Baraza Jipya: Pongezi kwa JamiiForums, WanaJF watatu(VERIFIED) waukwaa uwaziri

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,615
113,834
Wanabodi,

Nimelisikia Baraza Jipya kupitia Clouds Radio, miongoni mwa mawaziri, ni members watatu wa JF ambao ni verified, wameteuliwa kuwa mawaziri.

Hawa ni Mhe. Mwigulu Nchemba, Mhe. Nape Mnauye na Mhe. Dr. Kigwangala.

Inawezekana na wengine pia wapo ambao ni JF members ila sio verified, na pia kwa vile sura mpya ni nyingi, pia inawezekana miongoni mwao ni members wetu humu ila sijawajua.

Kitendo cha wana JF kuteuliwa mawaziri kwenye baraza dogo la Rais JPM, hii ni plus on JF side, kama memberrs wake wameteuliwa, inawezekana miongoni mwa sifa zilizowafanya kuteuliwa, ni pamoja na michango yao humu JF!.

Japo kuna baadhi yao sisi humu JF tumekuwa tukiwadharau sana, tukiwaona ni viazi, vibonde au ni vilaza tuu!, lakini kumbe "ganda la mua la jana, chungu aona kivuno", kile unachokidharau wewe, mwenzako anakithamini!, hivyo JPM amewaona hao wana jf watatu wanafaa kumsaidia, hivyo kuwamo. Kumbe ule msemo "nabii hakubaliki nyumbani" ni kweli kabisa!, hawa watu watatu humu jf tumewadharau sana humu na kuwabeza!, a lesson kwetu jf, tusiwe tunawabeza watu humu bila sababu za msingi, huwezi jua kesho nani atakuwa nani au atakusaidia vipi!.

Sisi kama wana jf, members wenzetu wanapofanikiwa, tunawajibika kuwasupport kwa hali na mali, ikiwemo kuwapongeza na kuwapa angalizo ya kazi kubwa iliyopo mbele yao!.

Kuna wakati Katibu Mkuu wa CCM, Kinana, aliwahi kuwabeza baadhi ya mawaziri kwa kuwaita ni 'mawaziri mizigo!', ila pia hakuna ubishi, kuna baadhi ya wabunge haswa wa viti maalum na wale wa kuteuliwa, wengine wana merits za kuwafanya wateuliwe, na wengine wanaukwaa ubunge kwa kubebwa tuu, ili waje kutoa huduma za kibinaadam, au baada ya kufanya kazi nzuri ya 'kubeba' nao 'wanabebwa!, inapotokea wabunge hawa wa kubebwa, kuukwaa uwaziri, then inamaanisha, uwaziri wao ni wa matokeo yale yale ya kubebwa!, hivyo kwa maoni yangu, wanamtihani mmoja mkubwa, "ukibebwa bebeka!", na sio ukibebwa bweteka!. Namuona Magufuli kama vile pia ameanza na kuibeba 'mizigo' tena kwa baadhi ya mizigo hii,ni mizigo mizito isiyobebeka, ambayo mbele ya safari itamuelemea na ama atalazimika kuibwaga, au uzito ukimzidia, itamwagusha na ataanguka nayo!.

Lazima tukiri, hawa wana jf wote walioukwaa uwaziri ni vichwa, ila huyu Mwana jf mwenzetu pale Wizara ya Afya, atakuwa na kazi kubwa ya ziada!, yeye ni dakitari kabisa, yaani a Medical Doctor, ndio kapewa unaibu, lakini bosi wake, sio tuu ni kama 'kiazi' fulani hivi, chenye kila dalili ya ni 'kidumu'!. Wale wataalamu wa mambo ya ndoo na vidumu, wanashauri kubeba ndoo na kidumu, ili maji ya kwenye ndoo yakimwagika, unabaki na kidumu, kinaokoa jahazi!, sasa kama wizara nyingine, inapotokea kidumu ndio kimetangulizwa mbele na ndoo nyuma, inamaana maji ya kidumu ndicho yatatangulia kumwagika, na ndoo ndio itaokoa jahazi!. Hapo Afya Kazi ipo!.

Ila pia tusemazane ukweli, line up ya wabunge wa viti maalum ya CCM, sii mchezo!, kwa watu wa Kanda ya Ziwa na ule udhaifu wetu wa mambo yetu yale, hivi vidumu au mali za watu sijui kama zitasalimika!, ukiona mtu ameteuliwa uwaziri au unaibu, huku hana merits zozote visible, then itakubidi tuu uelewe, huo uwaziri ni ama wa invitation to treaty ama ni asante kwa huduma nzuri!.

Hongera sana Mhe. Mwigulu Nchemba, Mhe. Nape Nnauye na Mhe. Dr.
HKigwangalla. Mfanye kazi na kudeliver ili msiilet down jf.
Hongereni sana!, Hongera JamiiForums.

Paskali
 
Hao vijana wote ni hazina ya taifa. Tunatarajia wawe marais wa baadae.

Ha ha ha HAMY D sio kila mtu anafaa kuwa rais! Ndio maana wewe leo hii ni mtumishi wa kawaida unafanya kazi za chama online. Kwa hiyo na wewe kwa maandishi yako na kazi kubwa uliyofanya ya kutetea chama basi tuseme unafaa kuwa rais?

Nadhani kuwa vigezo vingi vya kuzingatia na kwa wakati muafaka.
 
Nilikuwa natamani siku zote mhongo arudishwe kwenye wizara ileile ya nishati na Madini na lukuvi amalizie Kazi aliyoianza. Nilitamani Mwakyembe, January, kigwangara, nchemba wawemo. Cha kufurahisha ni uwepo wa Anthony Mavunde kwenye wizara inayohusu vijana. Thanks Magufuli! Wakafanye Kazi na wasikuangushe.
 
Hao vijana wote ni hazina ya taifa. Tunatarajia wawe marais wa baadae.

Kwahiyo leo hii mtu akiisha kuwa verified user wa JF kisha akateuliwa
kuwa waziri au naibu waziri basio huyo ana nadaliwa kuwa Rais
wa baadae wa Tanzania... This might be a joke to JPM.
 
Nape ameteuliwa kuwa waziri kwasabab ali weza kupiga Gitaa akiwa na Magufuli kwenye hafla iliyo fanywa na Wasanii Mlimani city ya kumuaga kikwete.
 
Back
Top Bottom