Baraza la mawaziri la mseto ni dawa au mbinu za kisiasa?

Hivi watu wa bara hamuoni upinzani ulivyozorota Zenji baada ya kuwa na serikali ya mseto? Mfano mnao na madhara mmeyaona lakini bado kuna watu wanaimani na serikali ya mseto. kazi kwelikweli.
 
Kweli kabisa, wabunge walioteuliwa toka vyama vya upinzani watakuwa wanatekeleza ilani ya CCM katika baraza jipya la mawaziri. Hii itazidi kuipa nguvu CCM na kuzorotesha upinzani. Chadema wasikubali kabisa kuingia kichwakichwa kama NCCR
 
Mseto kwa sasa haufai kwa tanzania yetu maana kinachotusumbua ni mfumo dhaifi wa ccm na serikali yake, kwa sasa tunataka serikali dhaifu ya ccm iondoke na mfumo wao mbovu ufutiliwe mbali hiyo ndio dawa pekee.
 
...labda Mkuu lakini nakumbuka juzi kusoma katika gazeti moja kwamba ujenzi wa barabara nyingi umesimama kwa Serikali kutokuwa na pesa na pia kutaka kuyalipa kwanza madeni ya nyuma ambayo ni zaidi ya shilingi 600 billioni kabla ya kuendelea na awamu nyingine za ujenzi.

Mara kadhaa magezeti yetu yamekuwa yanaandika kitu ambacho hakijafanyiwa upembuzi wa kutosha. Barabara nisemayo ya kutoka Dar kwenda Zambia, ni kipindi cha pasaka nimepita na kushihudia kazi ikifanyika. Yawezekana baadhi, lakini nyingine zinaendelea kujengwa.
 
Mkuu nakuelewa sana, ila wewe unaangalia kwa upande wa Rais, mimi naangalia upande wa CHAMA

Machelea kukubali approach yako kwani inamuangalia rais kama rais lakini upande wa pili unataka tena niangalie individuals.... labda kama tuko kibinafsi zaidi

Lakini kwa mtazamo wangu, we have to look at vyama kwani ndio challenge tuliyo nayo leo, tumefika kwenye janga hili kutokana na CCM kuendesha serikali kichama zaidi, hadi kikao cha juzi uliona jinsi walivyojaribu kuhamisha hoja iwe ni ya kichama zaidi, wameshabeza sana maamuzi ya maana ya wabunge wa chadema, walibeza kutoka nje wakati ule wa kuunda cabinet ya kipinzani, wakabeza wakati wa mchakato wa katiba nk. kujoin hapo bila kuwa na party reteat sio sahihi ... na hii si kwa vyama vya siasa, la hasha, sio sahihi kwa watanzania maskini (sio mimi na wewe kwani sisi tunaweza kujisemea) wasio na mtetezi

Si kitu kigeni, jambo kama hilo limeshatokea nchini Marekani, Obama baadhi ya candidates wa uwaziri kutoka chama cha upinzani, mmoja alikataa kwa hoja kwamba kuwepo ndani ya baraza la Obama ni kudhoofisha nguvu ya Republican, na anahofia kiti chake cha ubunge baada ya kuwa wazi kisijechukuliwa na Demokratic.
 
Strategically it will be a wrong move especially kama atachagua from CDM,Itakua wrong move kwa Opposition side.Why?

1.Chama cha upinzani kitakachotoa waziri hakitaepuka kuitwa CCM B,C,D na kadhalika.Baraza hili halitakua na jipya katika utendaji kwa sababu tatizo ni system,hivyo chama kitakachotoa waziri kutoka upinzani kitakua kimejiharibia mwisho wa siku.

2.Serikali inatekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi.Waziri kutoka NCCR atatekeleza ilani gani? Hilo haliwezekani.

Una hoja nzuri, maana yatokeayo Tanzania visiwani ni funzo tosha, maana CUF kisiwani imeshakufa, nilishangaa uchaguzi mdogo wa ubunge karibuni Chadema wakashika nafasi ya pili na CUF kuambulia nafasi ya tatu, jambo ambalo visiwani kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka juzi ilikuwa ndogo kutokea.
 
Hapo ndipo kikwete anarudi sasa nakuwasoma watu wake waliomwamin na kumpa uongozi.Its all about moving foward.Put right people to work! no matter they r white or blue. Afu ubaguzi unaniuzi!!! hasa huu wakivyama.GUYS WE ARE ALL TANZANIA.
 
Asiguse CDM awatumie cuf na nccr

kamanda mbona unataka kuwafanya hawa CDM kama watakatifu/saints sasa? hawa si wanasiasa tu kama wengine na wanataka kuonekana na kujulikana kitaifa ili wapate nguvu nyingi kisiasa (ofkoz na kiuchumi), sasa wewe kama nani unawakatalia mbunge wa CDM mfano Lissu, Mnyika, Zitto, kua waziri katika serikali ya CCM au unafikiri watakataa? mtu wa kukataa uwaziri CDM ni mbowe peke yake, wengine wote walio wabunge watakimbilia uwaziri na kujifanya wanaweka taifa kwanza kuwatumikia wananchi katika serikali iliyochaguliwa na wananchi..

acha ushabiki wa upofu
 
Kweli kabisa, wabunge walioteuliwa toka vyama vya upinzani watakuwa wanatekeleza ilani ya CCM katika baraza jipya la mawaziri. Hii itazidi kuipa nguvu CCM na kuzorotesha upinzani. Chadema wasikubali kabisa kuingia kichwakichwa kama NCCR

Huwezi jua, huenda Chadema wamemtolea nje Kikwete, ndo maana ameamua kugeukia upande wa NCCR Mageuzi kupoza machungu.
 
NI DAWA.Hatuwezi tukawaacha watu wazuri (tunavyosikia) kama huyo Janet, Mbatia, na Lipumba. Ila sidhani kama atachukua wengi, atajaribisha mmoja.Ila ni faida kuweka zadi ya mmoja, inaweza kuanza kuleta revolution ya kiuchumi
 
NI DAWA.Hatuwezi tukawaacha watu wazuri (tunavyosikia) kama huyo Janet, Mbatia, na Lipumba. Ila sidhani kama atachukua wengi, atajaribisha mmoja.Ila ni faida kuweka zadi ya mmoja, inaweza kuanza kuleta revolution ya kiuchumi

Kuweka mmoja tu haitakuwa na nguvu. Walao angetenga wizara kama tatu au nne hivi, hao wangejenga nao mtandao wa kujamini na kuwa mfano mzuri wa utendaji utakaokuwa chache kwa wizara nyingie, papo ni mwanzo mzuri wa kuleta utaifa zaidi, ingawa wenye itikadi kali za kisiasa wanasema ni kuua upinzani.
 
Nakubaliana na hoja zako, lakini kumbuka suala la uwaziri ni mtu binafsi na wala si chama. Hata kama chama wangekubali kuwa mbali na nafasi hizo, mtu binafsi mradi ni mbunge anaweza kukubali kuwa waziri kadiri ya dhamiri yake.

This is not proper. Huwezi kusimama peke yako bila kusimamia kwenye miguu ya chama chako. Na ukumbuke kuwa ubunge ulipatikana kupitia chama na sio mgombea binafsi.
 
This is not proper. Huwezi kusimama peke yako bila kusimamia kwenye miguu ya chama chako. Na ukumbuke kuwa ubunge ulipatikana kupitia chama na sio mgombea binafsi.

Kugombea ubunge ni ridhaa ya mtu binafsi, chama ni njia tu ambayo katika utoaji maamuzi bungeni hafungwi ila anaangalia utaifa zaidi. Wanaomchagua mbunge wanachama wake ni wachache zaidi kuliko wananchi wengi wasio wanachama. Hivyo kuingia baraza la mawaziri si kwa masilahi ya chama bali taifa. Kinachoaangaliwa utendaji na uajidifu wa utendaji wa mtu si itikadi za kichama.
 
Anaweza kugusa/kutumia chama chochote kwa maslahi ya kulijenga Taifa hili bila ulafi wa madaraka.

Acha kujidanganya kijana kwani nani hawajui CCM?kama anataka kuonyesha uzarendo kwa watanzania aachie ngazi,si lazima amalize kipindi chote.
 
Kuwachagua wapinzani itaisaidia sana CCM maana dawa yake unampa Zitto Kabwe uwaziri wa fedha halafu unampa task ya kuhakikisha kila wizara inapata mahitajio yake on time na makusanyo ya kodi yanakuwa ya kuridhisha.

On top, ahakikishe bajeti inakuwa inategemea makusanyo ya ndani kwa 90% halafu unamuangalia anavyohangaika, mwisho wa siku ananyoosha mikono anasema "POO".
 
kama itatokea Mheshimiwa Rais Dr. Jakaya Kikwete kuteua baraza la mawaziri la mseto itakuwa sio kwa ajili ya kujitafutia umaarufu baada ya kumaliza muda wake wa utawala. Bali kushirikisha watu wanaoonekana kuwa na mawazo mazuri na haiba njema, uadilifu na kuaminika kutokana na kigezo wapo nje ya system.

Maana baadhi ya watu tunawakubali kwa maneno yao ya matumaini na hasa pale wanapokuwa wa kwanza kutupatia njia mbadala ya kumaliza matatizo yetu kupitia benchmark ya utendaji wa serikali iliyopo madarakani. Ni vema wakapewa nafasi ili tuone na tulinganishe maneno na matendo.

Ikitokea hivyo haitakuwa kwa manufaa binafsi ya rais bali kwa taifa zima lililomwamini.
 
Back
Top Bottom