Baraza jipya: VIJANA Wasichaguliwe Uwaziri

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,396
7,968
Uzoefu wa toka JK ameingia madarakani vijana waliobahatika kupewa uwaziri wamegeuka kuwa genge la majizi na wahujumu uchumi. Lau Masha, Wiliam Ngeleja, Ezekiel Maige, Cyril Chami, Adam Malima, na wengine wametufanya tuamini kuwa vijana wa sasa hawajalelewa katika maadili mema ya uadilifu. Wanaiba wake za watu, wanatembea na wanafunzi, walevi kupindukia huku wizara zao zinaongoza kwa utendaji mbovu na hakuna ufanisi. Mfano wizara ya Ngeleja mgao wa umeme toka ameingia madarakani.

Mimi mtazamo wangu vijana wasipewe uwaziri, wachache wapate unaibu ili tuwachunguze kama wanaweza kuongoza na hawana tamaa. Mimi pia ni kijana lakini naona dhahiri vijana waliopo katika wabunge wa CCM hakuna msaada, wote ni majizi yanayotafuta vijiwe vya kufanyia uhalifu.

Nawakilisha...
 
Hii nakubali kabisa; ndio maana mimi si muumini kabisa wa "ujana" ni sawa sawa na "uongozi bora". Mifano iko mbele yetu na tukipuuzia tunapoteza haki ya kulalamika. Waachwe vijana wawe wabunge na taratibu waanze kujengwa; waendesha mashirika au makampuni yao n.k.. wapewe watu wenye uzoefu wa kuendesha biashara au shughuli zao kwa umakini na weledi..
 
nashauri watakaoteuliwa kwenye baraza wawe waadilifu,sioni umuhimu wa umri hapa.kuna utafiti wowote tuliofanya na kujua kati ya vijana na wazee nani anaongoza kwa uzembe na ufisadi?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Hii nakubali kabisa; ndio maana mimi si muumini kabisa wa "ujana" ni sawa sawa na "uongozi bora". Mifano iko mbele yetu na tukipuuzia tunapoteza haki ya kulalamika. Waachwe vijana wawe wabunge na taratibu waanze kujengwa; waendesha mashirika au makampuni yao n.k.. wapewe watu wenye uzoefu wa kuendesha biashara au shughuli zao kwa umakini na weledi..
Mkuu kweli wewe si muumini wa vijana lakini ukumbuke Nyerere aliukwaa Urais akiwa kijana wa miaka 37 hivi. Na wengi tunakiri kwamba alijitahidi katika uongozi wake na hakuwa mwizi. Wizi na ufisadi ni ni mmomonyoko wa maadili kwenye jamii yetu. Hivi Mkulo ni kijana yule? Mfutakamba je? Nundu? Mponda?

Tanzania bado tuna vijana wazuri tu na waadilifu watafutwe wawe vetted wapewe nafasi. Tatizo hapa katikati ilikuwa ni ukosefu wa vetting na kujua historia na uadilifu wa watu. Wengi walikuwa wakichukuliwa kwa kuwa kuna kauhusiano fulani ka mtaani ama mtandaoni. Nadhani sasa tutarudi kule kwa zamani ambapo wateule walikuwa hawapewi bali wanastahili kuteuliwa.
 
utendaji wa mawaziri unaongozwa na kanuni au umri?

Kweli kabisa mkuu MMKJ...

Sisi vijana kizazi cha sasa tumesoma wakati nchi iko mikononi mwa manyang'au, hasa between 1995 and 2012. Nakumbuka tulipomaliza vyuo kila mtu alikuwa anaongelea sehemu zenye urahisi wa kupata rushwa kama nzuri kuanzia kazi, eti unatajirika haraka the likes of TRA, Tanroads nk.

Ukiwapa nchi vijana kama hawa ndo tunakutana na ya akina Ngeleja. Coaching and Mentoring ya vijana wa kizazi cha sasa ni muhimu. Hii nchi iko nyuma sana kimaendeleo tunahitaji ku sacrifice baadhi ya mambo kwa ajili ya nchi yetu
 
Kusema za kweli vijana wa Tanzania kuna tatizo kubwa sana!
Katika mazingira ya kila kitu kutaka usasa na uzungu, taifa halina mfumo wa kimaadili na uzalendo!
Matokeo yake ni kila kijana anafikiria kupiga tu.
Taifa legelege limezaa vijana wenye ndoto na matarajio makubwa sana wakizungukwa na umasikini na majukumu mazito, hapo lazima mtu apige tu.
Sijui JK ageukie wapi, ndio maana haya mambo sio ya kuongea mara moja tu, kwakweli tunahitaji kuanza upya tufume upya taifa letu kwa matakwa na namna yetu sisi kama Tanzania.
Katika mfumo wa sasa hata hao wazee ndio wapuuzi nambari moja.
Hatuna pakugeukia kwa kweli.
Hatua za haraka turekebishe sheria zetu katika kuwajibisha maofisa wa serikali na masuala ya rushwa kwa ujumla sheria iongezewe makali kwa kufumua upya pccb na idara ya dpp.
 
utendaji wa mawaziri unaongozwa na kanuni au umri?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Kanuni hizo unazoziongelea zimebakwa kwa miaka 17 sasa na wabakaji wakubwa ni vijana. Hivi hujiulizi kwa nini akina Mzee Ntagazwa hawakuwahi kutapeli enzi za ujana wanakuja kupata kesi uzeeni? Enzi za ujana wao kulikuwa na malezi ya kiuongozi. Wasira alikuwa waziri wakati kijana akafanya vizuri sana lakini uwaziri wake wa sasa kukiwa na OMBWE umekuwa wa hovyohovyo tu
 
Mkuu kweli wewe si muumini wa vijana lakini ukumbuke Nyerere aliukwaa Urais akiwa kijana wa miaka 37 hivi. Na wengi tunakiri kwamba alijitahidi katika uongozi wake na hakuwa mwizi. Wizi na ufisadi ni ni mmomonyoko wa maadili kwenye jamii yetu. Hivi Mkulo ni kijana yule? Mfutakamba je? Nundu? Mponda?

Tanzania bado tuna vijana wazuri tu na waadilifu watafutwe wawe vetted wapewe nafasi. Tatizo hapa katikati ilikuwa ni ukosefu wa vetting na kujua historia na uadilifu wa watu. Wengi walikuwa wakichukuliwa kwa kuwa kuna kauhusiano fulani ka mtaani ama mtandaoni. Nadhani sasa tutarudi kule kwa zamani ambapo wateule walikuwa hawapewi bali wanastahili kuteuliwa.

Ila Kimbunga umesahau kitu kimoja, tunapozungumzia mawaziri kwa mfumo wa sasa ni unazungumzia wabunge, hebu tusaidie mfano wa mbunge wa ccm aliyepitia toka ngazi za michujo na michakato ya kuchaguliwa hadi kushinda ubunge bila michezo michafu!
Nina uhakika tutakesha tunawatafuta hapa, sasa kama hao wengi wamepata ubunge kwa mizengwe, fitna na rushwa kweli hapo kuna kijana wa maana msafi wa kukemea wengine?
Vijana wa hili taifa hatujapona na huu mfumo wa taifa legelege.
Tunahitaji kujadili hasa!
 
naunga hoja uliza ma bank,kampuni za simu jinsi DOT COM wanavyowaliza waajiri wao!wameamua kutowapa madaraka makubwa
 
Hii nakubali kabisa; ndio maana mimi si muumini kabisa wa "ujana" ni sawa sawa na "uongozi bora". Mifano iko mbele yetu na tukipuuzia tunapoteza haki ya kulalamika. Waachwe vijana wawe wabunge na taratibu waanze kujengwa; waendesha mashirika au makampuni yao n.k.. wapewe watu wenye uzoefu wa kuendesha biashara au shughuli zao kwa umakini na weledi..
Mkuu hapa sikubaliani na wewe,tatizo sio vijana wako vijana wengi na wenye uwezo hapa ni system iliopo katika kuchagua vijana hawa kuna mambo na vigezo ambavyo vinazingatiwa kwa chama tawala CCM.Kwanza ni wale watakalinda masilahi ya mafisadi,watakaotii na kupokea amrikutoka juu,wasio na uwezo wa kufikiri na kutoa mawazo yao,SISI TUNAKULA NAWE KULA KWA NAFASI YAKO USIHOJI USIULIZE SISI WOTE MAFISADI!Kwa utaratibu huukwa chamatawala kutegemea uwajibikaji ni ndoto.Hata huo uwajibikaji tuishukuru CHADEMA.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mbaya zaidi katiba hii tuliyonayo inamnyima rais wigo mpana wa kuchagua mawaziri inabidi apitie katika wabunge wake, ambao kwa vijana ni January, Serukamba, Kigwangala, Masele ambao namna walivyopata ubunge inatia shaka kubwa sana. Wadada wa viti maalum ndo akina Vicky Kamata na Ester Bulaya, kazi ipo.
 
Ila Kimbunga umesahau kitu kimoja, tunapozungumzia mawaziri kwa mfumo wa sasa ni unazungumzia wabunge, hebu tusaidie mfano wa mbunge wa ccm aliyepitia toka ngazi za michujo na michakato ya kuchaguliwa hadi kushinda ubunge bila michezo michafu!
Nina uhakika tutakesha tunawatafuta hapa, sasa kama hao wengi wamepata ubunge kwa mizengwe, fitna na rushwa kweli hapo kuna kijana wa maana msafi wa kukemea wengine?
Vijana wa hili taifa hatujapona na huu mfumo wa taifa legelege.
Tunahitaji kujadili hasa!
Mkuu hii uliyonipa ni challenge. Lakini ninachosema mimi ni kwamba siyo vijana tu ndio mafisadi na wezi. Wazee pia ni wezi tu. Tuna tatizo la kukosa maadili. Unakumbuka mara ya kwanza baraza lilipovunjwa waliondoka kwa ufisadi hawakuwa vijana bali wazee wenye umri wao. Hapo uliposema kwamba wanaingia kwenye ubunge kwa rushwa ndipo tatizo linapoanzia. Kama hakuna kijana aliyeingia bila mlungula basi hakuna mzee ambaye pia hakuingia bila mlungula. Hili sasa linakuwa tatizo la kijamii. Lakini pamoja na tatizo hilo bado kuna vijana ambao ni waadilifu wakipewa kazi wataifanya. Utaratibu wa kuwapata ndio ulikuwa na matatizo. Wengi waliingia kwa kuwa wana know who.
 
Japo mimi ni kijana pia si muumini wa ujana.
Vijana wengi waliopewa nafasi za uongozi wameboronga kupita kiasi.

Ila nnachojua awamu hii Jk hatamwacha yule mtoto wa Sheikh Yahya
 
Mkuu mwanakijiji,

Why umekuwa mwepesi kutoa jibu ambalo ulishawahi kuliandikia makala?

Wapee wazee?
 
Umri si tatizo, bali malezi na maadili ndiyo tatizo. Kuna wazee wangapi ambao ni wezi ndani ya serikali?.

Mkapa, Karamagi, Yona, Mramba, Chenge, Lowasa, Rostam, Mboma, Simbo - mkuu wa utawala jeshini je hawa ni vijana?.

Tujenge maadili ya kuwadhibiti, kuwafunga na kuwafilisi mali zao wezi wote wanaoibia serikali yetu. Umri si kigezo hata kidogo.
 
Japo mimi ni kijana pia si muumini wa ujana.
Vijana wengi waliopewa nafasi za uongozi wameboronga kupita kiasi.

Ila nnachojua awamu hii Jk hatamwacha yule mtoto wa Sheikh Yahya
Mkuu Mungi ina maama wewe kama kijana ukipewa Wizara hutaweza kuiongoza?
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom