Shukrani A. Ngonyani
JF-Expert Member
- Feb 23, 2014
- 1,179
- 2,004
Ndugu Maxence,
Salaam,
Pole na hongera kwa kipindi hiki unachopitia, ni kipindi kigumu lakini ni kipindi cha kujenga ujasiri na kukokomaza kifikra na msimamo.
Ndugu Maxcence wakati wewe umelala ktk kuta nene na ndefu za magereza, kwa "kosa" la kuweka jukwaa la kutoa maoni, mawazo na habari kwa matakwa ya ibara ya 18(1-1V) ya katibu huku ,kuna Wenzako wanakula raha.
kuna wezi wa ESCROW wapo wamelala na wake zao, wezi wa IPTL wamelala na mahawara zao, waliotupiga pesa ya radar wamelala na vimada wao, huku wewe uliyeweka jukwaa la kufichua uovu huo ukiwa nyuma ya milango ya chuma na kuta nene za magereza.
Wengi tulitarajia na tulijua kuwa wale malaika wa kufungia mitandao ya kijamii wataangukia Jamiiforums.
Jitahidi Kuwa mvumilivu wakati huu ambapo "malaika" wanakushikilia huku "mungu" wao akiwa kimya kama hajui kinachoendelea huku ikifahamika malaika wametumwa na mungu.
Ndugu Mello, tafadhali upatapo barua yangu nakuomba tulia utafakari na utambua unapigana vita muhimu sana tena muhimu kuliko hata maisha na roho yako.
Unalinda uhuru wa kutoa mawazo, maoni na kupashana habari, hivyo si suala dogo, kuwa mvumilivu, kuwa mzalendo, unaipigania Tanzania, Tanzania ni muhimu kuliko roho yako. hata hao mawakala wakikuua usijali, damu yako itakuwa imetumika kama wino wa kuandikia maneno mawili, UHURU na UKOMBOZI.
Hakika unaumia na unateseka sana kwa unayopitia, usife moyo, ukifa moyo tutaumia wengi, ni bora uvumilie upweke wako na mateso yako huko gerezani.
Ndugu yangu Maxcence tafadhali pokea pole, shukrani na pongezi kutoka kwangu.
Jisikie uko nasi hapo ulipo!
salaam!
Shukrani Ngonyani
Lilongwe.