SI KWELI Barack Obama Mwaka 2022 alimuidhinisha William Ruto kuwa Mgombea Urais Kenya

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Kuna picha nimeona Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama akizindua uidhinishaji wake wa mwisho wa mgombea urais 2022 nchini Kenya ambapo alionesha wazi kumuunga mkono Naibu Rais Ndugu William Ruto.

Barack Obama ana vinasaba vya Ujaluo, sijui ilikuwa vipi akashindwa kumuunga mkono Mjaluo mwenzio Mwamba Raila Amolo Odinga.

Chanzo: BBC

Ruto.jpg


Obama Ruto.png


===

Video halisi iliyotumika kutengeneza picha hiyo
 
Tunachokijua
Mwaka 2022 Wananchi wa Kenya walifanya Uchaguzi Mkuu wa kuchagua Wabunge na Rais wa nchi yao. Uchaguzi huo ulifanyika Agosti 9, 2022. Uchaguzi huo ulikumbwa na ushindani mkubwa kati ya William Ruto na Raila Odinga waliokuwa pande mbili zenye nguvu zinazokinzana.

Kama alivyodokeza mleta mada, wakati wa uchaguzi huo kuliibuka taarifa mbalimbali zilizotikisa vichwa vya habari. Miongoni mwa taarifa kubwa iliyotikisa wakati huo ni hii (soma hapa) iliyodai kuwa Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama alizindua uidhinishaji wake wa mwisho wa Mgombea Urais 2022 nchini Kenya ambapo alionesha kumuunga mkono Mgombea William Ruto.

Je, upi ukweli kuhusu madai hayo?
JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo inayodaiwa kutolewa na Shirika la Habari la BBC na kubaini kuwa taarifa hii iliwahi kukanushwa na Shirika la Habari la BBC kuwa haikuwa na ukweli.

Katika kufafanua uvumi huo mnamo 30/05/2022 BBC walitoa taarifa (Hii) wakikana kuhusika na habari hiyo. BBC walifafanua kuwa video hiyo ilikuwa ya uzushi na wala haikuhusiana na uchaguzi wa Kenya. Katika habari hiyo BBC wanabainisha kuwa Video hiyo ilihaririwa kwa kuingizwa rangi za BBC na kuwekwa picha ya Ruto ili kupotosha umma kuwa Obama anamuunga mkono William Ruto jambo ambalo halikuwa na ukweli. Taarifa hiyo inaeleza:

Tumekuwa tukichunguza baadhi ya machapisho na video za mitandao ya kijamii ambazo zinazunguka kwa njia ya kupotosha. Barack Obama hajamuunga mkono mgombea yeyote. Video imeibuka, ikidaiwa kuonyesha aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama, akimtangaza kumuunga mkono Bwana Ruto.

_124922006_2_peter_mwai-nc.png.webp

BBC wanaeleza kuwa, video hiyo imefanyiwa uhariri na haina uhusiano wowote na uchaguzi wa Kenya - Bwana Obama hajamuunga mkono mgombea yeyote. Video iliyosambazwa sana imehaririwa ili kuonyesha Obama akitangaza picha kubwa ya mgombea aliyemchagua, na mabango ya uongo yanayoonyesha ni kutoka kwa habari za BBC News, na awali ilichapishwa kwenye akaunti ya TikTok. Matini iliyowekwa kwenye video hiyo ina kosa la sarufi, herufi hazilingani, na rangi za bango hazifanani.

BBC wanaeleza kuwa Video halisi, ambayo ilitumika kama msingi wa ile bandia, ilirekodiwa katika Taasisi ya Smithsonian huko Washington mnamo 2018, ambapo Bwana Obama alikuwa akifunua picha yake mwenyewe.

Hivyo kutokana na kanusho hili kutoka katika kurasa rasmi za BBC pamoja na chanzo kutoka video halisi, JamiiCheck inakubali kuwa taarifa hiyo iliyosambaa wakati huo wa uchaguzi wa Kenya haikuwa na ukweli.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom