Baraza jipya: VIJANA Wasichaguliwe Uwaziri

u mean MAIGE amelaanika?atalaanika au analaanika?coz ameuza twiga na amenunua X 6 bmw
Mungi na Maige ni watu wawili tofauti hata kulaanika kwao kutakuwa tofauti.

Mkuu unaamini kwamba Waziri wa Maliasili na Utalii peke yake anaweza kuuza hata fisi achilia mbali twiga na akaruhusu ndege tena ya kijeshi ikatua na kuchukua fisi wetu?
 
Hii nakubali kabisa; ndio maana mimi si muumini kabisa wa "ujana" ni sawa sawa na "uongozi bora". Mifano iko mbele yetu na tukipuuzia tunapoteza haki ya kulalamika. Waachwe vijana wawe wabunge na taratibu waanze kujengwa; waendesha mashirika au makampuni yao n.k.. wapewe watu wenye uzoefu wa kuendesha biashara au shughuli zao kwa umakini na weledi..

Mkuu nadhani watu tu wanakosa maadili na uchungu kwa taifa lao.

Mbona kipindi cha Mwalimu Nyerere aliteuwa vijana wakati ule kina Salim Ahmed Salim.

Kuna wazee wengi mbona wizi wa mali za umma kama Andrew Chenge, Benjamin Mkapa, Kingunge Ngombale Mwilu. Daudi Balali, Nimrod Mkono.
 
Mkuu kweli wewe si muumini wa vijana lakini ukumbuke Nyerere aliukwaa Urais akiwa kijana wa miaka 37 hivi. Na wengi tunakiri kwamba alijitahidi katika uongozi wake na hakuwa mwizi. Wizi na ufisadi ni ni mmomonyoko wa maadili kwenye jamii yetu. Hivi Mkulo ni kijana yule? Mfutakamba je? Nundu? Mponda?

Tanzania bado tuna vijana wazuri tu na waadilifu watafutwe wawe vetted wapewe nafasi. Tatizo hapa katikati ilikuwa ni ukosefu wa vetting na kujua historia na uadilifu wa watu. Wengi walikuwa wakichukuliwa kwa kuwa kuna kauhusiano fulani ka mtaani ama mtandaoni. Nadhani sasa tutarudi kule kwa zamani ambapo wateule walikuwa hawapewi bali wanastahili kuteuliwa.

Unafikiri ni kwa sababu alikuwa "kijana" ndio maana alipata nafasi hizo na kukubaliwa na wazee? au alikuwa kijana pekee ambaye amesoma?
 
Mkuu hapa sikubaliani na wewe,tatizo sio vijana wako vijana wengi na wenye uwezo hapa ni system iliopo katika kuchagua vijana hawa kuna mambo na vigezo ambavyo vinazingatiwa kwa chama tawala CCM.Kwanza ni wale watakalinda masilahi ya mafisadi,watakaotii na kupokea amrikutoka juu,wasio na uwezo wa kufikiri na kutoa mawazo yao,SISI TUNAKULA NAWE KULA KWA NAFASI YAKO USIHOJI USIULIZE SISI WOTE MAFISADI!Kwa utaratibu huukwa chamatawala kutegemea uwajibikaji ni ndoto.Hata huo uwajibikaji tuishukuru CHADEMA.MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Unaona umesema "vijana wenye uwezo" well kuna tatizo gani basi kwa "wazee wenye uwezo"?
 
Mkuu mwanakijiji,

Why umekuwa mwepesi kutoa jibu ambalo ulishawahi kuliandikia makala?

Wapee wazee?

Gembe, kwa sababu naweza kuona toka mbali kuwa tunaweza kujikuta tunapelekwa vitani kupigana kwa sababu "kijana" kaamua tukapigane! bila kuelezwa vizuri na kutumia hekima ya kwanini vita ni chaguo la mwisho! Kuna hatari itaiangukia tanzania kwa sababu tunataka kusahaulishwa kuwa viongozi ambao leo tunawaona ni wazee karibu wote waliingia katika utumishi wakiwa ni vijana!!!!
 
hao wenye uzoefu ambao the so called WAZEE HAWAIBI?HAWANA KASHFA?
-mungai,
-mramba
-yona
-iddi simba
-ntagazwa
-

You are missing the point; binafsi sitaki kabisa kuangalia umri. Nataka kuangalia uwezo, uadilifu, umakini, busara, uthubutu n.k qualities ambazo hazijali jinsia, kabila, rangi, umri au hata chama!
 
...kizazi kinachoabudu utajiri na kuacha utu.Kuwaza mafanikio kwa njia za mkato, tamaa, kuiga yasio ya msingi, vibinti, uzembe uliopindukia vinaliangamiza taifa letu.Vijana wengi wametumbukia humo.
 
Sidhani kama umri wa mtu una uhusiano wa karibu sana na tabia za kifisadi, bali nadhani hiyo ni tabia mtu tu. Nyerere alianza kuongoza akiwa na umri mdogo sana na alikuwa na influence ya kufanya jambo lolote lile ambalo angetaka lakini hakutumia nafasi ile kifisadi.

Iwapo mtu alichaguliwa ubunge kwa kuhonga, tusitegemee kuwa atakapokuwa waziri hatalipiza kisasi kwa kupokea hongo pia. Katika vigezo vya kumteua mtu kushika madaraka serikalini kama waziri, ingekuwa ni vizuri sana kuangalia namna alivyoendesha kampeini zake na namna alivyoshinda uchaguzi. Mtu yeyote aliyeshinda uchaguzi kwa mbinde mbinde za namna yoyote, ikiwemo ushindi wa technicality, hafai kuwa Waziri.
 
Wakuu hapa hakuna cha kijana wala mzee wote ni wezi tu. Na hii ni tabia ya mtu binafsi. Mtu asipokuwa na hofu ya MUNGU hawezi kuwa mwadilifu awe kijana au mzee. Mifano imetolewa mingi tu hapa ya wazee mawaziri walio wezi wa kupindukia. Hata humu maofisini wako vijana wacha MUNGU wanachapakazi zao kwa uaminifu mkubwa lakini wana vita kali kutoka kwa wafanyakazi wenzao kwasababu wanawazibia ulaji (wizi). Watu tunapewa pesa za masurufu kwenda mikoani kikazi tukirudi tunarudisha pesa zilizobaki watu wanatucheka na kutuona wa ajabu. Kwahiyo wizi umejaa mioyoni mwa watu kuanzia ngazi za chini hadi juu.
 
Hii nakubali kabisa; ndio maana mimi si muumini kabisa wa "ujana" ni sawa sawa na "uongozi bora". Mifano iko mbele yetu na tukipuuzia tunapoteza haki ya kulalamika. Waachwe vijana wawe wabunge na taratibu waanze kujengwa; waendesha mashirika au makampuni yao n.k.. wapewe watu wenye uzoefu wa kuendesha biashara au shughuli zao kwa umakini na weledi..

ah okay...wazee ndio sio wezi na ndio wachapa kazi sio(lowasa,mkapa,kikwete,kingunge,malecela) mhh:nono:
 
You are missing the point; binafsi sitaki kabisa kuangalia umri. Nataka kuangalia uwezo, uadilifu, umakini, busara, uthubutu n.k qualities ambazo hazijali jinsia, kabila, rangi, umri au hata chama!

Mkuu kama hutaki kuangalia umri ni sawa. Kwa maana hiyo wewe kwako na kwangu vijana na wazee wana nafasi sawa. Wote wanaweza kuwa wazuri ama mafisadi. Hapa issue ni uadilifu wa mtu. Kuna vijana wazuri ambao bado wamo humu nchini na wakipewa nafasi watafanya kazi. Wapewe kazi kwa kufuata utendaji na uthubutu siyo kwa kujuana vijiweni ama mtandaoni.
 
Mkuu mharakati umenena vyema. Kitu hiki kinachoitwa security of tenure kinatuharibia nchi. Ukipewa madaraka makubwa hasa ya kitaasisi ya kusimamia serikali na kuendelea kuwepo pale kukategemea tamko la mtu mmoja tu basi unakosa hata maamuzi na ni rahisi kuingiliwa. Mkurugenzi wa PCCB hana security of tenure uwepo wake unategemea tamko la mkuu wa nchi. CAG yeye ana kauhakika kidogo kwani mkuu wa nchi hawezi kuamka na kumfuta kazi hadi mchakato fulani wa kikatiba ufuatwe. Hivyo CAG ameweza kutoa taarifa ile kwa kuwa ana kauhakika ka ajira yake. Pia anaacha legacy ya kiti hicho. Baada ya watu kumshutumu kwa ile ukaguzi wa Jairo ameamua kujitakasa. Lakini pia nadhani kwa hilo la CAG kuna political will from the top we call it tone at the top.

exactly security of tenure..inabidi tuwe makini kwenye katiba mpya tuweke mkazo katika kuzipa nguvu hizi taasisi muhimu za kitaifa ziwabane hawa wanasiasa..maana yake sheria mpya bila ya nguvu ya kuzitekeleza ni hamna kitu
 
Tatizo sio vijana ila ni aina ya vijana wanaopewa uongozi hata hao vijana wanaopigiwa debe na magazeti wengi wao hamna kitu
vile vyombo kama usalama wa Taifa hatujui vinafanya kazi gani na hii yote imesababishwa na viongozi waliokuja baada ya mwalimi kutoa vyeo kama zawadi ndio tukaona watoto wa mwinyi,malima,makamba,Nauye ambao wamefanya kama uongozi wa nchi ni wa kurithishana
lakini kama tunakuwa na system nzuri ya kuchagua viongozi haijarishi kama tuna kiongozi mzee au kijana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom