Waziri Chami amwaga chozi - Awataka watumishi wamuombee asiadhirike | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Chami amwaga chozi - Awataka watumishi wamuombee asiadhirike

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 9, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145

  • AWATAKA WATUMISHI WAMUOMBEE ASIADHIRIKE

  na Daniel Mwita


  ​

  SIKU mbili baada ya Rais Jakaya Kikwete kuwaapisha mawaziri wapya, aliyekuwa Waziri wa Viwanda na Biashara aliwaaga wafanyakazi wa wizara hiyo kwa majonzi huku akilalamika kuwa ameng’olewa uwaziri kwa kosa lisilomhusu.


  Chami ambaye ni Mbunge wa Moshi Vijijini, alitoa kauli hiyo jana wakati akizungumza na watumishi wa wizara hiyo mara baada ya kukabidhi ofisi kwa Waziri mpya, Dk. Abdallah Kigoda.

  Huku akionyesha huzuni kubwa na kuumizwa moyoni na uamuzi wa Rais Kikwete kumng’oa madarakani, Dk. Chami aliwaomba watumishi hao wamwombee kwa Mungu ili asiaibike zaidi huko aendako.


  “Ndugu zangu niombeeni sana kwa Mungu asiniadhiri kama ilivyotokea sasa ili niweze kufanikiwa huko ninakokwenda na ni matumaini kwamba kila mmoja wenu atafanya hivyo,” alisema Dk. Chami kwa huzuni kubwa.


  Waziri huyo wa zamani ambaye kwa miezi kadhaa iliyopita alikuwa nchini India kwa matibabu, alisisitiza kuwa ameadhibiwa kwa makosa ambayo hakuhusika nayo kwa kuwa hajawahi kufanya ubadhirifu wowote wa mali za umma katika kipindi chote cha uongozi wake.


  Alisema anatambua fika kwamba yeye ni mwadilifu katika nyanja zote kwenye wizara hiyo, lakini alisisitiza tena na tena kwamba ameadhibiwa kwa makosa ambayo hakuyatenda.

  Kutokana na kauli yake ya kuhuzunisha, mtumishi mmoja wa kike ambaye alikataa kutaja jina lake, alimfariji na kumtia moyo waziri wake huyo wa zamani kwa kusema kuwa kama anaamini kwamba aliwatumikia Watanzania kwa uaminifu, Mungu atakuwa pamoja naye, huku akinukuu mfano wa Ayubu katika kitabu cha Biblia.

  “Kwa kuwa tunaamini kwamba wewe ulikuwa mtumishi mwaminifu, Mungu atakuwa pamoja nawe hatakuadhibu na kutolea mfano wa Ayub kwenye kitabu cha Biblia kwamba aliadhibiwa kwa makosa ambayo hakustahili, lakini Mungu aliruhusu iwe hivyo. Mungu atakusaidia, hatakuacha,” alisema mtumishi huyo huku wenzake wakitikisa vichwa kuashiria kumuunga mkono.


  Mbali ya kuzungumzia kusikitishwa na kung’olewa kwenye uwaziri kwa kuonewa, Dk. Chami aliwapa wosia watumishi hao kuacha tabia ya majungu na kusemana kazini kwani vitu hivyo ni hatari katika maeneo ya kazi na vinaleta mahusiano mabaya kazini.


  “Mimi ninaondoka kwenye wizara hii, ninyi nyote ni mashahidi kuwa mimi sikuwahi kutuhumiwa kwa kosa lolote, ila imenilazimu kuondoka kwa sababu ya uajibikaji wa kisiasa, naomba niseme kitu kimoja kwenu na nadhani mkikitilia mkazo mtaweka mahusiano mazuri kazini, tabia ya watu kupinduana sio nzuri maana kuna wakurugenzi wasaidizi wanaotaka kuwa wakurugenzi hivyo wanapika majungu ili wakurugenzi waondolewe na wao washike nyadhifa hizo,” alisema Dk. Chami.


  Aliwataka kuwa wadilifu hasa katika swala zima la fedha, ambapo alisema endapo watendaji mbalimbali wa serikali watazingatia nidhamu ya fedha za umma, wizara nyingi zitakuwa na maendeleo makubwa.


  Hata hivyo gazeti hili lilipomtaka afafanue kama kuna ubadhirifu wowote wa fedha za umma umefanyika katika wizara hiyo alikana na kusema anachofanya ni kusisitiza uajibikaji wenye tija kwa watumishi wa umma.


  Chami na Naibu wake, Lazaro Nyalandu, ambaye kwa sasa amehamishiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, walikuwa kwenye mgogoro mkubwa unaotokana na mitazamo tofauti ya kikazi hususan suala la Mkurugenzi wa Shirika la Viwango nchini (TBS), Charles Ekelege.


  Katika sakata hilo, Chami alikuwa anamkingia kifua mkurugenzi huyo anayekabiliwa na tuhuma nzito zikiwemo za utendaji mbovu wa shirika hilo, huku Nyarandu akitaka bosi huyo wa TBS asimamishwe kupisha uchunguzi dhidi yake.


  Kwa upande wake, Nyalandu alitoa waraka uliombebesha mzigo waziri wake, Dk. Chami, akisema alimpa ushauri wa kumsimamisha kazi Ekelege kupisha uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), lakini hakutekeleza.


  Katika barua hiyo ya Februari 10, mwaka huu, kwenda kwa Chami, alimweleza kuwa wabunge walikuwa wanashuku kuwa mkurugenzi huyo alitoa taarifa zisizo sahihi.


  “Kikao cha briefing cha CAG na waheshimiwa wabunge, TBS imeshutumiwa kuhusiana na ukaguzi wa magari nje ya nchi na mchakato wote unaohusiana na suala hilo,” inasomeka dokezo hilo la Nyalandu.


  Alisema wabunge walioshiriki katika ziara ya nchi za Hong Kong na Singapore wametoa madai kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBS aliwadanganya juu ya kampuni zinazofanya ukaguzi wa magari na bidhaa nyingine nje ya nchi na wakatoa madai kuwa TBS imetoa taarifa tofauti na yale waliyoyaona katika ziara.


  Dk. Chami alikiri kupokea ushauri huo lakini, akasema wakati anautoa kulikuwa hakuna tuhuma zozote za kamati kuhusu Ekelege.


  “Ushauri ulikuwa mzuri lakini Ekelege ni mteule wa Rais hivyo huwezi kwenda kwa Rais kumtaka amwondoe wakati hakuna taarifa yoyote inayoonyesha tuhuma zake. Kuna njia mbili za kumsimamisha: kwanza, kumshauri Rais na pili hizo ripoti dhidi ya Ekelege zipelekwe kwenye Bodi ya Wakurugenzi ya TBS na baada ya hapo wakitoa maazimio ndiyo waziri anaweza kwenda nayo kwa Rais,” alisema Dk. Chami.


  Rais Kikwete wiki iliyopita alifanya mabadiliko makubwa katika Baraza la Mawaziri kwa kuteua wapya watatu na manaibu 10 huku akiwaacha sita.


  Pia aliwapandisha manaibu mawaziri wanne kuwa mawaziri kamili na kuwahamisha wizara mawaziri wanane na manaibu waziri sita, huku mawaziri na manaibu waziri 22 wakibaki katika wizara zao za awali.


  Kutokana na mabadiliko hayo, idadi ya mawaziri na manaibu wao sasa imeongezeka kutoka 50 katika baraza la awali hadi 55. Mawaziri kamili wameongezeka kutoka 29 hadi 30 huku manaibu waziri wakiongezeka kutoka 21 hadi 25.


  Mawaziri ambao wameng’olewa na wizara walizokuwa wakiziongoza kwenye mabano ni Mustafa Mkulo (Fedha), Dk. Hadji Mponda (Afya na Ustawi wa Jamii), William Ngeleja (Nishati na Madini), Dk. Cyril Chami (Viwanda na Biashara), Omar Nundu (Uchukuzi) na Ezekiel Maige (Maliasili na Utalii).


  Panga hilo la mabadiliko liliwakumba pia Manaibu Waziri wawili, Dk. Lucy Nkya (Afya na Ustawi wa Jamii) na Dk. Athumani Mfutakamba (Uchukuzi).


  Mawaziri wapya walioteuliwa na wizara zao kwenye mabano ni Mbunge wa Handeni, Dk. Abdallah Kigoda (Viwanda na Biashara), Mbunge wa Kalenga, Dk. William Mgimwa (Fedha) na Mbunge wa Kuteuliwa Profesa Sospeter Muhongo (Nishati na Madini).


  Walioteuliwa kuwa Manaibu Waziri ni Mbunge wa Rufiji Dk. Seif Suleiman Rashid (Afya na Ustawi wa Jamii), Mbunge wa Kibakwe, George Simbachawene (Nishati na Madini), Mbunge wa Bumbuli, January Makamba (Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia), Mbunge wa Buchosa, Dk. Charles Tizeba (Uchukuzi) na Mbunge wa Mvomero, Amos Makala (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo).


  Wengine ni Mbunge wa Makete, Dk, Binilith Mahenge (Maji), Mbunge wa Shinyanga Mjini, Stephen Maselle (Nishati na Madini – Madini), Mbunge wa Viti Maalumu, Angela Kairuki (Katiba na Sheria) na Wabunge wa Kuteuliwa Janet Mbene na Saada Mkuya Salum wote Fedha.


  Naibu Mawaziri waliopandishwa na kuwa mawaziri kamili wamo, Christopher Chiza (Kilimo, Chakula na Ushirika), Dk. Harrison Mwakyembe (Uchukuzi), Dk. Fenella Mukangala (Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo) na Khamis Kagasheki (Maliasili na Utalii).

   
 2. p

  politiki JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  sawasawa ulivyotimuliwa ofcourse ulikuwa na maslahi yako binafsi na mkurugenzi yule otherwise usingemkia kifua namna ile na acha kupotosha umma kwa kudai hulikuwa huna uwezo wa kumfukuza kwani hakuna aliyekwambia umfukuze bali umsimamishe pending on investigation lakini ukaamua kuvaa miwani ya mbao unastahili yote yaliyokufika nami ningekuwa rais nchi hii ningekuburuza mahakamani kwa kukataa ushauri ambao umepelekea taifa hili kupata hasara. kama kweli ukuliona bomu lile ambalo kila aliyena macho aliliona bali haukustahili hata kuwa waziri wa nyumba kumi. full of excuses go away disgraced minister.
   
 3. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #3
  May 9, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mwacheni apumzike. Mambo mengi yamemkuta huyu bwana mdogo.

  Kwanza bado mgonjwa,
  Pili walivunja nyumba yake huko kibosho na kukomba kila kitu,
  Tatu kazushiwa kifo,
  Nne kapungua uzito sana,
  Tano kafukuzwa uwaziri, na
  Sita, fungakazi 2015 Jimbo lake linaenda Chadema.

  Kwa madhila yote haya, kidume lazima mchozi umtoke.
   
 4. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #4
  May 9, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Ekelege kamponza
   
 5. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #5
  May 9, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Ndio faida ya Ushikaji katika kaziiiiii

  From PJN @ Selous Forest
   
 6. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #6
  May 9, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,528
  Likes Received: 882
  Trophy Points: 280
  imtetea ekelege

  sasa ndio ajue sisiemu ni chaka
   
 7. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #7
  May 9, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,198
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Mzee pumzika jimbo linahitajika na CDM kwi! Kwi! Kwi! Kwi!.......!!!!!
   
 8. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kama alitenda haki mungu atakulipia tu wala usiwe na wasiwasi maana yote yawezekana na unaweza pata kikubwa zaidi ya uwaziri uliokuwa nao
   
 9. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,314
  Likes Received: 5,606
  Trophy Points: 280
  Ekelege!!!!!mkongwe kwenye system tunasubiri tuone atafanywaje zaidi kufichwa tu na kurudi kijiweni pale makaburini!!ndio hao hao!!ukiambiwa hizo pesa zilitumika.......utakataa??EPA,Meremeta walisemaje?pesa zimetumika mambo ya usalama........period
   
 10. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #10
  May 9, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,178
  Likes Received: 10,517
  Trophy Points: 280
  Anasema wamwombee huko aendako kwasababu anajua fika kabisa kuwa atapoteza jimbo lake huko Moshi... Pole sana Chami CDM lazima ilichukue jimbo hilo.
   
 11. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #11
  May 9, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Asilie aende kwa Mengi atampa kazi pale IPP kwani wanatoka Moshi wote.
   
 12. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #12
  May 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Dongo kubwa kwa Nyalandu.

  Naona kuna hoja kuhusu Dr. Kumchukulia hatua Ekelege. Serikali haifanyi kazi kwa maneno inafanya kazi kwa taarifa.

  Mbona Dr. Chami ameondoka lakini Ekelege bado anapeta? Nilidhani Waziri mpya angeanza naye.
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  May 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Si angepewa uwaziri usio na wizara maalumu!
   
 14. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #14
  May 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Pamoja na hayo yote; afanye hima apate muafaka na mamsapu wake kisha arudi kwenye fani yake aliyosomea!! Mbona anajenga hofu ya maisha ilhal vyuo viko vingi na vinahitaji wahadhiri wengi sana wa fani yake! Ni siasa pekee inayoambatana na kuchafuana pamoja na majungu ila kwenye vyuo wewe ni kumwaga nondo vijana wakahangaike nazo! Hata ukiwa na mishe mishe nyingine hakuna wa kukufuata fuata. Rudi kwenye fani yako Mangi siasa haikufai!!!
   
 15. A

  Awo JF-Expert Member

  #15
  May 9, 2012
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 790
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Ndio huwa siwaelewi! Kwa hiyo unakuwa Waziri mwadilifu wakati watu wote chini yako ni wezi, unakaa tu huchukui hatua halafu unalialia hapa! Acha ujinga Chami!
   
 16. SIMBA WA TARANGA

  SIMBA WA TARANGA JF-Expert Member

  #16
  May 9, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 992
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Apumzike kwa amani huko aendako (sijui anaenda wapi)
   
 17. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #17
  May 9, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280

  Ekelege wala sio mkongwe kwenye system..hakuna mtu mbaya kama yule..kile cheo amekishika baada ya kumuua alie kua akikalie kiti kile ambae alikua ni Finance and Admin Manager na wakongwe wote wa TBS makao makuu wanajua..jamaa mshirikina hakuna mfano na fisadi sana..na bado..atateseka sana na hatokua na mwisho mzuri..kawachinja sana watu pale..muoneni vile vile..sio mtu yule na mungu atamkomesha we ngoja tu!
   
 18. The Stig

  The Stig JF-Expert Member

  #18
  May 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 884
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 80
  Ningekuwa mfanyakazi wa wizara, wakati anapomwaga chozi ningenyosha mkono na kumuambia Chami; "Usilie, huo ndiyo Uofisa"

  On a serious note, Chami na Nundu ni mifano mizuri kwa watu wanaopewa madaraka makubwa halafu wanashindwa kuyatumia ipasavyo. Mimi binafsi huwa najitahidi sana kutokosea kwenye hilo.
   
 19. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #19
  May 9, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Nae ameingia kwenye list ya wezi wanaosubiri kunyongwa 2015.
   
 20. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #20
  May 9, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  majuto mjukuu!!
   
Loading...