Baraza la mawaziri Zanzibar CCM 8 CUF 6

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
301
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, inatarajia kuunda baraza la mawaziri lenye wizara 14 ambazo zitagawanywa baina ya CCM na CUF kwa uwiano wa asilimia ya idadi wa wawakilishi katika Baraza la Wawakilishi.

Kwa mujibu wa taarifa tulizopata kutoka ndani ya serikali hiyo CCM itapewa wizara nane na CUF wizara sita.

Chanzo cha habari kimeeleza kuwa mchakato wa uundaji wa baraza hilo la mawaziri, umekamilika na kwamba rais Dk Ali Mohamed Shein, atalitangaza wakati wowote juma lijalo.

Muundo huo unatokana na Katiba ya Zanzibar inayotoa mwongozo kuwa serikali hiyo itaundwa kulingana na uwiano wa asilimia za uwakilishi ndani ya Baraza la Wawakilishi baina ya vyama hivyo viwili.

My take: Kipi kitakuwa chama kikuu cha upinzani au tunarudi miaka ileee yenye ukiritimba wa chama kimoja?
 
wizara kumi na nne

mbona nyingi hivi kwa nn wasingeunda kumi tu CCM nafasi sita na CUF nne ?

au logic gani wametumia hawa wenzetu ?

hebu tukae mkao wa kusubiri tuone
 
Hizi Znz wako watu wangapi ?

Inabdi kujiuliza kwa kweli inaweza kuwa gharama ya kuendeshaji kubwa kuliko huduma kwa jamii!

Sidhani kama idadi ya znz inazidi ya watu Dar.Income yao kiasi gani?
 
Mnachosahau ZNZ ni NCHI ndani ya muungano si mkoa ati! Hivyo si vema kuilinganisha na mmojawapo ya mikoa ya bara. Nyie kama mliiua 'tanganyika' hilo si suala letu. Tuacheni na nchi yetu!
 
Eti nchi yetu ya zanzibar,nchi gani hiyo wilaya tu,mnabebwa na siasa za kinafiki tu
 
Zanzibar and Pemba have a population of approx. 1.1 million as of July this year. It is a country formed within a country, with a president under a president. This country (Zanzibar & Pemba) has no opposition in its House of representatives. Its government is formed by a coalition of two strongest political parties (CCM and CUF).
 
Hapo hamna upinzani tena! Nilitegemea serikali ya mseto iundwe na vyama ili kuwa na majority dhidi ya vyama vingine. Kama nchi ina vyama viwili tu vikagawana madaraka 6:4 basi hakuna upinzani tena, na ukiritimba unarudi kule kule. Nilichoona ni kama vile maalim alikuwa anahangaikia madaraka kuliko ile demokrasis halisi; sasa kayapata, basi hakuna kitu demokrasia tena mbele yake.
 
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, inatarajia kuunda baraza la mawaziri lenye wizara 14 ambazo zitagawanywa baina ya CCM na CUF kwa uwiano wa asilimia ya idadi wa wawakilishi katika Baraza la Wawakilishi.

Kwa mujibu wa taarifa tulizopata kutoka ndani ya serikali hiyo CCM itapewa wizara nane na CUF wizara sita.

Chanzo cha habari kimeeleza kuwa mchakato wa uundaji wa baraza hilo la mawaziri, umekamilika na kwamba rais Dk Ali Mohamed Shein, atalitangaza wakati wowote juma lijalo.

Muundo huo unatokana na Katiba ya Zanzibar inayotoa mwongozo kuwa serikali hiyo itaundwa kulingana na uwiano wa asilimia za uwakilishi ndani ya Baraza la Wawakilishi baina ya vyama hivyo viwili.

My take: Kipi kitakuwa chama kikuu cha upinzani au tunarudi miaka ileee yenye ukiritimba wa chama kimoja?

Upinzani uko wapi? Nani atakayeikosoa serikali? CUF byeeeee!!!!
 
Hapo hamna upinzani tena! Nilitegemea serikali ya mseto iundwe na vyama ili kuwa na majority dhidi ya vyama vingine. Kama nchi ina vyama viwili tu vikagawana madaraka 6:4 basi hakuna upinzani tena, na ukiritimba unarudi kule kule. Nilichoona ni kama vile maalim alikuwa anahangaikia madaraka kuliko ile demokrasis halisi; sasa kayapata, basi hakuna kitu demokrasia tena mbele yake.

Naomba nitoe yangu mawili matatu hapa..

Binafsi sioni kosa la kuundwa kwa serikali ya aina hii. It is what we have, nadhani CCM ikiunda serikali ya peke yake itakuwa worse zaidi, hasa ukizingatia margin ndogo ya ushindi ulipata ( ambao ni suspected hata hivyo). Cha msingi tuone utendaji wa hii serikali na tutaanzia kuwahukumu na kuupima kuanzia hapo.
 
Unajua there is a need to talk again on this matter of union. Where are they getting money to accommodate 14 ministry while the population is just 1.6 million people? it is crazy!
 
Huwezi kuziba tundu la ngalawa wakati safari ikiendelea na upepo ukisukuma wanachofanya CCM na CUF ni kama kupunguza maji ili mtumbwi usizame. Ninavyoona huko mbeleni kuna hatari ya tundu kuzidi.
 
Hata mimi sioni kosa au tatizo lolote. CHADEMA wagekuwa na guts za kuendesha libeneke za vurugu baada ya uchaguzi kwa wiki mbili hivi, JK angeshinikizwa kuanzisha serikali ya mseto na Slaa angetafutiwa cheo kama ilivyotokea Kenya. Hiyo ni demokrasi ya nchi za kiAfrika.

Anyway punditry ya nani spika imekwisha ngoja watu waanze na tetesi za nani atakuwa waziri mkuu.
 
Msishangae kusikia Lipumba akiwa mbunge wa kuteuliwa na rais BJMT(Bunge la Jamhuri ya Muungano Tz) Washachakachuliwa hao
 
Unajua there is a need to talk again on this matter of union. Where are they getting money to accommodate 14 ministry while the population is just 1.6 million people? it is crazy!

Get life. 14 ministries ni wizara chache.
 
Huwezi kuziba tundu la ngalawa wakati safari ikiendelea na upepo ukisukuma wanachofanya CCM na CUF ni kama kupunguza maji ili mtumbwi usizame. Ninavyoona huko mbeleni kuna hatari ya tundu kuzidi.

Toa maoni yako..wewe ulitakaje?
 
Wizara 9 zingeliwatosha wazanzibari. CCM 5 na CUF 4. na hapohapo jamaa atateua manaibu waziri wanini?? Kodi ya wananchi ni vyema ikahudumia wananchi wenyewe na sio kunufaisha wachache.
 
Back
Top Bottom