Barrick yaweka masharti kulipa Dola milioni 300

Tuangalie vizuri wanachosema Barrick kwenye kugawana 50/50.

Yaani, hiyo 50% ya Tanzania ni: Gawio letu 16%, Kodi yetu 30%, na mrahaba wetu 4%. Sasa hapo jipya sana na tunaloshangilia sana ni lipi, au labda mimi ndio mshamba na huwa sipambanui mambo haraka?
Kwa hyo kuhusu kugawana faida itakuaje
 
Yaani, Mimi nasikia oooh oooh ndumba za MziziMkavu na mshana jr zinafanya kazi mbona wasitupatie tuwawekee hawa wazungu koko?

Kwa nini wanatusumbua wakati wametuibia?

Sasa hayo mashimo yatakayobakia sisi tutayazibia kwa mchanga wa baharini au tutatengeneza maziwa; Ziwa North Mara, Ziwa Bhughyakulu, Ziwa Geita na ziwa sijui lingine liwe Ziwa Mwadui and the like?

Serikali, ikomae kuwa wametubadilishia tena gia angani na tufunge migodi yote maana hamna namna tena kama wanaanza huu uduanzi.
Kazi kwenu hapo hakuna cha uchawi wala nini wanachotaka wazungu muwasikilize kwa njaa yenu mukubali wawape pesa wanazo taka kuwapa.Ili na nyinyi muwape mali zenu nipe nikupe hakuna uchawi hapo ni biashara tu ifanyike kwa makubaliano.
 
Dar es Salaam.
Licha ya kupata hasara kwenye robo ya tatu ya mwaka, kampuni ya Barrick imetenga dola 300 milioni za Marekani (zaidi ya Sh660 bilioni) kuilipa Serikali, lakini imeweka sharti; inataka iruhusiwe kusafirisha makinikia.

Acacia, kampuni tanzu ya Barrick na inayomiliki migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, imezuiwa tangu mwezi Machi kusafirisha mchanga huo wa madini kwenda kuuyeyusha nje ya nchi kwa ajili ya kupata mabaki ya dhahabu, shaba, fedha na madini mengine yaliyoshindikana kuchenjuliwa migodini.

Baada ya majadiliano baina ya Serikali na Barrick, kampuni hiyo ya Canada ilikubali kulipa dola 300 milioni “kuonyesha uaminifu”.

Taarifa ya miezi mitatu ya Barrick (Julai-Septemba) iliyotolewa juzi, inaonyesha kuwa ilipata hasara ya dola 11 milioni (zaidi ya Sh24 bilioni) tofauti na faida ya dola 175 milioni (zaidi ya Sh385 bilioni) iliyopata katika kipindi kama hicho mwaka jana (dola moja ya Kimarekani ni sawa na takriban Sh2,200 za Tanzania).

“Kupungua kwa mapato kunatokana na kushuka kwa uzalishaji na bei ya dhahabu pamoja na zuio la kusafirisha makinikia ambalo Serikali ya Tanzania iliiwekea Acacia,” inasema ripoti hiyo.

Vilevile, Barrick inasema kupungua kwa mapato yake kumechangiwa na ongezeko la makadirio ya kodi yanayofika dola 172 milioni (zaidi ya Sh378 bilioni) zilizopendekezwa kwenye majadiliano ya mustakabali wa operesheni za Acacia nchini.

Wakati Barrick ikitenga kiasi hicho cha kodi, Acacia ina dola 128 milioni (zaidi ya Sh282 bilioni) na kufanya jumla ya dola 300 milioni zilizokubaliwa kwenye mazungumzo yaliyofanyika kwa miezi mitatu iliyopita.

Masharti hayo si ya kwanza, itakumbukwa kwamba siku chache baada ya mkutano wa kukabidhi ripoti ya majadiliano hayo, kampuni ya Acacia ilisema haiwezi kulipa Dola 300 milioni kwa mkupuo na kwamba Barrick inajua hilo.

Ofisa fedha mkuu wa Acacia, Andrew Wray alinukuliwa na vyombo vya habari akisema: “Hatuna huo uwezo kuilipa Tanzania ili tumalizane kwenye mgogoro wa kodi uliopo.”

Wray alisema hayo Oktoba 20 wakati Acacia ilipokuwa ikiwasilisha ripoti yake ya fedha kwa robo ya tatu ya mwaka iliyoishia Septemba, ikionyesha kushuka kwa mapato na faida ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Barrick imeiunga mkono Acacia kwenye msimamo wake kuhusu malipo hayo ya dola 300 milioni ikisema: “Kutokana na hali ya Acacia kifedha, malipo haya yanapaswa kufanywa kwa awamu yakitegemea mauzo ya dhahabu na usafirishaji wa makinikia.”

Katika robo hiyo ya tatu, faida ya Acacia imeshuka kwa asilimia 70 kutoka dola 52.878 milioni (zaidi ya Sh116.331 bilioni) mpaka dola 16.038 (zaidi ya Sh35.283 bilioni).

Wakati wa mkutano na vyombo vya habari uliofanyika Ikulu, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi ambaye alikuwa mwenyekiti wa wawakilishi wa Serikali alisema Barrick wamekubali kutekeleza masharti yote ya sheria mpya ya madini.

Lakini kwenye taarifa yake, kampuni hiyo inasema itaendelea kuzungumza na Serikali ili kuondoa zuio la kusafirisha makinikia na kwamba mazungumzo hayo yataenda sambamba na kutafuta suluhu ya deni la kodi la kiasi cha dola 190 bilioni (zaidi ya Sh424 trilioni) ambazo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeitoza Acacia ikiwa ni malimbikizo ya kodi, faini na riba.

“Tunatarajia mazungumzo haya yatakamilika ndani ya nusu ya kwanza ya mwaka ujao,” inasema Barrick.

Pamoja na hasara hiyo ya robo ya tatu, kwa miezi yote tisa, Barrick imepata faida ya dola 1.752 bilioni (zaidi ya Sh3.854 trilioni) ambayo ni zaidi ya mara saba ikilinganishwa na iliyopata kwa muda kama huo mwaka jana. Mwaka uliopita, ilitangaza faida ya dola 230 milioni (zaidi ya Sh506 bilioni).

Mbali na taarifa hiyo ya fedha, Barrick imefafanua kwa wadau wake kuhusu makubaliano yaliyoafikiwa kwenye majadiliano ya miezi mitatu baina yake na Serikali.

Makubaliano

Kwenye ripoti hiyo, Barrick inasema imekubaliana na Serikali kuhusu mfumo mpya wa uendeshaji ambao, endapo utaridhiwa, utatoa mwelekeo mpya wa shughuli za Acacia nchini. Barrack imefanya mazungumzo hayo kwa niaba ya Acacia kwa kuwa ndiye mmiliki mkuu wa hisa, ikimiliki asilimia 63.9.

Lakini, pamoja na ukweli huo, inasema chochote kitakachoafikiwa kitapaswa kutathminiwa na kuthibitishwa na Acacia kabla ya utekelezaji, ingawa Barrick inaamini makubaliano yaliyofikiwa yataleta suluhu ya mgogoro uliopo kwenye uchimbaji wa dhahabu nchini.

Mgogoro kati ya kampuni ya Acacia, mchimbaji na msafirishaji mkubwa wa dhahabu ya Tanzania, na Serikali ulishika kasi Machi baada ya kampuni hiyo kuzuiwa kusafirisha mchanga wa madini.

Baadaye Rais John Magufuli aliunda kamati mbili kuchunguza kiwango cha madini kilichokuwa katika makontena 270 yaliyokuwa Bandari ya Dar es Salaam, athari za kuusafirisha kwenda nje, sheria na mikataba.

Kamati hizo zilisema zimebaini kiwango cha dhahabu ni mara kumi ya kile kilichotangazwa na Acacia, kukwepa kodi na kukiuka sheria, huku mikataba ikionekana kunufaisha wawekezaji.

Ripoti hizo zilisababisha mawaziri kuwajibishwa na baadaye Serikali na Barrick kukubaliana kuunda timu za majadiliano, ambayo yalijikita katika muundo na mfumo mpya wa uendeshaji wa kampuni tanzu za Barrick, kubadilisha uendeshaji wa biashara ya madini na kuwanufaisha zaidi wananchi wanaoizunguka migodi.

Mengine ni kubadilisha mikataba ya madini (MDA) ili iendane na sheria mpya kwa lengo la kuongeza ushiriki na mapato ya Serikali, pamoja na kuainisha fidia ya makosa ya Acacia. Makubaliano manne yalipata muafaka na la mwisho bado linajadiliwa.

“Kwa makubaliano haya tunaamini tutapata suluhu ya kudumu na operesheni za Acacia nchini Tanzania zitaendelea kama kawaida,” inasema taarifa hiyo.

Mgawanyo wa mapato
Alipokuwa akiwasilisha ripoti ya majadiliano hayo kwa Rais Magufuli, Profesa Kabudi alisema Barrick wamekubali kutekeleza masharti yote ya sheria mpya za madini.

Alisema kuanzia sasa mapato au faida itagawanywa sawa kati ya Acacia na Serikali.

Siku ya pili alitoa ufafanuzi zaidi ikisema: “Mgawanyo wa asilimia 50 kwa 50 wa faida ni baada ya tozo na kodi nyingine zote kulipwa. Kwa ujumla, Tanzania itapata asilimia 70 na Barrick asilimia 30. Kwingineko wanagawana asilimia 50 kwa 50 zikiwamo kodi, sisi tulikataa hilo.”

Lakini Barrick ikasema: “Mgao wa asilimia 50 za Serikali utahusisha mrabaha, kodi na asilimia 16 ya hisa itakazopewa kukidhi matakwa ya sheria mpya za madini.”




Chanzo; mwananchi

Hawa jamaa hawawezi kuendelea kutuwekea masharti.Sisi ni equal partners,infact tu zaidi ya wawekezaji,we have the real stuff,Gold.They bring to us the fake,useless,priceless papers printed by the US government called the US $ in exchange for the real thing,called Gold and then they attach strings,stupid.The government must be strict,they adhere to what is agreed upon,or pack and go.Strictly no export of soil where gold has not been extracted.Hatuwezi kuuziwa mbuzi kwenye gunia,that will be very stupid of us.
 
Hawa jamaa hawawezi kuendelea kutuwekea masharti.Sisi ni equal partners,infact tu zaidi ya wawekezaji,we have the real stuff,Gold.They bring to us the fake,useless,priceless papers printed by the US government called the US $ in exchange for the real thing,called Gold and then they attach strings,stupid.The government must be strict,they adhere to what is agreed upon,or pack and go.Strictly no export of soil where gold has not been extracted.Hatuwezi kuuziwa mbuzi kwenye gunia,that will be very stupid of us.
Mapema sana kwako kuanza kulialia, unaikumbuka comment yako hii ya jana, who is dancing now.
Mtahangaika sana,lakini the bottomline is,mliyotaka yawe hayakuwa na hata hayatakuwa.Mlisema tutapelekwa kwenye International Court of Arbitration, hatukupelekwa.Mkasema hatutatalipwa tutalipwa.Sasa mmebaki kucheza na lini tutalipwa.Hiyo siyo ishu,ishu ni kwamba they are dancing to our tune,we are not dancing to their tune anymore.Hayo ni mafanikio makubwa.Asiyeona mafanikio hayo ana shida kubwa.
 
Mapema sana kwako kuanza kulialia, unaikumbuka comment yako hii ya jana, who is dancing now.
Mkuu hawa watalipa,we have the upper hand.We just have to tighten our strings.Remember that their Tanzanian mines are the most profitable and they have made massive capital investment at Bulyankulu etc.Quinine, there is no way these fellows can pack and go,Tanzania is their lifeline.Yes I repeat,they will dance to our tune.
 
Kazi kwenu hapo hakuna cha uchawi wala nini wanachotaka wazungu muwasikilize kwa njaa yenu mukubali wawape pesa wanazo taka kuwapa.Ili na nyinyi muwape mali zenu nipe nikupe hakuna uchawi hapo ni biashara tu ifanyike kwa makubaliano.


Duuiuuuuuuuuuh, huuuuuh huuuuuuuh.

Basi, MziziMkavu , hakuna namna ngoja tuendelee kupambana hadi mwisho japo tutashinda ila siku zitakuwa zimesonga kidogo.
 
Mbona Mh Rais alisema walipe haraka hizo hela yeye ana kazi nazo, itakuwaje sasa?

Kweli Posa si Ndoa.
Juz si amesema HERA ANAZO ZA KUTOSHA?
1.Kujenga reli
2.Kujenga mradi wa umeme
3.Kununua ndege 6
Sasa za Bariki anazitaka haraka kivipi?
 
Kusafirisha makinikia hakuna tatizo iwapo watadeclare viwango halali vya Copper, Silver and Gold vilivyopo kwenye makinikia kama vilivyobainishwa na kamati ya Prof Mruma.
Watawezaje kuclear bila mashine za kuchenjulia,?

Movie ndo imeanza, kishikauchumba lazima kitutoe jasho.
 
Kusafirisha makinikia hakuna tatizo iwapo watadeclare viwango halali vya Copper, Silver and Gold vilivyopo kwenye makinikia kama vilivyobainishwa na kamati ya Prof Mruma.

Ndoto ni nzuri sana, haswa pale unapoiota mchana. Endelea na ndoto. "Professorial Rubbish".
 
Kwani wakiruhusiwa kusafirisha makinikia yenye sifa ya kuitwa makinikia kuna shida gani hapo-hili swala si lipo kimkataba na pia kuna sheria mpya ambayo inaelezea umilikaji wa madini ambatano ambayo siyo dhahabu.
Embu twendeni taratibu wakuu
 
Back
Top Bottom