Vijana Wamemuangusha JK; Wasimuangushe Tena

Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,941
9,947
Kumbukumbu zangu zinaonyesha kwamba JK aliingia madarakani akiwa anaungwa mkono na kundi kubwa la vijana. Naye alipoingia madarakani hakuwatupa mkono vijana. JK aliwateua vijana lukuki kwenye Baraza lake la Mawaziri; wengi wakiwa ni manaibu waziri. Ndani ya safari, akaja kuwapandisha wengi wao kuwa mawaziri kamili: William Ngeleja alipandishwa kushika uwaziri wa Nishati na Madini, Lawrence Masha akachukua uwaziri kamili wa Mambo ya Ndani, Dr. Emmanuel Nchimbi akachukua wizara ya Vijana Utamaduni na Michezo, Ezekiel Maige akachukua Uwaziri kamili wa Maliasili na Utalii na Dr. Cyril Chami naye akautwaa Uwaziri kamili wa Viwanda na Biashara.

Kwenye safari yake ya miaka kumi ambayo haijafika mwisho, JK tayari amewaacha baaadhi ya vijana njiani kwa wao wenyewe kushindwa kutekeleza majukumu aliyowakabidhi hadi umati ukapiga kelele.

Masha alishindwa Ubunge japokuwa watu walikuwa wakipigia kelele utendaji wake. Imekuja hii kubwa ya hawa wa sasa kwamba wamewajibishwa kwa kushindwa kusimamia wizara zao/Ufisadi.

Mimi ni muumini wa vijana kupewa madaraka kwa kuwa bado wana nguvu na wanaweza kuhimili misukosuko. Lakini naona akina Ngeleja, Maige na Chami wameshindwa kuwatendea haki vijana wenzao ambao waliwategemea wao kuwa mfano wa kupigiwa chapua. Wameshindwa kutenda kufikia matarajio ya wananchi wakiwa bado vijana mno.

Nashindwa kuelewa hatima yao ya kisiasa. Kwa umri wa hawa vijana kuondolewa kwenye uwaziri kwa sababu za ufisadi/uwajibikaji ina maana hawana nafasi tena ya kuweza kuwa mawaziri!

Nimpe hongera Dr. Comrade Emmanuel Nchimbi manake naona tangia ameingia serikalini nyota yake imekuwa iking'ara na sasa amekabidhiwa roho za Watanzania; Niamini tu kwamba atatutendea haki na si vinginevyo.

Pamoja na hao kumwangusha lakini naona JK bado ana imani na vijana. Sasa amewaleta akina January, Masele na Simbachawene. Ummy Mwalimu naye amekabidhiwa dhamana ya kuingia kwenye mikutano ya Baraza la Mawaziri. Comrade Nchimbi amekabidhiwa roho za watanzania ambalo ni jukumu zito hasa katika changamoto za sasa za kisiasa. Basi na ninyi vijana mlioingia ama kubakishwa basi msimuangushe tena. Fanyeni kazi kwa uadilifu Tanzania ya sasa si ya mwaka 47 ni ya dot.com mnamulikwa na kila mtu.

Tunasemaje?
 
So kwa sehemu unaamini matatizo ya nchi hii yanatokana na umri. Kwamba ukiweka watu wengi wa umri fulani utapata matokeo fulani and vice versa?
 
So kwa sehemu unaamini matatizo ya nchi hii yanatokana na umri. Kwamba ukiweka watu wengi wa umri fulani utapata matokeo fulani and vice versa?

Mkuu naamini vijana wana muda wa kufanya kazi na kuhimili mikikimikiki na changamoto nyingi ukilinganisha na wakongwe.
 
Mkuu naamini vijana wana muda wa kufanya kazi na kuhimili mikikimikiki na changamoto nyingi ukilinganisha na wakongwe.

Hao wakongwe nao walikuwa vijana wakati fulani. Unaonaje tukisema hawa vijana nao (kama hao wazee) wanaeleka huko huko kwenye ubinafsi, rushwa, uzembe, ubadhirifu nk?

Je hapo suluhisho bado ni umri?
 
Kwenye tope ambalo hii nchi imezama ni ndoto ya alinacha kudhani vijana hawa wa Tz wanaweza kuitoa nchi...!
Ni sawasawa na Scania imeingia kwenye tope huko Bhwilando afu upeleke dereva ambaye toka amejua gari ye ni anaendasha Auto tu, hapo ni utakwama tu na gari litakufa kabisa!

Mi pia ni kijana sana tu, ila kwakweli siridhishwi na namna sisi vijana tunavyoendesha mambo tukiachiwa usukani.
Kama taifa tulishapoteza dira ya namna ya kuandaa vijana, badala yake vijana tumeamini kuwa kila kitu katika mafanikio ni mizengwe na fitna!
Unaweza ukastaajabu ukisimuliwa jinsi hao vijana walivyobaki kwenye hzo wizara.
Kigezo cha utendaji kinaweza kisiwe namba moja....
Bado kama nchi tunahitaji kupika vijana wetu!
Mfano katika uelewa wa siasa za dunia na dira hasa ya nchi kuna kijana anaweza kusimama na kukataa mipango isiyo na tija ya IMF na WB??
Wanasema "experience is the best teacher"
Mi naamini kuna madingi ya utashi na uwezo sana wa kuirudisha hii nchi kwenye dira kuliko hchi kizazi chetu cha masharobaro wakipewa safari ya Marekani wanaona wamepewa dunia nzima na wanaweza kusaini mikataba ya kijinga, wanalingishiana "gamba jeusi" (Diplomatic Passport)
kwa muhtasari, ujana wa watz wengi umezingirwa na ulimbukeni wa usasa na uzuzu!
Inaweza kuwa hatari zaidi watu hawa kuachiwa usukani katika maamuzi ya kinchi.
Ni kweli kuwa wazee ndio wametufikisha hapa ila ni sahihi zaidi kuwa ni bora tupate wazee wenye weredi, utashi kuweza kututoa hapa kuliko vijana ambao wengi wao hata hawajui tumeingia-ingiaje hapa ila tu wanajua tumekwama!
 
Ujana vs Uzee kwenye uongozi wa serikali si hoja ya msingi. La msingi sana ni uzoefu, umakini, na uadilifu. Mwenye vigezo hivyo anaweza kupatikana wa umri wowote na akatufaa. Hata hivyo kwa bwana William Ngeleja rais alichemka sana. We utamteua vipi mtu ka Ngeleja, mwanasheria kijana chekibobu kuongoza wizara nzito, nyeti, kama ile? Nishati na Madini, Fedha, Serikali za Mitaa, Viwanda na biashara, mali asili na utalii -- hakuna room for errors katika uteuzi kwenye hizi wizara. Hizi ni moyo wa serikali na ni uzembe sana kubahatisha katika kuteua mawaziri, makatibu wakuu au wakurungenzi katika hizi wizara.
 
Kufuatia kuondolewa kwa vijana ambao tulitarajia wangekuwa mfano wa kuigwa katika baraza la mawaziri (Maige, Ngeleja, Chami etc), ni wakati kwa vijana wengine katika siasa na uongozi katika taasisi za seraikali na binafsi kuelewa maana ya madaraka na kuepuka kubweteka.

Majigambo siyo kigezo cha kuwa kiongozi wa kuigwa.
 
Mkuu hapo na mimi nakuunga mkono, ni aibu kubwa kwa rika letu kushindwa kuishinda tamaa na kuwanyesha wazee tuko tayari kuliongoza taifa, japokuwa kuna akina megawatt waliwekwa kwa maslai ya akina ra.
Tusife moyo , wapo upande wa pili akina jj mnyika , zitto na wengineo wengi , wanatoa ishara ya uwepo wa hiki kizazi.
 
Kufuatia kuondolewa kwa vijana ambao tulitarajia wangekuwa mfano wa kuigwa katika baraza la mawaziri (Maige, Ngeleja, Chami etc), ni wakati kwa vijana wengine katika siasa na uongozi katika taasisi za seraikali na binafsi kuelewa maana ya madaraka na kuepuka kubweteka.

Majigambo siyo kigezo cha kuwa kiongozi wa kuigwa.
Mkuu hilo ni funzo kubwa kwa vijana wa kizazi hiki. Wakipewa madaraka wafanye kazi wakijua wao ni role model ya vijana wote wa nchi hii. Bila hivyo tutarudi kulekule kwenye kauli ya Vijana ni Taifa la kesho.
 
Mkuu mi nadhani JK mwenyewe kashindwa kuwa na msimamo,we unadhani angekuwa na msimamo na mtu mwenye karipio kali,mfuatiliaji na wa kuwajibisha,je hao vijana wangefanya hujuma?na je kuna nini hasa mpaka anashindwa kuwakaripia na kuwajibisha mpaka iwe shinikizo?je kuna maslahi anayaangalia?kutokana na msimamo wa JK ulivyo inaonekana wazi hata hao vijana wapya wanaenda kuendeleza hujma.
 
Mkuu hilo ni funzo kubwa kwa vijana wa kizazi hiki. Wakipewa madaraka wafanye kazi wakijua wao ni role model ya vijana wote wa nchi hii. Bila hivyo tutarudi kulekule kwenye kauli ya Vijana ni Taifa la kesho.

Kimbunga, mimi nina mtizamo tafauti kabisa kuhusu hii issue. Kwakifupi mimi bado naona vijana ni muhimu kwenye uongozi lakini si vijana wa "mtandao" au wanaojua kusema ndio kila kitu bila ku-challenge issues. JK tokea baraza lake la kwanza (akina Masha) hawa sio kwamba walikuwa na uwezo; bali waliwekwa kwasababu ni watu wake wakaribu. Vijana wachapakazi naamini wapo lakini most likely hawako kwenye mtandao na hivyo ni vigumu kupewa nafasi hizo. As I see it, JK hawezi kuchagua mtu ambaye atakwenda kinyume na masharti yake/hapokei order. Ni wazi aliowateua toka mwanzo ni reflection yake yeye. JK amepata nafasi lukuki ya kujisahihisha lakini bado anatuletea vijana matapeli; ni wazi yeye huwa anaangalia/chagua kwenye pool ambayo walioko huko wataweka interest zake mbele na sio za taifa. Sidhani kama kuna mtu mwenye msimamo, work ethics, na mzalendo wa kweli anaweza kufanya kazi na JK akafanikiwa bila mikiki mikiki. Ni kweli kwamba vijana wana-nafasi kubwa yakufanya vizuri kwasababu ya uwezo wao mentally, and physically. Nakubaliana na wanaosema experience matters, lakini tuangalie sana kufanya kazi na mazoea bila kupanua mawazo zaidi (kuongeza uelewa), kuna madhara yake pia. Na hii iko sana kwenye ofisi za serikali; mtu anafanya kazi kwa miaka zaidi ya 30 hataki hata ku-think outside the box. Ku-conclude tu mimi siwalaumu hawa vijana, bali nalaumu aliyewachagua. JK amechagua "sample" mbovu hivyo imeshindwa ku-deliver. Same applies kwa spika, hatuwezi kusema wanawake wametuangusha kwenye uongozi wakati waliochaguliwa (e.g. spika, na wabunge wengi wa viti maalum) wamechaguliwa kwa shughuli maalumu.
 
Kimbunga, hebu nikuulize, hao vijana watakaoteuliwa na Kikwete wamezaliwa wapi na wakalelewa vipi? Vipi kijana aliyezaliwa ndani ya mfumo huu, akalelewa na kukulia ndani ya mfumo huu, akawa bega kwa bega na wazee wake ndani ya mfumo huu, akafaidi matunda ya mfumo huu, akawekeza katika mfumo huu na ana matumaini ya kuvuna ndani ya mfumo huu, ukamtegemea kufanya kinyume cha status quo ilifomfikisha hapo!

Hata mtoto mdogo ukimwamsha usingizini sidhani kama atashindwa kujua kuwa matatizo yetu yanasababishwa na nini lakini yaonekana wewe kama vile mbuni, you have decided to bury your head in the sand! Naomba uelewe wewe Kimbunga kuwa katika vita hii tuliyo nayo mbele yetu kama taifa watu wasio na msimamo kama wewe ni wanafiki na ni wa hatari kweli kweli na kadri siku zinavyosonga mbele, ndivyo mtakavyozidi kujiumbua!

Tulipofikia kama taifa ni lazima tutambue kuwa tunakoelekea siko, tunaelekea kubaya na dawa pekee ni kupiga about turn. Nahodha wetu CCM keshalemaa, haoni wala hasikii, amezama kwenye tope pamoja na wafuasi wake wote, kwa nini Kimbunga unataka na sisi wengine tuzame naye? Hapana, hilo hatutakubali...mfumo umeoza na njia pekee ya kujikwamua ni nahodha huyu kuketishwa pembeni pamoja na marugaruga wake wooote, period.
 
Last edited by a moderator:
..give me a break!!

..JK anawateua Ngeleja na Malima kwa wizara nyeti kama Nishati na Madini what do u expect??

..halafu juu yake anamteua swahiba wake David Jairo kuwa Katibu Mkuu.
 
Ndugu zangu mna moyo, tena moyo wa kutoamini kinachotokea mbele ya macho yenu. Ndio kukamilika kwa mazingaombwe! Mnataka kujiaminisha kabisa kuwa ukibadilisha rangi na ukubwa wa ndoo basi maji utakayochota toka kisima kichafu yatageuka kuwa masafi. Kwa hiyo unaendelea kudumbukiza ndoo za ukubwa mbalimbali na za rangi mbalimbali...

Huamini kuwa unakoroga uchafu tu. Mna moyo wenzetu!
 
Kumbukumbu zangu zinaonyesha kwamba JK aliingia madarakani akiwa anaungwa mkono na kundi kubwa la vijana. Naye alipoingia madarakani hakuwatupa mkono vijana. JK aliwateua vijana lukuki kwenye Baraza lake la Mawaziri; wengi wakiwa ni manaibu waziri. Ndani ya safari, akaja kuwapandisha wengi wao kuwa mawaziri kamili: William Ngeleja alipandishwa kushika uwaziri wa Nishati na Madini, Lawrence Masha akachukua uwaziri kamili wa Mambo ya Ndani, Dr. Emmanuel Nchimbi akachukua wizara ya Vijana Utamaduni na Michezo, Ezekiel Maige akachukua Uwaziri kamili wa Maliasili na Utalii na Dr. Cyril Chami naye akautwaa Uwaziri kamili wa Viwanda na Biashara.

Kwenye safari yake ya miaka kumi ambayo haijafika mwisho, JK tayari amewaacha baaadhi ya vijana njiani kwa wao wenyewe kushindwa kutekeleza majukumu aliyowakabidhi hadi umati ukapiga kelele.

Masha alishindwa Ubunge japokuwa watu walikuwa wakipigia kelele utendaji wake. Imekuja hii kubwa ya hawa wa sasa kwamba wamewajibishwa kwa kushindwa kusimamia wizara zao/Ufisadi.

Mimi ni muumini wa vijana kupewa madaraka kwa kuwa bado wana nguvu na wanaweza kuhimili misukosuko. Lakini naona akina Ngeleja, Maige na Chami wameshindwa kuwatendea haki vijana wenzao ambao waliwategemea wao kuwa mfano wa kupigiwa chapua. Wameshindwa kutenda kufikia matarajio ya wananchi wakiwa bado vijana mno.

Nashindwa kuelewa hatima yao ya kisiasa. Kwa umri wa hawa vijana kuondolewa kwenye uwaziri kwa sababu za ufisadi/uwajibikaji ina maana hawana nafasi tena ya kuweza kuwa mawaziri!

Nimpe hongera Dr. Comrade Emmanuel Nchimbi manake naona tangia ameingia serikalini nyota yake imekuwa iking'ara na sasa amekabidhiwa roho za Watanzania; Niamini tu kwamba atatutendea haki na si vinginevyo.

Pamoja na hao kumwangusha lakini naona JK bado ana imani na vijana. Sasa amewaleta akina January, Masele na Simbachawene. Ummy Mwalimu naye amekabidhiwa dhamana ya kuingia kwenye mikutano ya Baraza la Mawaziri. Comrade Nchimbi amekabidhiwa roho za watanzania ambalo ni jukumu zito hasa katika changamoto za sasa za kisiasa. Basi na ninyi vijana mlioingia ama kubakishwa basi msimuangushe tena. Fanyeni kazi kwa uadilifu Tanzania ya sasa si ya mwaka 47 ni ya dot.com mnamulikwa na kila mtu.

Tunasemaje?

Nani kakudanganya vijana wote wanafaa kuwapa dhamana ya uongozi especialy kama ni aina yake?
 
Mkuu Unstoppable nimeipenda hiyo comment yako hasa kwenye sample selection. Tunaweza tukawa na shida hapo. Uzalendo na ethics ni muhimu. Vijana wanatakiwa waonyeshe uzalendo wakati wanawatimikia wananchi. wakipewa kazi wafanye wasije wakawapa watu la kusema kwamba vijana hawawezi.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu naamini vijana wana muda wa kufanya kazi na kuhimili mikikimikiki na changamoto nyingi ukilinganisha na wakongwe.

Unaposema vijana sema baadhi ya vijana maana ukisema vijana kwa ujumla utakuwa unajidanganya maana walio wengi hasa wa ccm wamedhihirisha kutokuwa na uchungu na taifa na kuishia kama ilivyo jadi kwa chama chao cha magamba!
 
Mkuu Mag3 shambulia hoja. Hapa hoja ni utendaji wa vijana kama wanawawakilisha vijana ipasvyo ili kuwapa vijana nguvu kwamba vijana si taifa la kesho.
 
Last edited by a moderator:
Hao wakongwe nao walikuwa vijana wakati fulani. Unaonaje tukisema hawa vijana nao (kama hao wazee) wanaeleka huko huko kwenye ubinafsi, rushwa, uzembe, ubadhirifu nk?

Je hapo suluhisho bado ni umri?
Mkuu unaamini kwamba vijana ni taifa la leo? Tatizo ni kwamba ukiwa kijana ukawa mnafiki ukiwa mzee utakuwa mchawi. Tunataka vijana watende kazi kwa uadilifu kwa kuwa miaka ya karibuni tumekuwa tukisema wazee ndio wametufikisha hapa. Leo vijana wanapewa nafasi hawawa approve wrong wazee. Hii si haki kwa vijana ambao hajapewa nafasi.
 
Back
Top Bottom