Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, inatarajia kuunda baraza la mawaziri lenye wizara 14 ambazo zitagawanywa baina ya CCM na CUF kwa uwiano wa asilimia ya idadi wa wawakilishi katika Baraza la Wawakilishi.
Kwa mujibu wa taarifa tulizopata kutoka ndani ya serikali hiyo CCM itapewa wizara nane na CUF wizara sita.
Chanzo cha habari kimeeleza kuwa mchakato wa uundaji wa baraza hilo la mawaziri, umekamilika na kwamba rais Dk Ali Mohamed Shein, atalitangaza wakati wowote juma lijalo.
Muundo huo unatokana na Katiba ya Zanzibar inayotoa mwongozo kuwa serikali hiyo itaundwa kulingana na uwiano wa asilimia za uwakilishi ndani ya Baraza la Wawakilishi baina ya vyama hivyo viwili.
My take: Kipi kitakuwa chama kikuu cha upinzani au tunarudi miaka ileee yenye ukiritimba wa chama kimoja?
Hapo hamna upinzani tena! Nilitegemea serikali ya mseto iundwe na vyama ili kuwa na majority dhidi ya vyama vingine. Kama nchi ina vyama viwili tu vikagawana madaraka 6:4 basi hakuna upinzani tena, na ukiritimba unarudi kule kule. Nilichoona ni kama vile maalim alikuwa anahangaikia madaraka kuliko ile demokrasis halisi; sasa kayapata, basi hakuna kitu demokrasia tena mbele yake.
Huwezi kuziba tundu la ngalawa wakati safari ikiendelea na upepo ukisukuma wanachofanya CCM na CUF ni kama kupunguza maji ili mtumbwi usizame. Ninavyoona huko mbeleni kuna hatari ya tundu kuzidi.Naomba nitoe yangu mawili matatu hapa..
Binafsi sioni kosa la kuundwa kwa serikali ya aina hii. It is what we have, nadhani CCM ikiunda serikali ya peke yake itakuwa worse zaidi, hasa ukizingatia margin ndogo ya ushindi ulipata ( ambao ni suspected hata hivyo). Cha msingi tuone utendaji wa hii serikali na tutaanzia kuwahukumu na kuupima kuanzia hapo.
Naomba nitoe yangu mawili matatu hapa..
Binafsi sioni kosa la kuundwa kwa serikali ya aina hii. It is what we have, nadhani CCM ikiunda serikali ya peke yake itakuwa worse zaidi, hasa ukizingatia margin ndogo ya ushindi ulipata ( ambao ni suspected hata hivyo). Cha msingi tuone utendaji wa hii serikali na tutaanzia kuwahukumu na kuupima kuanzia hapo.
Unajua there is a need to talk again on this matter of union. Where are they getting money to accommodate 14 ministry while the population is just 1.6 million people? it is crazy!
Huwezi kuziba tundu la ngalawa wakati safari ikiendelea na upepo ukisukuma wanachofanya CCM na CUF ni kama kupunguza maji ili mtumbwi usizame. Ninavyoona huko mbeleni kuna hatari ya tundu kuzidi.