Baraza jipya la Mawaziri: Tanzania Mpya tuliyoitegemea imeanza kuyeyuka..!

Sio kweli.. magufuli inawezekana humfahamu..jiridhishe kwanza kabla hujaongea..kama ni fukuzafukuza jk ameifanya sana..

Wewe unaemfahamu hebu tueleze hili
wizara ya viwanda na biashara ni waziri tu bila naibu
halafu wizara ya michezo na sanaa ni waziri na naibu
nini hiko?
 
Kuna watu bado hamjui nguvu ya chama?
Magufuli kapewa order tangaza baraza...
na kaambiwa awe makini na kufukuza watu
Nadhani watu watatuelewa.

Tulisema akianza na kamati kuu, lazima apigwe pini na huo ndio utakuwa mwanzo wa kufungwa mikono na miguu.
Tukasemwa sana, leo watu wanaona wenyewe

Lukuvi na video ya ubaguzi pale Dodoma hakupaswa kuwa katika baraza lake.
Kumteua maana yake amemsamehe kwa ile video iliyoligawa Taifa na kuleta ukakasi.
Hivi hakuna mtu mwingine zaidi ya Lukuvi. Ujumbe gani ameutoa hapo

January, alishindwa kudhibiti kodi ndogo sana za simcard. Mwenzetu Mwanakijiji alianzisha movement iliyobadili hali
Makamba hakuweza. Makamba amechaguliwa pengine kwa role yake katika uchaguzi hasa upande wa 'mitandao'

Ummy, wa BMLK amepewa wizara nyeti ya afya. Hatuna historia ya utendaji wake ukilinganisha na kinachoitwa kasi

Mwayembe alikuwa bandari. Hatujui haya madudu yanayotokea yanamgusaje akiwa kiongozi

Mwigulu, ndio walikuwa wizara ya fedha ambako kuna uhusiano sana na TRA na Bandari

Kipi kipya hapo? Wapi kasi inayosemwa?

Lazima mambo yaende kichama. Alipotoka Dodoma tayari keshawekwa sawa. Back to square one, CCM ni ile ile
 
Haitwi Mulungo anaitwa Professor Muhongo!

Kwakuwa unakimbilia kuandika bila utafiti wa kina unafikiri una point. Prof. alijihudhuru na wala hakufukuzwa, kazi aliyofanya kwa kipindi chake kila mtu aliiona.
Anadhani prof mhongo ni level za akina prof jay wao amaizing!!!!
 
Magufuli kateua baraza zuri kabisa.
Hasa kumrudisha prof. Muhongo, leo talala usingizi mzuri sana.
Halafu tukiamka, tunamwelekeza Mwakyembe sehemu ya kubadili sheria ili tuendelee kutumbua majipu.
 
Ndugu -Wenye tafakari pana watakuuelewa-kimsingi watu wenye nia njema ya dhati juu ya nchi hii imewafadhaisha sana uteuzi huu
 
Kamati kuu ina nguvu kuliko Rais
Rais anakuwa na nguvu kama yeye ndo mwenyekiti ana set agenda
kamati kuu marais wastaafu wanaitwa sometimes...

kuna kitu kinaitwa 'usikiaibishe chama'
au 'huyu mwenzetu usimuumbue'

huwezi tu jifanyia kila kitu the way unavyotaka
mkapa alibanwa,Kikwete alibanwa na Jpm wanambana pia...

Ndiyo maana huwa wanasema ccm ina wenyewe, kumbe ndio hao!
 
Nadhani watu watatuelewa.

Tulisema akianza na kamati kuu, lazima apigwe pini na huo ndio utakuwa mwanzo wa kufungwa mikono na miguu.
Tukasemwa sana, leo watu wanaona wenyewe

Lukuvi na video ya ubaguzi pale Dodoma hakupaswa kuwa katika baraza lake.
Kumteua maana yake amemsamehe kwa ile video iliyoligawa Taifa na kuleta ukakasi.
Hivi hakuna mtu mwingine zaidi ya Lukuvi. Ujumbe gani ameutoa hapo

January, alishindwa kudhibiti kodi ndogo sana za simcard. Mwenzetu Mwanakijiji alianzisha movement iliyobadili hali
Makamba hakuweza. Makamba amechaguliwa pengine kwa role yake katika uchaguzi hasa upande wa 'mitandao'

Ummy, wa BMLK amepewa wizara nyeti ya afya. Hatuna historia ya utendaji wake ukilinganisha na kinachoitwa kasi

Mwayembe alikuwa bandari. Hatujui haya madudu yanayotokea yanamgusaje akiwa kiongozi

Mwigulu, ndio walikuwa wizara ya fedha ambako kuna uhusiano sana na TRA na Bandari

Kipi kipya hapo? Wapi kasi inayosemwa?

Lazima mambo yaende kichama. Alipotoka Dodoma tayari keshawekwa sawa. Back to square one, CCM ni ile ile



Mkuu Nguruvi3 halafu tazama na haya
alijitapa Tanzania ya Magufuli ya viwanda halafu kateua waziri hataki naibu waziri
kama manaibu hawana umuhimu sana na sio lazima iweje tena wizara ya michezo kamteua Nape na naibu waziri juu
ni kama unajiuliza kipi kipaumbele?
sanaa na michezo au viwanda?

halafu kuna kitu kingine cha kushangaza..walemavu wizara ingine
ustawi wa jamii wizara ingine....na bado hiyo ya sanaa na michezo
almost kama vitu vya wizara moja kuwekwa wizara tofauti bila sababu...
 
Great Thinker huwa hakosoi bila kufanya analysis.

Nilitegemea uainishe sehemu uliyoona ina shida, ueleze hiyo shida na utoe mapendekezo Kama kweli wewe ni mzalendo. Vinginevyo jitoe kwenye group la GT's.

Queen Esther

Hbr wakubwa!? Mbele na kiza kinene sana kwa awamu hii ya tano! Kwa baraza hili kiukweli hakuna Jipya, Japo ntatukanwa lakin huu ndo ukweli, Picha ya ovyo kabsa ktk awamu hii tano inameanza kuonekana leo ktk baraza la mawazir, Nam naungana na mamilion ya watanzan ambao wanasema watakuwa wa mwisho kumuamin Magufuli
 
Ccm ni ile ile ,sio uongo nilianza kidogo kua na imani na Magufuli na ndio maana hakuna sehemu yeyote kwenye comments zangu nime muadress kama raisi badala yake nlikua natumia jina Lake kipimo cha mwisho kilikua kwenye baraza la mawaziri kwa hili la Nape na Sospeter Muhongo wa ESCROW WAZIRI ALIYEKATAA KUPANDA NDEGE ECONOMY CLASS KUHUDHURIA MKUTANO EGYPT KISA KAKOSA TICKET YA FIRST CLASS ,HUYU HUYU ALIYESEMA WATANZANIA UWEZO WAO NI KUWEKEZA KWENYE JUICE ,HIZI KWANGU NI DHARAU.

BORA JANUARY NA MAZINGIRA AKASHIKE MA FYKEO HUKO NAONA MZEE UMEAMUA KUTUKUCHOMA NGAZI ULIYOPEWA UPANDE NAYO
LOWASA ATAENDELEA KUA RAISI WA MOYO WANGU KWA MIAKA MINGI IJAYO YEYE PEKE YAKE NDIO ALIKUA NA NGUVU YA KUVUNJA HUU MFUMO WA CCM.

LEO NIMEPATA LOGIC YA KILE KICHEKO CHA JK WAKATI AKIKUSIFU MAGUFULI KWA ULIYOYAFANYA MUHIMBILI. KILE KICHEKO WAKATI WATU WANAKUFA MUHIMBILI KILINITATIZA SANA..
Subir basis lowasa atangaze baraza lake la mawazir akina prof jay mzee was mitulinga hili la rais wet wa mioyo yet tuachie ss tuliomchagua
 
Kama hutaki kumuamini hama nchi. Kwani Nape ana kasoro gani mpaka asipewe Uwaziri kwa mfanio? Mnalingana?? Mpendekeza kakako basi kama unaona hafai.
Kuhusu Prof Muhongo una ushahidi na unachokisema? Peleka Mahakamni ushahidi wako...

Taratibu basi mbona mkali km pilipili kichaaa, imekupalia nini
 
sasa mh.rais anakuwa na majibu ya namna ile. anasema 'hata wewe kwenye gazeti lako kuwa nawafanyakazi wachache tu'.

sasa ajira zitapatikana vp. wakati angekuwa anaiomba sekta binafsi itengeneze ajira kwa wa tz.
 
Ndugu zangu kama sio unafiki ni madharau yaleyale yanaendelezwa mbele ya macho ya watanzania tukiwa tunaona.

Nilianza kuwa na imani na Rais kwamba kwa kuwa ameanza kuonyesha mfano mzuri kwa utendaji kwa mwezi huu mmoja basi atatuletea watu wenye mwenendo mzuri na background yao ni safi.

Kitendo cha kutuletea Mwigulu aliyekuwa naibu waziri wa Fedha ili awe waziri kamili huku akiwa na makashfa kibao ya wizara yao kushindwa kukusanya kodi ni madharau.

Mwakyembe aliyeweka wezi waliofukuzwa siku chache zilizopita kule bandarini na kila siku tunasoma kwenye magazeti jinsi alivyotuletea mabehewa feki leo anarudishwa eti ni msafi anaweza kazi, hayo ni madharau kwa watanzania.

Huyu Makamba naye hana sifa yoyote ya kuwa Waziri ndani ya nchi yetu kwa uwezo wake mdogo na kashfa kibao za majungu na kupepeta maneno hatutaki mtu kama huyu.

Huyu Muhongo aliyerudishwa Nishati si ndiye yuleyule aliyefukuzwa serikali iliyopita kwa kushindwa kazi? Leo hii anarudishwa tena mkifikiri tumesahau hasara aliyotuingizia?

Nilianza kuwa na imani kwa mbaali na huyu Rais japo yupo CCM nilianza kidogo kumuamini lakini sio kuamini chama chake.

Nilikuwa nasubiri nione ni watu gani ataleta ili wawe wasaidizi wake sasa basi kama ndio hao imani yangu imekufa moja kwa moja na huniambii tena kitu mara hii, tusubiri tuone.

Watanzania wenye uwezo na wasomi mbona wapo wengi, mpaka Nape unampa Uwaziri? Kweli upo serious au unatutania?

Sitaki tena kumuamini huyu Rais.

Mlimsimamisha fisadi angombee urais. mbona hilo hukulisema ulikaa kimya ukabunda kama bundi la kingunge. leo sijui umetoka toilet unakurupuka na uchafu wako unakuja kuongea utumbo lofa wewe
 
Back
Top Bottom