Baridi ya Mbeya, Iringa, Arusha na kwingineko hapa Tanzania

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
4,105
2,498
Baridi ya wapi ni kali na tamu kwa wale waliobahatika kuzunguka sehemu mbili tatu au zote
 
Mkuu ukiwa ujafika sehem yenye baridi unaona baridi ni kitu cha kawaida ila ni heri ya joto kuliko baridi,mbeya baridi ni kali zaidi hasa maeneo ya mbeya mjini,pale arusha nia maeneo ya arusha mjini na tengeru kipindi cha mwezi wa saba baridi ni kali sana,iringa sijawai kufika ila nipo njiani naerekea uko
 
Mbeya kuna sehemu inaitwa kituro nahisi ndo mahali kwenye barid Kali kuliko sehemu nyingine hapa TZ.
 
Kuna sehemu inaitwa Kikeo msitu wa mjerumani ni sehemu flan za mkoa wa morogoro kata ya mgeta kule hapana hadi ukipita msituni unahisi mvua inanyesha kumbe ni miti inadondosha manyunyu.
 
Kuna sehemu inaitwa Kikeo msitu wa mjerumani ni sehemu flan za mkoa wa morogoro kata ya mgeta kule hapana hadi ukipita msituni unahisi mvua inanyesha kumbe ni miti inadondosha manyunyu.

Aisee, hiyo sehemu unafikaje? tupe ramani mkuu
 
Mbeya kuna sehemu inaitwa kituro nahisi ndo mahali kwenye barid Kali kuliko sehemu nyingine hapa TZ.

Ni kweli mdau. Mbeya inabaridi kali sana
Makambako kuna baridi yenye upepo
Njombe na Mafinga baridi hadi ganzi mwilini yaani ni shida!
 
baridi ya Njombe ni mateso kwa kweli...watu wanavaa makoti mazito 24/7
 
Makete huko njombe ndio funga kazi ikifuatiwa na kituro Mbeya... Huko makete barafu hudondoka kama ulaya
 
Arusha ndo kuna baridi kali na tamu hasa kipande cha Usa river maeneo ya ndani.

Katesh (manyara), Njombe, iringa, mbeya, makambako inaumiza sana. Inaambatana na upepo mkali na vumbi...

Kitulo kwa yale mandhari ingekua tamu km pangekua na hoteli za maana... na barabara.

Bashnet unakauka mno. Halafu ni pale mlimani tu mi naona. Bashnet hadi katesh huko wanalima sana vutunguu swaumu...
 
Aisee, hiyo sehemu unafikaje? tupe ramani mkuu

Kama unatoka moro mjini panda gari la mgeta kisha unafika mwisho wa gari panaitwa nyandira. Baada ya hapo utakodi boda boda hadi hapo msituni ni tshs elfu10 tu.
"Angalizo" kuna sehemu barabara haina tofauti na mlima kitonga ila ni pabaya zaidi halafu ina matuta kwa kifupi hakuna coaster wala hiace za kwenda mgeta ni mwendo wa 14B tu.
 
Back
Top Bottom