king'amuzi
JF-Expert Member
- Jan 10, 2011
- 614
- 225
wachome kwenye media na tafuta mwanasheria mzuri utafanikiwa.mpe pole!
Sheria inaweza ikawa upande wao kwenye hili, wewe uko responsible kwa cheque zote zinazodunda. Pesa inaweza kuingia hata siku hiyo hiyo kwenye account ila cheque inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kudunda.
Sasa kwa vile walikuambia kuwa baada ya siku 21 uko salama hii inaweza ikabadilisha kesi, ila tatizo ni katika ushahidi, je utaweza kuprove kuwa uliambiwa siku 21 zinatosha, je alipata ahadi hiyo katika maandishi? Mkienda mahakamani mashahidi watasemaje? etc
Scam za aina hii ni very common, unatumiwa cheque, unaipeleka benki inaclear, kisha aliyekutumia anakuambia mtumie some % kwa wire transfer kisha kilichobaki ni chako, ukishafanya hivyo baada ya muda benki inakwambia cheque imedunda, inakula kwako.
Kwa kifupi kupokea cheque ni hatari sana.
Wana JF nashukuru kwa mchango wenu, nimewasiliana na ndugu yangu kuwa aandae vielelezo vyote kwa ajili ya kuwapeleka mahakamani, lakini sasa naomba kama kuna mwenye kumjua wakili mzuri asiye na tamaa na asiyecheza double dill, basi tufahamishane ili hatua zaidi ziendelee,ntakuwa nawapa hatua kwa hatua juu ya hii kesi, nilimhadithia rafiki yangu mmoja mholanzi, akashangaa sana akaniuliza, kwani huko tanzania mawakili huwa wanafanya kazi gani? au hakuna?. nikamwambia wapo lakini hawajui wajibu wao kazi yao ni kufunga tai na suti halafu wanapiga mizinga kwa machinga
Sheria inaweza ikawa upande wao kwenye hili, wewe uko responsible kwa cheque zote zinazodunda. Pesa inaweza kuingia hata siku hiyo hiyo kwenye account ila cheque inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kudunda.
Sasa kwa vile walikuambia kuwa baada ya siku 21 uko salama hii inaweza ikabadilisha kesi, ila tatizo ni katika ushahidi, je utaweza kuprove kuwa uliambiwa siku 21 zinatosha, je alipata ahadi hiyo katika maandishi? Mkienda mahakamani mashahidi watasemaje? etc
Scam za aina hii ni very common, unatumiwa cheque, unaipeleka benki inaclear, kisha aliyekutumia anakuambia mtumie some % kwa wire transfer kisha kilichobaki ni chako, ukishafanya hivyo baada ya muda benki inakwambia cheque imedunda, inakula kwako.
Kwa kifupi kupokea cheque ni hatari sana.
Kuna ndugu yangu ana-bank na barclays bank,yeye ni mfanyabiashara wa kawaida tu.anauza bidhaa zake za kutoka china, hivi majuzi walikuja wateja kutoka comoro na wakahitaji bidhaa kwake lakini hawa wateja walikuwa hawana cash walikuwa na cheque ya bank yao ya comoro.
Huyu ndugu yangu akawaambia hawezi kupokea cheque labda mpaka awasiliane na watu wa bank ili wampe utaratibu. cheque ilikuwa ni ya ml 30, wale wacomoro wakamwambia hakuna shaka yeye achukue cheque na aende nayo bank. yule jamaa akachukua cheque na kwenda nayo bank ambayo ni barclays, akakutana na maofisa wa bank akawapa ile cheque
Wale watu wa bank wakamwambia kwa kawaida cheque international huwa inachukua muda wa siku 21 kumature. jamaa akaweka cheque bank ili asubiri siku 21, akarudi kwa wacomoro akawaambia kuwa hawatoweza kuchukua bidhaa zake mpaka siku 21 ziishe na awe ameona pesa zimeingia ktk account yake.
wale wacomoro wakakubali kusubiri, baada ya siku 21, jamaa alipocheki ktk account yake akakuta tayari pesa imeingia, akawapigia simu wale wacomoro waje wachukue bidhaa zao, wakachukua wakaondoka zao
baada ya wiki 2 barclays wakampigia huyu ndugu yangu simu, ati arudishe zile pesa na ati ile cheque ilikuwa fake, huyu jamaa yangu akaenda bank, akawauliza yeye ana makosa gani? barclays wakamwambia itabidi awatafute wale wacomoro wamrudishie bidhaa,hapo ndipo nilipochoka na bank za kibongo, hadi sasa hivi ninavyoandika hapa jamaa bado pesa zake zimeshikiwa na bank,
ANAOMBA MSAADA WA KISHERIA WANA JF
Major,
NimekuPM namba ya wakili anayefanya kazi benki ili aweze kukusaidia. Sidhani kama anaweza kukuchakachua.
na sitashangaa ikiwa Barclay's walisha wasainisha mkataba wateja wote wa kibongo kwamba ikitokea bifu yeyote kesi baraza la usuluhishi Uingerezaaaa! Lawyer wake wa kibongo stress zinaanza kwenye kutafuta nauli, visa, na mahala pa kufikia, akiingia kwenye kesi anaanza kushangaa shangaa wenzake wanatema cheche kwa kwenda mbele, by the time anatasfiri kichwani from english to kiswahili to kidengeleko then from kidengeleko to swahili to English arudishe majibu... nyundo la jaji buuum! Mshikaji anahukumiwa kuwalipa Barclay's!
ukipeleka cheque huwa wanarekodi siku ambayo wamepokea,
Kwa hiyo kama ni hivyo, basi kila anayelipwa kwa check anakuwa hajalipwa, kwa maana aliyekulipa anaweza kudil na watu wa benki halafu akarudishiwa pesa wakati wewe unakuwa umesha-delever bidhaa, nijuavyo mimi kama check imebaunzi, wanatakiwa wakurudishie check yako kabla hawajakulipa, ili upate ushahidi wa kumdai aliyekupa check, sasa huyu ndugu yangu,ameomba wamrudishie check yake, lakini wanasema check hawana, huu ni wiziTatizo sio siku waliyopokea wala siku waliyoweka pesa benki. Wewe kama mtu uliyepeleka cheque benki uko responsible kwa ile cheque yaani majukumu yote kuhusu uhalali wa ile cheque yako juu yako, na kuingia kwa hela kwenye account yako haimaanishi kuwa ile cheque ni halali.
Sasa kama walimhakikishia siku 21 zinatosha basi anaweza akawa na kesi,tatizo litakuwa kwenye kupata ushahidi kuwa walimhakikishia.
Yaani fikiria, kama majukumu yote yangekuwa ya Benki watu kibao wangeandika cheque zinazodunda kisha hela ikiingia wanazitumbua zote, Benki zingepata hasara sana.
Tatizo sio siku waliyopokea wala siku waliyoweka pesa benki. Wewe kama mtu uliyepeleka cheque benki uko responsible kwa ile cheque yaani majukumu yote kuhusu uhalali wa ile cheque yako juu yako, na kuingia kwa hela kwenye account yako haimaanishi kuwa ile cheque ni halali.
Sasa kama walimhakikishia siku 21 zinatosha basi anaweza akawa na kesi,tatizo litakuwa kwenye kupata ushahidi kuwa walimhakikishia.
Yaani fikiria, kama majukumu yote yangekuwa ya Benki watu kibao wangeandika cheque zinazodunda kisha hela ikiingia wanazitumbua zote, Benki zingepata hasara sana.
Benki wanapotoa muda kwa hundi ku-clear ni utaratibu waliojiwekea ili kuweza kuchunguza uhalali wa hundi hiyo pamoja na kuwasiliana na benki inayohusika kama mlipaji ana pesa kwenye account yake. Ndio maana huweka siku 3 za kazi kwa hundi za hapa nchini na siku 21 kwa hundi za nje....Isitoshe, kwa hundi za nje mteja hutozwa ada fulani kwa ajili ya gharama za mawasiliano na benki za huko nje n.k.
Ni jukumu la benki kujiridhisha kwanza kama hundi ni halali au la kabla hawajamlipa mteja...siku wanazotoa kwa amteja kusubiri zinatosha kabisa kuwasiliana na benki husika kama hundi hiyo ni halali na kama mlipaji ana kiasi cha kutosha kwenye account yake. Ikitokea kama hundi ina matatizo basi wanatakiwa kumrudishia mteja wao ili akapambane na huyo mdeni wake.
Kwenye hii issue ya Barclays lazima kuna uzembe fulani ulifanyika ndani ya benki yenyewe kwa kushindwa kufanya uhakiki unaotakiwa kabla ya kumwekea pesa huyo jamaa...