Barakoa zitashindwa pia sawa na lockdown

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,313
12,613
Lockdown imeshindwa duniani kote, Mataifa yote yameshindwa kuendelea nayo kutokana na madhara yake. Imeshindwa kwakuwa ni against nature, Mungu alivyoumba na anavyotaka tuwe is against lockdown.

Uvaaji wa barakoa utashindwa, tena vibaya sana kutokana ni against nature na uumbaji. Hewa inayohitajika mwilini kwa nyakati za matukio tofauti ya mwili imepimwa kiasi chake. Hewa inayokwenda na inayotoka mwilini kwenye matukio tofauti imepimwa na Mungu.

Kuna wakati wa kulala, kukaa, kusimama, kutembea, kukimbia, kufanyakazi mbalimbali, nk kunakohitaji kiasi tofauti Cha oxygen na uondoshwaji wa carbon dioxide mwilini. Uvaaji wa barakoa unapunguza kiwango Cha hewa inayoingia na kutoka mapafuni hivyo lazima Kuna Jambo baya litatokea mwilini Kama mtu ataendelea kuvaa barakoa hizi kwa muda mrefu. Madaktari huwa wanavaa barakoa lakini huwa hawakimbii wala kufanyakazi za nguvu zinazohitaji oxygen nyingi mwilini Kama vile kutembea, kukimbia au kufanya kazi za nguvu, hivyo barakoa haziwasumbui sana kuzivaa, tena hawazivai Mara kwa Mara Kama ilivyo kwa CORONA Sasa.

Haijulikani ni carbon dioxide kiasi gani inarundikana mwilini kwa kuvaa barakoa na haifahamiki mwili unakosa oxygen kwa kiasi gani kwa kuvaa barakoa. Haifahamiki madhara kwa watoto, wajawazito na wagonjwa wa pressure, figo, sickle cell, asthma, moyo na wanaofanya kazi za nguvu wakiwa wamevaa barakoa ambazo hata hazifahamiki viwango vyao vya kupitisha hewa na unyevu. Dunia ijiandae kukabiliana na shida nyingine inayozalishwa na upunjaji wa hewa mwilini.

Baadhi ya madhara ya barakoa ni pamoja na mwili kupungukiwa na nguvu, mapafu kuwa na unyevu kuliko kawaida na mwili kuwa acidic. Hii pia Ni against nature hivyo Kuna adhabu itafuata juu ya hili.

Watu waelimishwe kwelikweli kuhusu uvaaji wa barakoa, na barakoa lazima zitengenezwe kitaalam ili kufahamu kiwango Cha kupitisha hewa na unyevu kwenda na kutoka mwilini. Mungu alitengeneza mwili, pua, mapafu, damu, red blood cells na hemoglobin kwa vipimo/ratio. Kuziba pua na mdomo kwa wakati mmoja kutatengeneza kiumbe kingine ambacho sio binadamu wa kawaida.

Kinachoendelea sasa ni programme pana ya Mungu ya kurejesha mazingira kwenye sehemu yake. Hata Marekani bila shaka wanaipata adhabu hii kutokana na kukataa mpango wa dunia wa kuyalinda mazingira. Nadhani Marekani hawatakuwa wabishi baada ya CORONA kuwatandika kisawasawa kuliko taifa jingine
 
Mola atusaidie kwa kweli Mana bila huruma yake hali itazidi kuwa mbaya....Kama kunawa,,kutumia sanitizer na kuvaa barakoa ndiyo ingekuwa kinga natiba sahihi basi mataifa makubwa Watu wake wasingepukutika hivi. Tumrudie Mola na tumuombe sana atuhurumie.
 
Mola atusaidie kwa kweli Mana bila huruma yake hali itazidi kuwa mbaya....Kama kunawa,,kutumia sanitizer na kuvaa barakoa ndiyo ingekuwa kinga natiba sahihi basi mataifa makubwa Watu wake wasingepukutika hivi. Tumrudie Mola na tumuombe sana atuhurumie.
Wataalamu wetu Kama kasuku wanatuambia vitu ambavyo hawana uhakika navyo. Hata hawatoi maelekezo kuhusu madhara ya kuvaa barakoa kwa muda mrefu kwa watu wenye shida ya kupata hewa kama wale wenye shida za anemia, figo, pressure, moyo, na mapafu.
 
”Life will not get back to truly normal, hadi tupate ‘vaccine’ within a period of 18 months”.

By Alien from Microsoft, the reptile.
 
”Life will not get back to truly normal, hadi tupate ‘vaccine’ within a period of 18 months”.

By Alien from Microsoft, the reptile.
Life will not get to normal hadi yafuatayo yatimizwe:
1. Tuache kuendelea kuchafua mazingira.
2. Tuyarudishe mazingira kule yalikokuwa (miti,maji, joto, viumbe)
3. Idadi ya watu ipungue wabaki wanaotosha kuwepo kwenye sayari baasi. Uwezo wa juu kabisa wa idadi ya watu wanaoweza kuishi duniani ni 11 bil. Hivyo kila idadi hii inavyokaribia lazima utaona mabadiliko tusiyoyafahamu. Mvua nyingi kubwa za muda mrefu, joto jingi, kuongezeka kwa maradhi mapya na ya zamani, mimea kushindwa kuzaa vizuri ni miongoni mwa dalili za kuelekea 11 billion.

Mvua hizi zinaiandaa Sayari kugubikwa na maji mengi sana/mafuriko/gharika, njaa nyingi, viumbe wengi wapya, wadudu wa maradhi mengi, vifo vingi vya watu, uoto mwingi na hatimaye Sayari mpya ya dunia yenye afya tele tena (miti, hewa, maji, optimal temperature, matunda, wanyama, samaki, phytoplankton, na viumbe wengine wengi)
 
Back
Top Bottom