Baraza Jipya: Pongezi kwa JamiiForums, WanaJF watatu(VERIFIED) waukwaa uwaziri

Ukitaka kujua tofauti ya wanasiasa na viongozi wa CCM wanaojua kucheza karata vizuri na wanaoweza kubadirika kufuatana na hali ya hewa ya kisiasa basi MUANGALIE LUKUVI. Huyu Jamaa ana mahesabu makali sana na anajua kunusa fursa.ni SEASONED POLITICIAN! Muulize anasemaje kuhusu miaka 7 sikia jibu lake halafu muulize MKAMIA au ccm-Akademia(Jerry Muro) swali hilohilo majibu yao yatakuambia ni kwanini LUKUVI Maraisi wote waliopita wanaendelea kumwamini na kumpa nafasi
 
Naamini si u jf members wala michango yao iliyowafanya wateuliwe bali je,wanaweza ku deal na upinzani kwa namna yoyote ile?Wanauwezo wa kusema ndiyo kwa kila jambo analowatuma anayewateua bila kuhoji wala kusimama ktk misimamo yao?
 
Kaka Pascal Mimi napendaga Sana kusoma makala zako humu jf. Nimesoma hoja yako hapo juu lkn kupitia ulivyoandika nimepata swali la kukuuliza.

Je wakati mheshimiwa Rais anateua Baraza la mawaziri vip nyie waandishi wa habari mliwahi kuuhabarisha umma kuhusu uteuzi wa sekta nyeti ubase kwenye proffessiolism ?

Au mnasubiri outcome ndo muanze Kupost habari za kulaumu

Sent using Jamii Forums mobile app
Karibu pande hizi.
P
 
Yani hawa watu watatu wametia aibu.
Huyu kigwa ndio kabisa ni waziri na wizara yake imelufa hakuna stimulaji package yoyote anayoishauri kwa rais au waziri wa fedha.
Jamaa lipo Twitter linatukana watu na nje ya box yake na vijembe majivuno.
Yani sijui kwa nini januar makamba hatumiwi.
Ingetakiwa pale dodoma January ndio awe rais sasa hivi nchi ingekuwa mbali sana .
Wanabodi,

Nimelisikia Baraza Jipya kupitia Clouds Radio, miongoni mwa mawaziri, ni members watatu wa JF ambao ni verified, wameteuliwa kuwa mawaziri.

Hawa ni Mhe. Mwigulu Nchemba, Mhe. Nape Mnauye na Mhe. Dr. Kigwangala.

Inawezekana na wengine pia wapo ambao ni JF members ila sio verified, na pia kwa vile sura mpya ni nyingi, pia inawezekana miongoni mwao ni members wetu humu ila sijawajua.

Kitendo cha wana JF kuteuliwa mawaziri kwenye baraza dogo la Rais JPM, hii ni plus on JF side, kama memberrs wake wameteuliwa, inawezekana miongoni mwa sifa zilizowafanya kuteuliwa, ni pamoja na michango yao humu JF!.

Japo kuna baadhi yao sisi humu JF tumekuwa tukiwadharau sana, tukiwaona ni viazi, vibonde au ni vilaza tuu!, lakini kumbe "ganda la mua la jana, chungu aona kivuno", kile unachokidharau wewe, mwenzako anakithamini!, hivyo JPM amewaona hao wana jf watatu wanafaa kumsaidia, hivyo kuwamo. Kumbe ule msemo "nabii hakubaliki nyumbani" ni kweli kabisa!, hawa watu watatu humu jf tumewadharau sana humu na kuwabeza!, a lesson kwetu jf, tusiwe tunawabeza watu humu bila sababu za msingi, huwezi jua kesho nani atakuwa nani au atakusaidia vipi!.

Sisi kama wana jf, members wenzetu wanapofanikiwa, tunawajibika kuwasupport kwa hali na mali, ikiwemo kuwapongeza na kuwapa angalizo ya kazi kubwa iliyopo mbele yao!.

Kuna wakati Katibu Mkuu wa CCM, Kinana, aliwahi kuwabeza baadhi ya mawaziri kwa kuwaita ni 'mawaziri mizigo!', ila pia hakuna ubishi, kuna baadhi ya wabunge haswa wa viti maalum na wale wa kuteuliwa, wengine wana merits za kuwafanya wateuliwe, na wengine wanaukwaa ubunge kwa kubebwa tuu, ili waje kutoa huduma za kibinaadam, au baada ya kufanya kazi nzuri ya 'kubeba' nao 'wanabebwa!, inapotokea wabunge hawa wa kubebwa, kuukwaa uwaziri, then inamaanisha, uwaziri wao ni wa matokeo yale yale ya kubebwa!, hivyo kwa maoni yangu, wanamtihani mmoja mkubwa, "ukibebwa bebeka!", na sio ukibebwa bweteka!. Namuona Magufuli kama vile pia ameanza na kuibeba 'mizigo' tena kwa baadhi ya mizigo hii,ni mizigo mizito isiyobebeka, ambayo mbele ya safari itamuelemea na ama atalazimika kuibwaga, au uzito ukimzidia, itamwagusha na ataanguka nayo!.

Lazima tukiri, hawa wana jf wote walioukwaa uwaziri ni vichwa, ila huyu Mwana jf mwenzetu pale Wizara ya Afya, atakuwa na kazi kubwa ya ziada!, yeye ni dakitari kabisa, yaani a Medical Doctor, ndio kapewa unaibu, lakini bosi wake, sio tuu ni kama 'kiazi' fulani hivi, chenye kila dalili ya ni 'kidumu'!. Wale wataalamu wa mambo ya ndoo na vidumu, wanashauri kubeba ndoo na kidumu, ili maji ya kwenye ndoo yakimwagika, unabaki na kidumu, kinaokoa jahazi!, sasa kama wizara nyingine, inapotokea kidumu ndio kimetangulizwa mbele na ndoo nyuma, inamaana maji ya kidumu ndicho yatatangulia kumwagika, na ndoo ndio itaokoa jahazi!. Hapo Afya Kazi ipo!.

Ila pia tusemazane ukweli, line up ya wabunge wa viti maalum ya CCM, sii mchezo!, kwa watu wa Kanda ya Ziwa na ule udhaifu wetu wa mambo yetu yale, hivi vidumu au mali za watu sijui kama zitasalimika!, ukiona mtu ameteuliwa uwaziri au unaibu, huku hana merits zozote visible, then itakubidi tuu uelewe, huo uwaziri ni ama wa invitation to treaty ama ni asante kwa huduma nzuri!.

Hongera sana Mhe. Mwigulu Nchemba, Mhe. Nape Nnauye na Mhe. Dr.
HKigwangalla. Mfanye kazi na kudeliver ili msiilet down jf.
Hongereni sana!, Hongera JamiiForums.

Paskali
 
Hii ID ni ya January Makamba mwenyewe nini?maana siamini mtanzania mbaye hajaathirika na kitu anaweza waza kuwa January Makamba anafaa kuwa Rais wa Tanzania. Labda awe Rais wa familia yako au ukoo,kabila lenu. Uraisi wa Tanzania kabisa? Please bwana muwe mnakuwa serious kwenye baadhi ya mambo. Hata kama watanzania ni wapuuzi lakini si kiasi hicho.



Yani hawa watu watatu wametia aibu.
Huyu kigwa ndio kabisa ni waziri na wizara yake imelufa hakuna stimulaji package yoyote anayoishauri kwa rais au waziri wa fedha.
Jamaa lipo Twitter linatukana watu na nje ya box yake na vijembe majivuno.
Yani sijui kwa nini januar makamba hatumiwi.
Ingetakiwa pale dodoma January ndio awe rais sasa hivi nchi ingekuwa mbali sana .
 
Kwa hio kat ya January na Magufuli who can make best president?
Pamoja na kila mtu na mapungufu yake
Hii ID ni ya January Makamba mwenyewe nini?maana siamini mtanzania mbaye hajaathirika na kitu anaweza waza kuwa January Makamba anafaa kuwa Rais wa Tanzania. Labda awe Rais wa familia yako au ukoo,kabila lenu. Uraisi wa Tanzania kabisa? Please bwana muwe mnakuwa serious kwenye baadhi ya mambo. Hata kama watanzania ni wapuuzi lakini si kiasi hicho.
 
X100 aendelee Magufuli kama ndo mnawaza hivi bora abaki magufuli.yaani tanzania imekosa kabisa presidentila material mpaka mnamfikiria makamba? Huku ni kututukana sisi watu wazima...kweli ni matusi makubwa sana. Kwa nini lakini?mimi nmewahi kukukosea nini saint?.nmeumia sana.

Kwa hio kat ya January na Magufuli who can make best president?
Pamoja na kila mtu na mapungufu yake
 
Back
Top Bottom