Barua kutoka kwa Mtanzania aliyefungwa Hong Kong kwa kukamatwa na Madawa ya Kulevya

Ufungwe kwa amani mkuu.........ukitoka usibebe simu za kichina hazitaruhusiwa tena kuanzia June
 
Kama hajawataja waliombebesha hayo madawa anakuwa hajatusaidia bado katika vita hii.
 
Really!? ''..Usilete madawa Hongkong au Bara la Asia''.

I think this letter is strategically designed to pose threat/warning to drug-traffickers in attempt to reduce the size of the problem... In my thinking, it could possibly be written by Tz embassy or Hongkong with an intention of discouraging the business...

I may be wrong anyway..
kwa jinsi yeyote iwayo, hio biashara haifai.........
 
pole sana , na nife na umaskini wangu, na hiyo shida hata ije na mapanga bado sifanyi hiyo biashara, ntasimama na mungu wangu ambae ndie aliempa Bakhresa na Mengi, najua kwa juhudi zangu ntafika pale ninapotaka hata kama ni pole pole muhim sijastop na sikati tamaa.
Unazijua shida unaziskia
 
Story ya huyu mdada ina kitu kina miss kuifanya authentic..... kilichomfanya abebe unga ni school fees tu au tamaa ya kuendesha X6 kama Masanja?
Anyway, yameisha mkuta, lakini sijui kama angerudi fresh tungeweza kupata story hii jamvini. Na hata aandikeje au serikali ijitahidi kupiga vita biashara hii, bado vijana wengi wanatafuta opportunity ya kuwa "punda" kubeba mzio kupeleka china amabako anajua wanaua. Wana neno watumialo "woga wako ni umaskini wako"
Siamini utafiti wake wa drug traffickers kwamba watanzania tuko juu zaidi, sio kweli ukweli ni kwamba West Africans na South Americans ndo vinara wa biashara hii. Mtanzania unakuta kakamatwa na kilo 1 au mbili, lakini hawa wenzetu ni kilo 20 hadi 50.
 
Tanzania yangu hadi nashindwa kuelewa, madawa ya kulevya kutoka Tanzania inamaana Tanzania ndipo yanapozalishwa au yameingizwa kwa wingi hadi imeanza kuhudumia na dunia pia?au ndo tafsiri ya Tanzania kuitwa shamba la bibi?
Chakushangaza kingine mtuhumiwa kaongea porojo nyingiiiiii mwisho wa siku hakutaka hata kumtaja aliyemtuma,asa unajiuliza mtu huyo amepanga kuisaidia nchi yake kweli au mpango ni kuendelea kuteketeza vijana??
Ningekuona kweli unamapenzi ya dhati ya nchi yako na vijana wenzako kama ungemtaja aliye kutuma ili ashughulikiwe yeye kwanza.
 
Kama hajawataja waliombebesha hayo madawa anakuwa hajatusaidia bado katika vita hii.

Yes, imekuwa tabia yetu kufikiri tukiyafanya "jumla" majanga ya kitaifa na kutoa nasaha za ujumla kwa wananchi kuwa wema basi masuala hayo kama kukithiri kwa tatizo la madawa ya kulevya Tanzania litatoweka mara raia wakiamua "kuwa wema". Hili suala ni jinai kubwa au ufisadi mkubwa unaofahamika vizuri sana. Na vinara wanaoendesha biashara hiyo kufikia kiwango cha Tanzania kupata sifa ya kuwa notorious duniani ni ama viongozi wakubwa au watu wenye sauti sana serikalini.

Kazi kubwa inatakiwa ifanyike kuwazima hao ma-don. Kuasa watanzania wasifikirie kusafirisha madawa ni sawa na kauli ya "utii wa sheria bila shuruti" au kuwaomba majambazi wafikirie athari za vitendo vyao; wabadilike na kuwa watu wema. Ni kauli za kuvutia lakini mwisho wake ni hapo tu - kuvutia. Tusisahau kuwa walioasisi usimamizi wa sheria na vyombo vya dola kuwa sehemu muhimu sana ya utawala makini hawakuwa wajinga. Hulka ya binadamu inafahamika karne na karne. Jamii ina watu wa kila aina. Nasaha za ujumla bila udhibiti haziwezi kuwa na tija. Badala yake zinazalisha kejeli toka kwa mafisadi. Kwa kifupi, tulicho nacho hapa Tanzania ni "systems failure". Tuone labda kama hayo matumaini yaliyowekezwa kwa mtu mmoja: Magufuli, yatatoa tija.
 
Sababu za kujiingiza katika biashara hii si maisha magumu. Wazee wetu walikuwa na maisha magumu maradufu ya yetu. Sababu kubwa ni hizi:
1- Tamaa ya utajiri wa haraka haraka
2- Ukosefu wa maadili ya kiroho
3- Kukithiri kwa vijana wenye 'bora elimu' na si elimu bora
4- Uvivu wa kufikiri (janga kubwa sana Tanzania ambapo fursa nyingi zilizopo hazionekani)
5- Utawala mbaya hasa wa awamu ya nne (umefanya kuiba, rushwa, ufisadi... kuonekana kuwa ni 'ujanja')
6- Kukithiri kwa tabia ya uongo (angalia namba 2)
7- Drug Lords
 
Fr John Wotherspoon is a "Verified User", and is well known for his efforts in the fight against drug trafficking! He has visited Tanzania and has visited families of Tanzanians imprisoned in HK. Do you have a substantial reason to doubt him?
Maybe or maybe not. Mtu anaweza kum quote Colin Powell vizuri, lakini anaandika Naigeria. Unaweza kufikiri barua imekuwa dictated.
 
Back
Top Bottom