! Mi nina maziwa.
Ona sasa, sijuwi maziwa yamekatika na kuwa mtindi. Ila ndiyo siku ya kufa nyani tena ivoo....
 
pretty artistic style,,hongera xana mwenye macho na aone na mwenye masikio na asikie,,ila leo hii kupata mwanamke kama huyo sijuii wote candyshop"after money"
 
Khaaah Mentor

Kweli hii ni barua
Usiwe mvivu kama babu Asprin wewe...isome umuite na mumeo Erickb52 na mashemeji zako Arushaone na Filipo na LiverpoolFC waisome...maana yaweza wakuta haya!

Mentor, it is a great story, I have enjoyed reading it. Hongera sana, kuna mengi ya kujifunza hapa.

Hii story inafundisha haya:-

1. Ni muhimu sana kupatia kuoa mwanamke ambaye kweli anafaa kuwa mke. Ni mwanamke mwerevu na mwenye busara pekee anaweza pita kwenye mtihani huu kama alivyoweza kufanya Mwallu, ki ukweli; wengine wangeweza kuacha Mentor ujifie after all anakuwa na hasira kuwa umemsaliti.

2. Sijui watu huwa wanatumia vigezo gani kudhania mwanamke na mwanaume ni sawa. Wanaume wanao tembea na wake za watu wana risk kubwa sana, tena hasa kama hayo mahusiano ni long term, kheri hata wale ambao wanakuwa wamegusa siku moja na kupotea kabisa (sina maana kuwa ni acceptable). Mke wa mtu ni sumu jamaniii... Kaka/baba zetu yapaswa muwe waoga katika hilo. Ni hatari!

3. Wazazi wana umuhimu katika maamuzi yetu ya kila siku. Lakini unapokuwa ni mtu mzima inapaswa kuji emancipate kuwa na uwezo wa kuchagua na kusimamia maamuzi yako. Pengine huyo shombe shombe angefanikiwa kuolewa na wewe asingekusaliti kwa mwanaume mwingine maana inaonyesha wazi (tokana na story uliyotoa) alikuwa anakupenda.

4. Wanaume acheni kupenda dezo na kutaka mteremko. Unatoka na mke wa mtu, huoni aibu jamani hata nafsi kukusuta kwenda kulala kitanda alicho nunua mwanaume mwenzio na kwenda kuvitumia vitu vyake hapo nyumbani? Unaridhika na kujiachia kabisa kana kwamba ni kwako? In such cases ni kheri wale wenye uwezo mtoke nje ya mji kabisa (narudia sina mana kuwa na support - naelezea facts).

5. Wanawake ni muhimu kutambua na kujua thamani ya mume. Hata kama humpendi hata kama hakuridhishi si haki kabisa kumdhalilisha kwa kutembea na mwanaume mwingine tena kwenye nyumba ambayo kakujengea/pangia yeye na mnaishi naye.

6. Kwa wanandoa... Ndoa si mteremko. Na ndoa huimarika zaidi tokana hasa na misuko suko muipatayo na mkafaulu kupitia hayo majaribu. Kwa stori kama hii, naamini kwa kiasi kikubwa Mentor ni lazima ashike adabu, awe mpole, aongeze mapenzi na kujikita katika kuhakikisha anamfurahisha mkewe. Maana Mentor kapata bahati ya kuelewa na kuona ni to what length mkewe anampenda, kumthamini na kuwajibika kama mke mwema.

7. Kwa mwanamke yeyote yule katika ndoa ni muhimu akatambua umuhimu wa kuacha walau kanafasi kadogo sana katika imani ya kuwa mumeo anaweza kukuangusha ama kukuumiza kwa namna moja ama nyingine. Hili husaidia pale matatizo kama haya yakitokea unakuwa una nguvu ya maamuzi sahihi wakati wa kutafakari tukio. Mwallu alizimia, kwa mwingine magonjwa kama pressure yanaweza ibukia hapo hapo sababu tu uliweka imani yako yote hapo. Nisinukuliwe vibaya kuwa wanaume hawaaminiki: ila naomba nieleweke kuwa ni rahisi kuumizwa nae hasa kama unampenda na pengine hata kama na yeye pia anakupenda.


Pamoja Saana.

Salaam dada AshaDii,
I am humbled and thanks for the contribution.

Ila shukran kubwa na za kipekee zimwendee mke wangu kipenzi mwallu ( Cc: Kaizer na mwekundu ) kwa kunikubali hata baada ya yote haya...love u babes, I certainly will make it up to u soon.
 
Last edited by a moderator:
Ablessed na Heaven on earth nawaapia na ajitokeze mwanaume atakayejibu kuwa atamsamehe mkewe kama mwallu alivyonifanyia....iDoubt kama yupo. Women r a special kind of creation. #respect

Afu we heveni umenieka pending sana ujue....bin waiting tangu juz sio furesh ivo.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom