Baraza la Seneti lapitisha mpango wa dola trilioni 1.9

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,843
2,000
Baraza la Seneti la nchini Marekani limepigakura kuidhinisha mpango mkubwa wa msaada wa fedha wa trilioni 1.9 ambazo Rais Joe Biden amesema zitasaidia kuufufua uchumi.

Wajumbe wa chama cha Democratic katika Baraza la Seneti walifanikiwa kupiga kura na kuupitisha muswada wa mpango huo wa misaada ya fedha kwa ajili ya kuwasaidia wafanyakazi na wafanyabiashara walioathiriwa vibaya na janga la virusi vya corona.

Muswada huo uliidhinishwa kwa kuzingatia misingi ya vyama baada ya zoezi refu zaidi la upigaji kura katika historia ya siasa za nchini Marekani. Ilichukua muda wa saa 12 mpaka yalipopatikana maelewano miongoni mwa wanachama wa chama cha Democratic kwa ajili ya kumshawishi Seneta mwenye msimamo wa kihafidhina Joe Manchin, ambaye alikuwa anapinga kiwango cha fidia kinachopangwa kutolewa kwa watu wasio na ajira.

Muswada huo wa jumla ya dola trilioni 1.9 za misaada ya kifedha sasa utarudishwa kwenye Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kupitishwa na kuwa sheria. Baada ya hapo utaweza kusainiwa na Rais Joe Biden.

Rais Biden anataka mpango huo mkubwa wa fedha usaidie kuufufua uchumi wa nchi yake na kuwezesha kupatikana mamilioni ya nafasi za ajira mpya. Miongoni mwa mambo mengine, muswada huo utawawezesha Wamarekani wengi wanaolipa kodi kupatiwa moja kwa moja kiasi cha dola 1,400.

Muswada huo, maarufu miongoni mwa wapiga kura wa Marekani, umekuwa ni wa kipaumbele kwa utawala wa rais Joe Biden.

Watu milioni 9.5 walipoteza kazi mwaka uliopita wa 2020 wakati janga la maambukizi ya virusi vya corona lilipotokea. Ikulu ya Marekani imesema itachukua miaka kadhaa hadi kuisawazisha hali hiyo ya ukosefu wa ajira. Hata hivyo, takwimu za nwishoni mwa wiki zilionyesha kuwa nafasi mpya za ajira zipatazo 379,000 ziliongezeka mnamo mwezi Februari, kiwango hicho kizuri hakikutarajiwa na wachumi.

Baraza la Seneti liliupitisha muswada huo kura 50 za ndio huku kura 49 zikiwa zinaupinga. Wademocrat walipata ushindi huo finyu baada ya Seneta wa chama cha Republican wa jimbo la Alaska, Daniel Sullivan kutoshiriki kwenye kura hiyo kutokana na kulazimika kwenda kuhudhuria mazishi ya mwanafamilia, ikimaanisha kwamba Makamu wa Rais Kamala Harris hakulazimika kuingilia kati na kupiga kura yake ili kukipa ushindi chama chake. Baraza la Seneti lina wajumbe 50 wa chama cha Democtratic na chama cha Republican pia kina jumla ya wajumbe 50.

Rais Joe Biden amempongeza kiongozi wa Baraza la Seneti, Chuck Schumer na wajumbe wengine wa baraza hilo wa chama cha Democratic kwa hatua hiyo kubwa iliyofikiwa ambayo inafungua njia ya kuendelea mbele na ajenda za chama cha Democratic, lakini kiongozi wa chama cha Republican Mitch McConnell, kilicho na wajumbe wachache kwenye Baraza la Seneti hakuisherehekea hatua hiyo, amesema Baraza la Seneti halijawahi kutumia fedha nyingi namna hiyo na kwa mtazamo wake fedha hizo zitatumika kwa njia mbaya.
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
27,371
2,000
1.9t * 2300 = 4,370,000,000,000,000/- (4,370 Trillions)
Daaah ni mpunga mrefu sana *****
ebu tumia hii link upate jibu maana nimeweka figure zinanizingua. 1.9 t unaziandikaje kwa namba
 

famicho

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,006
2,000
ebu tumia hii link upate jibu maana nimeweka figure zinanizingua. 1.9 t unaziandikaje kwa namba
1.9x1,000,000,000,000= 1,900,000,000,000

Hizo juu ni dolari,

Kuileta kwa mkwanja wa jiwe zidisha kwa 2300 tsh

Unapata Shilingi tilioni 4,370/- za kitanzania.

Hebu tuilete kwa bajeti yetu ya tilion 40 kwa mwaka tujue tunaweza zitumbua kwa miaka mingapi ili tiharahei na wauza vitambulisho vya jiwe wale bata tu kwa hiyo miaka.

4370÷40 = 109.25 (miaka 109 na miezi 3 - kizazi cha sasa chote kitakwisha mpunga bado upo tu)

Ushauri tu, wale jamaa wala sio watu wa kubishana nao na wala kuwatunishia msuli,ikiwa sisi rambirambi tu tunakula
 

Emmanuel J. Buyamba

Verified Member
May 24, 2013
1,071
2,000
1.9x1,000,000,000,000= 1,900,000,000,000

Hizo juu ni dolari,

Kuileta kwa mkwanja wa jiwe zidisha kwa 2300 tsh

Unapata Shilingi tilioni 4,370/- za kitanzania.

Hebu tuilete kwa bajeti yetu ya tilion 40 kwa mwaka tujue tunaweza zitumbua kwa miaka mingapi ili tiharahei na wauza vitambulisho vya jiwe wale bata tu kwa hiyo miaka.

4370÷40 = 109.25 (miaka 109 na miezi 3 - kizazi cha sasa chote kitakwisha mpunga bado upo tu)

Ushauri tu, wale jamaa wala sio watu wa kubishana nao na wala kuwatunishia msuli,ikiwa sisi rambirambi tu tunakula
Duh!.
Hatari sana.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
14,133
2,000
1.9t * 2300 = 4,370,000,000,000,000/- (4,370 Trillions)
Daaah ni mpunga mrefu sana *****
Hebu iweke vizuri ili angalau na sisi wa F2B tupate picha Mkuu. Iko hivi, Tanzania ilipanga kutumia USD 15.14 billion (Tanzania plans to spend 15.14-bln-USD in 2020/2021 fiscal year - Xinhua | English.news.cn) kwenye bajeti yake ya 2020/2021.

Tukirudi kwenye fedha Senate ilizoidhnisha kusaidia athari za Corona, maana yake ni sawa na bajeti ya Tanzania kwa miaka: 1,900 bn./15.14 bn = 125.5 years! Huo ni msaada wa athari za Corona; sio bajeti ya Marekani. Swali; bajeti ya taifa la Marekani ni kiasi gani? Uchumi wa kati!
 

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
32,109
2,000
Viongozi wa nchi za wenzetu wanawajali raia wake, huku kwetu walisema tule nyasi ili rada sijui ndege ya rais inunuliwe.
 

Naby Keita

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
5,241
2,000
Hawawezi kufanya huo ujinga hata siku moja

Hela siku zote huwa iko benki
USD haiwi backed na kitu chochote tangible ili kuipa thamani ndo maana Mrusi na wenzie wanataka kuzifanya sarafu zao ziwe backed na dhahabu maana mfumo wa sasa ulivyo hizo pesa ni karatasi tu zilizopewa thamani na waliobadili mfumo wa kutoka sarafu kua backed na rasilimali fulani hadi kuja mfumo wa sasa ambao sarafu ni karatasi tu iliyopewa thamani fulani ni Marekani kwa ujanja janja wake
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom