Baraza la mawaziri la mseto ni dawa au mbinu za kisiasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Baraza la mawaziri la mseto ni dawa au mbinu za kisiasa?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, May 4, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Dalili ya mvua ni mawingu, hata isiponyesha leo kuna mategemea kuwa mvua yaja. Rais Kikwete kuteua wabunge wapya kipindi hiki kabla hajasuka baraza la mawaziri, mmoja akiwa kutoka chama cha upinzani, ni dalili ya kunukia kuwa na baraza la mawaziri mseto kutoka vyama kadhaa vya kisiasa nchini.

  Kuna mambo kandaa ambayo yanaweza kumsukuma Kikwete kuchukua hatua hiyo, machache ya mambo hayo ni kama ifuatavyo.

  1. Kujulikana kwake kimataifa anataka kujijengea jina zuri kabla ya muda wake kumalizika duniani.
  2. Anamwiga Obama ambaye ana baraza la mawaziri mseto kutoak Democratic na Republican.
  3. Kuingiza dawa mpya kutoka upinzani ili kubutua mtandao wa wanaCCM walafi.
  4. Amekata tamaa kwa kutegemea wa kutoka CCM tu, kwani wanamwangusha kiutendaji
  5. Anatengeneza mazingira mazuri atakapomaliza muda wake akubalike kama Biblia isemavyo juu ya Karani mbaya.
  6. Wengi ndani ya CCM wana kashfa ya ulafi.

  Kunaweza kuwa na tafsiri nyingi, lakini uamuzi huo ni uamuzi mgumu ambao kwa mtazamo wa harakaharaka WanaCCM wenzake wanaweza kufikiria amesaliti chama, lakini Kikwete ameangalia zaidi utaifa, na kujenga nchi yanye kujiamini, kwani kutegemea CCM pekee mambo yanazidi kuharibika, na nchi haitawaliki.
   
 2. M

  Mbinga Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Katiba haimruhusu JK kuwa na baraza mseto!
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Katiba inaruhusu kwa vile Rais yuko huru kuchagua mawaziri kutokana na wabunge, na haijaainishwa kwamba mawaziri watokane na chama chenye kushinda uchaguzi mkuu.
   
 4. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Asiguse CDM awatumie cuf na nccr
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hakuna uhasama katika suala ya utumishi kwa umma, mradi Rais akipima kwamba baadhi ya wabunge wa Chadema anaweza kuwaaminisha majukumu ya kumsaidia katika utawala ni jambo jema. Tuweni wastaarabu jamani, nch hii ni moja na sote ni watanzania, na tunawapongeza ambao wako tayari kututumikia kwa moyo na roho njema kwa manufaa ya nchi yetu.
   
 6. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  CHD ikikubali wabunge wake wawe mawaziri kwenye hii serikali ya CCM, JK atakuwa ameua upinzani kisayansi
   
 7. b

  busara ya mzee Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sababu moja umeacha kwa makusudi,nayo ni njia moja wapo ya kuivuruga chama cha chadema,ukweli usiopingika nguvu ya chadema itongezeka wabunge wake wasipoteuliwa kuwa mawaziri,chadema msikubali hilo,mbunge atakae kubali na atoswe
   
 8. b

  busara ya mzee Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: Apr 25, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na hasa chadema mikakati yote ya serikali ya mseto ni kuimaliza chadema
   
 9. m

  mahoza JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 1,242
  Likes Received: 411
  Trophy Points: 180
  Lakini jamani kwani wanavhama wa ccm wameisha hadi ageukie upinzani? Ni kuwa wanaccm hawana imani naye tena ndio maana anajikomba kwahao wanafiki Mbatia.
   
 10. no9

  no9 Senior Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: Nov 11, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  wataoteliwa wanawajibika serikalini watumishi wa umma si chama.natumaini atatutoa point a kwenda b
   
 11. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  CHADEMA kukubali kuingia seriakli hii ni suicidal

  Itakua ni kuunga mkono utendaji, na madhara yake makubwa ni neutralization ya M4C
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tusiangalie upande mmoja tu wa shilingi, kuna mambo mengi ambayo yanaweza kumsukuma Kikwete kuwa baraza la mawaziri la mseto. Tukiangalia upande mmoja tu tutakuwa tumefikira kiwango cha kiubaguzi na ubinafsi zaidi.
   
 13. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Yote yawezekana, kudhoofisha upinzani au kuimarisha uwajibikaji serikalini. Ujue Kikwete huenda anakuwa peke yake, hakuna wa kumwunga mkono kwa vile wenzake wanaangalia zaidi masilahi binafsi na chama chao na kuweka kiporo mambo ya manufaa kitaifa.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  May 4, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,878
  Likes Received: 83,359
  Trophy Points: 280
  ...Nakubaliana nawe kabisa. Kama kutakuwa na baraza la mawaziri la mseto basi CDM wakae nalo mbali sana na waelekeze nguvu katika kujiimarisha zaidi katika kila kona ya Tanzania tayari kuchukua nchi 2015. Alama za nyakati zinaonyesha kwamba anguko kubwa la magamba haliko mbali hivyo hakuna sababu yoyote ya CDM kuwapa uhai magamba.

   
 15. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  huwezi kuongeza uwajibikaji serikali kwa kuweka two or three ministers from chadema mkuu

  wewe unaona hata wilaya zenye wabunge wa upinazni ziko suffocated....

  think outside the box...... the move would be suicidal to chadema, it is a wrong move to accept kuwepo kenye cabinet

  Remember all along chadema has been fighting for an accountable government, accountability hailetwi na 2-3 people being in a corrupt government

  if there is any smart tanzanian thinking it is ok for chadema to join serikali, basi ujue huyo hajui kabisa maana ya kinachotokea

  kuhusu jk kuwa peke, hiyo ndio red alert number one.......... dont join a lonely president, cause it is a confirmation that it is a failed state
   
 16. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2012
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Anaweza kugusa/kutumia chama chochote kwa maslahi ya kulijenga Taifa hili bila ulafi wa madaraka.
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  May 4, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,878
  Likes Received: 83,359
  Trophy Points: 280
  ...CDM sioni mtu wa kuukubali uwaziri toka kwa Kikwete isipokuwa yule mganga njaa Shibuda....
   
 18. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na hoja zako, lakini kumbuka suala la uwaziri ni mtu binafsi na wala si chama. Hata kama chama wangekubali kuwa mbali na nafasi hizo, mtu binafsi mradi ni mbunge anaweza kukubali kuwa waziri kadiri ya dhamiri yake.
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  May 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Unaonaje wizara kama tatu hivi wangepewa wapinzania waonyesha utendaji, ingawa kule Tanzania visiwani hatujui tofauti ya utendaji serikalini kati ya wanaotoka CCM na wanaotoka CUF.
   
 20. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  where is the collective responsibility and party caucus???

  Come on CS.... you are better than that; unless uniambie kwamba we dont have strong will to drive what we believe for at least a few months.... kumbuka kuna kigeukegu cha chama misemo soon, na hapa ndipo party morals kama chadomo watakubali watu wao waamue bila chama na hasa kamati kuu kukubaliana!!!:A S 109:

  I think my signature tells it like it is
   
Loading...