Baraza jipya la Mawaziri: Tanzania Mpya tuliyoitegemea imeanza kuyeyuka..!

aafu angalia wizara aliopewa sina uhakika kama atamaliza miezi mitatu hakujazuka kutokuelewana ,huyu nape ni mkato mkato na ubabe ,na ni mmoja wa asiekubali ushauri hapa kazi tu !

Kauli nyingi za nape ni za kulazimisha na zilizojaa utata aafu mwengine ni yule mwiguru sasa naamini mwaka huu tutaona mambo ya ajabu zaidi kama uliona ajabu ya kikwete utastaajabu ya magufuli na huyu mdini nae amepata uwaziri mtu ambae hafai kuwemo ndani ya serikali ya muungano lukuvi ,wazenji hawataki hata kumuona haswa kwa hotuba yake iliyonaswa ndani ya kanisa ,leo amekuwa waziri tena ,waislamu wanayo kazi,ila kwa zanzibar watazidi kupiga makelele kuwa wanataka na kudai nchi yao.


kwenye hilo barazaaa nape ndo mwenye iq kubwa kuliko wenzake,uchaguzi wa mwaka huu kuwezesha goli la mkono was almost a nightmare,but amemanage
 
Wanabodi
Salaam,

Ukiangalia muundo wa baraza la mawaziri la kikwete na baraza la mawaziri la magufuli,kikwete aliunda baraza la mawaziri zuri sana ukilinganisha na hili jipya la Rais wa awamu ya tano. Tatizo la kikwete alikuwa mpiga dili na serikali yake.
Angalia muundo wa kikwete;




WAZIRI MKUU: MH. MIZENGO PINDA



OFISI YA RAIS [PRESIDENT?S OFFICE]

-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-[Utawala Bora]

-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais [Menejimenti ya Utumishi wa Umma]

-Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais [Mahusiano na Uratibu]

-Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais [Waziri Asiye na Wizara Maalum]

OFISI YA MAKAMU WA RAIS [VICE PRESIDENT?S OFFICE]

-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais[ Mazingira]

-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais [Muungano]

OFISI YA WAZIRI MKUU [PRIME MINISTER?S OFFICE]

-Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu [Uwekezaji na Uwezeshaji]-

-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu [Sera, Uratibu na bunge]

-Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu [TAMISEMI]


-WIZARA YA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA

-WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO

-WIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA


-WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA

-WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA YA MASHARIKI.

-WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

-WIZARA YA NISHATI NA MADINI


-WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI

-WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA

-WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII


-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

-WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO

-WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

-WIZARA YA KATIBA NA SHERIA

-WIZARA YA KAZI NA AJIRA

-WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

-WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI

-WIZARA YA MALIASILI NA UTALII

-WIZARA YA UJENZI

-WIZARA YA UCHUKUZI

-WIZARA YA MAJI NA UMWAGILIAJI

Tukiweka ushabiki pembeni,muundo wa kikwete ulikuwa na tija sana kwa taifa,tatizo lilikuwa ni udhaifu wa Rais ktk kuwasimamia mawaziri wake. Na zaidi ilikuwa serikali ya wapiga dili.

Hebu angalia muundo wa baraza la magufuli.



:
1.Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.

2.Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira

3.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
4.Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

5.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

6.Wizara ya Fedha na Mipango

7.Wizara ya Nishati na Madini

8.Wizara ya Katiba na Sheria,

9.Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

10.Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

11.Wizara ya Mambo ya Ndani

12.Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
13.Wizara ya Maliasili na Utalii

14.Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

15.Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi.

16.Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

17.Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo

18.Wizara ya Maji na Umwagiliaji

Hakukuwa na haja ya kuvuruga wizara za kikwete,alichotakiwa kufanya ni kuteua watu makini na kudhibiti matumizi yasiyokuwa ya lazima. Nchi hii ni kubwa,muundo wa kikwete ulizangatia ukubwa wa nchi yetu na mahitaji. Rais aache kutafuta sifa hata ktk mambo ya ki-taifa.
 
Maudhui ya uzi huwa mwanzo na hitimisho. Unaweza kuwa na lengo jema lakini aina ya uwakishi ukawa wa kuudhi badala ya kushauri.
 
KILICHOFANYIKA NI KIINI MACHO TU!! umepunguza MAMAZIRI,wakati MAKATIBU WA WIZARA wamebaki walewale na idadi ileile, SAWA NA "MVINYO MPYA KWENYE CHUPA YA ZAMANI"
 
KILICHOFANYIKA NI KIINI MACHO TU!! umepunguza MAMAZIRI,wakati MAKATIBU WA WIZARA wamebaki walewale na idadi ileile, SAWA NA "MVINYO MPYA KWENYE CHUPA YA ZAMANI"

Makatibu wakuu lazima waendane na wizara zilizopo. Kwa kupunguza wizara automatically hata makatibu wakuu wa wizara zilizopunguzwa wametolewa.
rejea hotuba ya rais ya uteuzi wa mawaziri.
 
Yaani ulitaka tuendelee kuwa na wizara 300? Utakuwa umepungukiwa kitu fulani kiongozi wangu! Mbona hata za Magufuli zimekaa vizuri tu ingawa zimeunganisha mambo mengi!!
 
Alitwambia atajenga mahakama ya mafisadi .... Sasa mbona baraza lake ndo mafidi mwenyewe atapataje kuwapeleka mahakan....
 
Naona sasa mafisadi,wezi,wauza unga na wazembe mnashangilia.Hongereni,uovu hatimaye umeshinda.
Kabla hujaleta hili andiko, ulipaswa kujiuliza wewe kwanza ni jambo gani umeifanyia Tanzania? Huenda wewe ni miongoni mwa majipu yanayosubiri kutumbuliwa au umeshatumbuliwa. Hata wewe kwenye familia au ukoo wako sidhani kama unayofanya na kuyaamua yanapokelewa na wote kwa mtazamo chanya. Watu wa aina yako hawakosi katika jamii na kwa namna yoyote maisha lazima yaendelee.
 
Back
Top Bottom