Barrick yaweka masharti kulipa Dola milioni 300


miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Messages
1,514
Likes
2,587
Points
280
miss zomboko

miss zomboko

JF-Expert Member
Joined May 18, 2014
1,514 2,587 280
Dar es Salaam.
Licha ya kupata hasara kwenye robo ya tatu ya mwaka, kampuni ya Barrick imetenga dola 300 milioni za Marekani (zaidi ya Sh660 bilioni) kuilipa Serikali, lakini imeweka sharti; inataka iruhusiwe kusafirisha makinikia.

Acacia, kampuni tanzu ya Barrick na inayomiliki migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi, imezuiwa tangu mwezi Machi kusafirisha mchanga huo wa madini kwenda kuuyeyusha nje ya nchi kwa ajili ya kupata mabaki ya dhahabu, shaba, fedha na madini mengine yaliyoshindikana kuchenjuliwa migodini.

Baada ya majadiliano baina ya Serikali na Barrick, kampuni hiyo ya Canada ilikubali kulipa dola 300 milioni “kuonyesha uaminifu”.

Taarifa ya miezi mitatu ya Barrick (Julai-Septemba) iliyotolewa juzi, inaonyesha kuwa ilipata hasara ya dola 11 milioni (zaidi ya Sh24 bilioni) tofauti na faida ya dola 175 milioni (zaidi ya Sh385 bilioni) iliyopata katika kipindi kama hicho mwaka jana (dola moja ya Kimarekani ni sawa na takriban Sh2,200 za Tanzania).

“Kupungua kwa mapato kunatokana na kushuka kwa uzalishaji na bei ya dhahabu pamoja na zuio la kusafirisha makinikia ambalo Serikali ya Tanzania iliiwekea Acacia,” inasema ripoti hiyo.

Vilevile, Barrick inasema kupungua kwa mapato yake kumechangiwa na ongezeko la makadirio ya kodi yanayofika dola 172 milioni (zaidi ya Sh378 bilioni) zilizopendekezwa kwenye majadiliano ya mustakabali wa operesheni za Acacia nchini.

Wakati Barrick ikitenga kiasi hicho cha kodi, Acacia ina dola 128 milioni (zaidi ya Sh282 bilioni) na kufanya jumla ya dola 300 milioni zilizokubaliwa kwenye mazungumzo yaliyofanyika kwa miezi mitatu iliyopita.

Masharti hayo si ya kwanza, itakumbukwa kwamba siku chache baada ya mkutano wa kukabidhi ripoti ya majadiliano hayo, kampuni ya Acacia ilisema haiwezi kulipa Dola 300 milioni kwa mkupuo na kwamba Barrick inajua hilo.

Ofisa fedha mkuu wa Acacia, Andrew Wray alinukuliwa na vyombo vya habari akisema: “Hatuna huo uwezo kuilipa Tanzania ili tumalizane kwenye mgogoro wa kodi uliopo.”

Wray alisema hayo Oktoba 20 wakati Acacia ilipokuwa ikiwasilisha ripoti yake ya fedha kwa robo ya tatu ya mwaka iliyoishia Septemba, ikionyesha kushuka kwa mapato na faida ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Barrick imeiunga mkono Acacia kwenye msimamo wake kuhusu malipo hayo ya dola 300 milioni ikisema: “Kutokana na hali ya Acacia kifedha, malipo haya yanapaswa kufanywa kwa awamu yakitegemea mauzo ya dhahabu na usafirishaji wa makinikia.”

Katika robo hiyo ya tatu, faida ya Acacia imeshuka kwa asilimia 70 kutoka dola 52.878 milioni (zaidi ya Sh116.331 bilioni) mpaka dola 16.038 (zaidi ya Sh35.283 bilioni).

Wakati wa mkutano na vyombo vya habari uliofanyika Ikulu, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi ambaye alikuwa mwenyekiti wa wawakilishi wa Serikali alisema Barrick wamekubali kutekeleza masharti yote ya sheria mpya ya madini.

Lakini kwenye taarifa yake, kampuni hiyo inasema itaendelea kuzungumza na Serikali ili kuondoa zuio la kusafirisha makinikia na kwamba mazungumzo hayo yataenda sambamba na kutafuta suluhu ya deni la kodi la kiasi cha dola 190 bilioni (zaidi ya Sh424 trilioni) ambazo Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeitoza Acacia ikiwa ni malimbikizo ya kodi, faini na riba.

“Tunatarajia mazungumzo haya yatakamilika ndani ya nusu ya kwanza ya mwaka ujao,” inasema Barrick.

Pamoja na hasara hiyo ya robo ya tatu, kwa miezi yote tisa, Barrick imepata faida ya dola 1.752 bilioni (zaidi ya Sh3.854 trilioni) ambayo ni zaidi ya mara saba ikilinganishwa na iliyopata kwa muda kama huo mwaka jana. Mwaka uliopita, ilitangaza faida ya dola 230 milioni (zaidi ya Sh506 bilioni).

Mbali na taarifa hiyo ya fedha, Barrick imefafanua kwa wadau wake kuhusu makubaliano yaliyoafikiwa kwenye majadiliano ya miezi mitatu baina yake na Serikali.

Makubaliano

Kwenye ripoti hiyo, Barrick inasema imekubaliana na Serikali kuhusu mfumo mpya wa uendeshaji ambao, endapo utaridhiwa, utatoa mwelekeo mpya wa shughuli za Acacia nchini. Barrack imefanya mazungumzo hayo kwa niaba ya Acacia kwa kuwa ndiye mmiliki mkuu wa hisa, ikimiliki asilimia 63.9.

Lakini, pamoja na ukweli huo, inasema chochote kitakachoafikiwa kitapaswa kutathminiwa na kuthibitishwa na Acacia kabla ya utekelezaji, ingawa Barrick inaamini makubaliano yaliyofikiwa yataleta suluhu ya mgogoro uliopo kwenye uchimbaji wa dhahabu nchini.

Mgogoro kati ya kampuni ya Acacia, mchimbaji na msafirishaji mkubwa wa dhahabu ya Tanzania, na Serikali ulishika kasi Machi baada ya kampuni hiyo kuzuiwa kusafirisha mchanga wa madini.

Baadaye Rais John Magufuli aliunda kamati mbili kuchunguza kiwango cha madini kilichokuwa katika makontena 270 yaliyokuwa Bandari ya Dar es Salaam, athari za kuusafirisha kwenda nje, sheria na mikataba.

Kamati hizo zilisema zimebaini kiwango cha dhahabu ni mara kumi ya kile kilichotangazwa na Acacia, kukwepa kodi na kukiuka sheria, huku mikataba ikionekana kunufaisha wawekezaji.

Ripoti hizo zilisababisha mawaziri kuwajibishwa na baadaye Serikali na Barrick kukubaliana kuunda timu za majadiliano, ambayo yalijikita katika muundo na mfumo mpya wa uendeshaji wa kampuni tanzu za Barrick, kubadilisha uendeshaji wa biashara ya madini na kuwanufaisha zaidi wananchi wanaoizunguka migodi.

Mengine ni kubadilisha mikataba ya madini (MDA) ili iendane na sheria mpya kwa lengo la kuongeza ushiriki na mapato ya Serikali, pamoja na kuainisha fidia ya makosa ya Acacia. Makubaliano manne yalipata muafaka na la mwisho bado linajadiliwa.

“Kwa makubaliano haya tunaamini tutapata suluhu ya kudumu na operesheni za Acacia nchini Tanzania zitaendelea kama kawaida,” inasema taarifa hiyo.

Mgawanyo wa mapato
Alipokuwa akiwasilisha ripoti ya majadiliano hayo kwa Rais Magufuli, Profesa Kabudi alisema Barrick wamekubali kutekeleza masharti yote ya sheria mpya za madini.

Alisema kuanzia sasa mapato au faida itagawanywa sawa kati ya Acacia na Serikali.

Siku ya pili alitoa ufafanuzi zaidi ikisema: “Mgawanyo wa asilimia 50 kwa 50 wa faida ni baada ya tozo na kodi nyingine zote kulipwa. Kwa ujumla, Tanzania itapata asilimia 70 na Barrick asilimia 30. Kwingineko wanagawana asilimia 50 kwa 50 zikiwamo kodi, sisi tulikataa hilo.”

Lakini Barrick ikasema: “Mgao wa asilimia 50 za Serikali utahusisha mrabaha, kodi na asilimia 16 ya hisa itakazopewa kukidhi matakwa ya sheria mpya za madini.”
Chanzo; mwananchi
 
malisoka

malisoka

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2012
Messages
1,428
Likes
1,606
Points
280
malisoka

malisoka

JF-Expert Member
Joined Jul 8, 2012
1,428 1,606 280
Ukipenda Boga penda na ua lake. Kama wanataka kuchimba madini na yatawapa faida waendelee na kazi na kama wanaona hailipi na kodo inawabana waondoke tu.
 
MastaKiraka

MastaKiraka

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2015
Messages
1,089
Likes
1,262
Points
280
MastaKiraka

MastaKiraka

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2015
1,089 1,262 280
Maigizo tu mwisho wa siku hayo makontena yenye Dhahabu na madini mengine ya Wizi lazima yasafirishwe. Hiyo dola mil 300 inatoka humo humo, then Tunaendelea kudanganyana na kuendelea kuita press conference za kuwapumbaza wa Tz
 
Nichumu Nibebike

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2016
Messages
8,807
Likes
15,124
Points
280
Age
34
Nichumu Nibebike

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2016
8,807 15,124 280
Kusafirisha makinikia hakuna tatizo iwapo watadeclare viwango halali vya Copper, Silver and Gold vilivyopo kwenye makinikia kama vilivyobainishwa na kamati ya Prof Mruma.
 
ze-dudu

ze-dudu

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Messages
8,661
Likes
7,723
Points
280
ze-dudu

ze-dudu

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2014
8,661 7,723 280
atawaruhusu tu maana izo pesa ana shida nazo
 
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
45,383
Likes
31,625
Points
280
Saint Ivuga

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
45,383 31,625 280
si walikubaliana kuwa wanajenga kinu hapa hapa? hawa jamaa wameshachoka.. Magu haya madini mpe Kagame
 
Jambazi

Jambazi

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2014
Messages
16,253
Likes
15,357
Points
280
Jambazi

Jambazi

JF-Expert Member
Joined Jan 18, 2014
16,253 15,357 280
Kazi kweli kweli......
 
Masiya

Masiya

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
5,105
Likes
3,431
Points
280
Masiya

Masiya

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
5,105 3,431 280
Mgawanyo wa mapato
Alipokuwa akiwasilisha ripoti ya majadiliano hayo kwa Rais Magufuli, Profesa Kabudi alisema Barrick wamekubali kutekeleza masharti yote ya sheria mpya za madini.

Alisema kuanzia sasa mapato au faida itagawanywa sawa kati ya Acacia na Serikali.

Siku ya pili alitoa ufafanuzi zaidi ikisema: “Mgawanyo wa asilimia 50 kwa 50 wa faida ni baada ya tozo na kodi nyingine zote kulipwa. Kwa ujumla, Tanzania itapata asilimia 70 na Barrick asilimia 30. Kwingineko wanagawana asilimia 50 kwa 50 zikiwamo kodi, sisi tulikataa hilo.”

Lakini Barrick ikasema: “Mgao wa asilimia 50 za Serikali utahusisha mrabaha, kodi na asilimia 16 ya hisa itakazopewa kukidhi matakwa ya sheria mpya za madini.”
Hili naona nalo itabidi wakae tena au kamati ndogo ije na ufumbuzi anacho ongea waziri ni tofauti na wanachosema barrick. Ningependa anayosema waziri ndo yawe lakini huenda ikawa ni ndoto kuliko ukweli. Tusubiri lakini hata hiyo ya Barrick iko poa bora gharama za uzalishaji "zisipikwe" kupitia transfer pricing.
 
samurai

samurai

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2010
Messages
5,174
Likes
5,597
Points
280
samurai

samurai

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2010
5,174 5,597 280
Watulipe hela zetu waache longolongo bwana....
 
Harrison Justine

Harrison Justine

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2015
Messages
1,140
Likes
524
Points
280
Age
56
Harrison Justine

Harrison Justine

JF-Expert Member
Joined Jun 19, 2015
1,140 524 280
Swali la nyongeza ni lini wanalipa
 
J

jojipoji koromije

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2017
Messages
788
Likes
1,032
Points
180
J

jojipoji koromije

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2017
788 1,032 180
Navyomjua Magu Muda Si Mrefu atatangaza kuitaifisha migodi yote. Subirini muone!!!! Huyu Mkoromije bado ana ubabe wa kisukuma ambao ni asili yetu. Hatupendi madharau especially pale tunapokuwa na madaraka!!!
 

Forum statistics

Threads 1,236,822
Members 475,301
Posts 29,269,023