Barabara zenye viwango na imara Tanzania

Barabara zenye viwango na imara Tanzania

Mwanza/Bukoba/Kampala usithubutu kupita, kuna kipindi basi ya abiria kidogo ianguke ilipodumbukia katika shimo lililokuwa katikati ya barabara limefunikwa na maji ya mvua. Basi ilikatika spring na abiria wakakomea hapo safari yao. Yalikuwa mateso!
 
Yani hii mada ni perfect, kodi zetu zimepotea kwa kuwalipa makandarasi kujenga barabara hovyo zisizo na mpangilio wala miundombinu ya maji, barabara zimejaa mashimo kila kona hazijamaliza hata miaka mitano,

kimsingi alichofanya magufuli sikioni zaidi ya kukariri idadi ya barabara, idadi ya samaki, idadi ya makandarasi na kilometa za barabara
 
Sisi kwasababu tunatumia usafiri wa barabara tunayaona mashimo na barabara zilizobonyea mfano ruvu/chalinze, inawezekena wengine wanatembea kwa usafiri wa ndege sio rahisi kuona tunayo ona sisi au wapo nchi zingine idadi za km za barabara kujengwa wanasoma ktk vitabu. Nani hakumbuki ajali ya basi lililo angukukiwa na container na kuuwa watanzania kibao nawengine wamekuwa vilema kabla ujafika iringa ilisababishwa na shimo kubwa barabarani. Kitu kama hicho huwezi kuona japani, china uingereza na kwingine ambako barabara zinajengwa kwa kiwango kimoja na na tanzania. wapumbavu macho yao wanaweka pazia lkn werevu atakama utaweka pazia watachungulia tu, aibu yako wewe sijui unandiko na mikono yenye nini naona haya kusema na macho yako sijui yanatumiwa na mwingine kuonea naona aibu kusema pia
 
Jaribu kulinganisha Barbara za magufuli na ile ya salender bridge, nani anakumbuka ile Barbara imejengwa mwaka gani au hata hizi zilizofanyiwa ukarabati na konoike kipindi cha mwinyi je unaweza kuzilinganisha na magufuli ? Au angalia Barbara za mseven toka MASAKA mpaka kampala huone hata kwa kuingalia tu Barbara unahisi itadumu miaka 60.
 
Kingunge ndiye aliyekuwa chinjachija wa ccm toka ujana wake na sasa ni kikongwe lkn kashtuka maana panya anaonekana kuwa na akili zaidi maana anangata na kupuliza unakuja stuka baadaye. Sasa inawezeka madaktari wa vichaa kutoka _,_,_ bingwa wanaiba dawa za wagonjwa wanakunywa lkn kibaya zaidi wanakunywa over dose
 
Inaelekea unaandikia mkono wa mavi au macho yako yanamakengeza hauoni vizuri...hakuna mtanzania utakayemdaganya kuhusu barabara...hadi mwenyekiti wako wa Chadema anajua kazi iliyofanywa na huyu bwana mkubwa na alishampa sifa kedekede...hebu pita humoo👇 uone usivo na akili

http://youtu.be/j0xaIuEaX18

Ni kwa sababu tu za ushabiki tu ndo maana utasifia. Kiuhalisia mapungufu ni mengi sana, na mapungufu haya yanasababishwa na jambo moja kubwa, nalo ni kuangalia IDADI au UKUBWA na suala la UBORA halizingatiwi! Yaletale ya kuwa na shule nyingi ambazo hazina vifaa na matokeo yake ule uwingi wa wanafunzi unakosa maana stahiki kwa kuwa wote wanapata Division 5! Sawa na kujaza mile kibao za barabara za lami lakini zikiwa na viwango hafifu!
 
Sisi tunasema barabara zina mashimo na hazikidhi viwango na tunataja kwa ushahidi, wewe hautaki, unapinga sasa nani mavi na nani kipofu, bora hata kipofu maana shimo atalitambua hata kwa fimbo.

Inaelekea unaandikia mkono wa mavi au macho yako yanamakengeza hauoni vizuri...hakuna mtanzania utakayemdaganya kuhusu barabara...hadi mwenyekiti wako wa Chadema anajua kazi iliyofanywa na huyu bwana mkubwa na alishampa sifa kedekede...hebu pita humoo👇 uone usivo na akili

http://youtu.be/j0xaIuEaX18
 
Kibaya zaidi hizo barabara nyingi mbovu zimetumia pesa ya walala hoi na haziwezi kurudi kuwa nzuri tena kilometa moja ya barabara ni sawa na 1.6 bilioni sasa fanya utafiti kujua ni kilometa ngapi zimejengwa chini ya kiwango utajuwa nchi imepoteza pesa kiasi gani kuna ubadhilifu mwingine unapakwa rangi na watu wanapinga makofi. Mwl Nyerere alisema mtu mwenye akili akikuambia jambo la kijinga wewe ukakubali anakuona mjinga sana
 
Sidhani kama mtu akikupa zawadi ya kuku jogoo kubwa lakini mlemevu utashindwa kutoa shukrani lakini unakuwa una matatizo kama hutajiuliza maswali kwanini nimepewa kuku jogoo mkubwa lakini mlemavu. Sidhani kama kuna ubishani kwa barabara kujengwa nchi nzima hoja ya msingi ni barabara zipo chini ya viwango au na hilo tukae kimya basi sisi mabwege..

Mwl Nyerere aliulizwa habari za rushwa na mwandishi mmoja wa nje ktk serikali yake, alijibu rushwa ipo dunia nzima lkn tofauti ya rushwa ya afrika mfano alitoa mtoto wa wazari wa nchi za mashariki ya mbali anaweze kupewa ukandarasi wa kujenga barabara fulani lkn anajenge kwa kiwango bora lkn kitendo cha kupewa nafasi kwa upendeleo ni rushwa, lkn kwetu hapa mtu anapewa nafasi kwa rushwa lkn ile nafasi pia anaitua vibaya kwakuwa watu wa nchi zetu pia hawahoji na ukijitokeza kuhoji wenzako walala hoi wanakushangaa. Hili ni tatizo kubwa sanaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Wakati tunapata uhuru China na Tanzania tulikuwa tuko Sawa kiuchumi leo hii china wanabarabara zipitazo juu ya milima miezi sita iliyopita wamejenga madaraja baharia gar zinapita

Nenda Ukaishi Huko China
 
Tangu kuanza kwa utawala wa awamu ya nne kumekuwa na kasi kubwa ya ujenzi wa miundombinu karibu pande zote za nchi hii.

Pamoja na kwamba ujenzi huo ulianzia kwenye awamu ya tatu chini ya raisi mstaafu BWM,Waziri wa sasa miundombinu kwa kiasi kikubwa sana amebakia kuwa msimamizi na kiongozi wa wizara hii na kwa mtaji huo ameteuliwa na chama tawala kugombea nafasi ya urais katika awamu ya tano.

Pamoja na kuwa na sifa ya uchapakazi ambayo ndio sifa inayohusishwa na ujenzi wa barabara na madaraja katika ya awamu ya nne,Mhe.John Pombe Magufuri tayari amebatizwa kuwa ni BULLDOZER kwa kuwa yeye ndiye anatwishwa mzigo wa kukisafisha chama tawala,na hasa kunadi mafanikio yaliyopatikana katika kujenga miundombinu ya nchi hii,Nawauliza watanzania wenzangu kama kweli tunaridhishwa na viwango vya barabara tunazokabidhiwa kuwa zimekamilika,hapa nikilenga vigezo kama unene wa lami inayowekwa,upana wa barabara,kingo za barabara,elevation za barabara zetu na zaidi sana alama za barabarani.

Nimesafiri kwa barabara tanzania nzima kupitia kwenye hizi barabara zetu zinazonadiwa kuwa zinajengwa karibu
nchi nzima lakini kwa masikitiko makubwa nashindwa kuelewa ni kwa nini wataalamu wetu walioaminiwa katika wizara ya miundombinu,pamoja na kuwa na exposure ya kutosha,kusafiri nje ya nchi kujifunza,Wanakubali vipi kupokea miradi ya barabara iliyokamilika lakini chini ya viwango?.

Ni kweli kabisa enzi za Mkapa ili kufika Mwanza,Musoma,Bukoba kwa lami ililazimu kupitia Kenya,vinginevyo vumbi ndiyo ilikuwa mpango mzima.

Pamoja kuwa sasa unaweza kusafiri kupitia kwenye barabara ya lami kutoka Dar hadi Mwanza,Mtwara,Songea,Mbeya,Rukwa,Tanga na Arusha.Je ni kweli kuwa tuna barabara za kujivunia tukilinganisha na majirani zetu?

Nadiriki kusema wazi kuwa barabara zetu ni finyu,ziko chini ya viwango na kwa ajili hiyo zinaharibika baada ya muda usiozidi hata miaka mitano.

Ningependa wadau tulijadili hili kwa kutumia uzoefu tuliowahi kuuona katika barabara za nchi mbali mbali ambazo baadhi yetu humu tumeziona na
kuzipitia.Hasa wale waliowahi kusafiri nchi ulaya na asia watupe uzoefu wao.Nawasilisha.View attachment 269987

ndo maana raisi lowassa alivokuja mwanza kutokana na uchafu wa barabara tulilazimika kufagia na kudeki ili apite. Nafikili aliliona hilo coz tulikuwa tunadeki na kufagia mbele ya msafara wa gari yake
 
Naarifu: Barbara kutoka Tanga kwenda mpakani HoroHoro iliyokabidhiwa si zaidi ya miaka mitano iliyopita, sasa inatiwa viraka!
 
Nakumbuka kama jana JK alipokuwa akiitaka NEC impendekeze yeye alisema: ' Nimejua kwa sababu gani nchi huendelea na kwa sababu gani nchi hubaki maskini. Mkinipitisha nitatumia ujuzi wangu kuikwamua Tazania kutoka umaskini'
 
Hizi Barabara za Lami CCM wanazotamba nazo zinatuharibia magari, ni heri barabara za vumbi, nimetoka Singida kuja DSM kila baada ya KM chache wameweka Rasta, hizi Rasta zinaharibu sana haya magari yetu ya bei rahisi, wengine hatujamaliza hata mikopo. Hivi hamuwezi kuweka matuta ya kawaida na Vihashiria, ukipunguza mwendo kwenye rasta unaweza kusababisha ajali. Hizi barabara ni kodi zetu acheni kuziharibu sio kila mtu anaendesha Prado.

Kama hakuna alama ni tatizo. Kuna kipindi watu waliiba sana zile alama kwa ajili ya chuma chakavu sasaivi naona ule wizi umepungua.

Barabara ya dar mbeya upande wa alama super kabisa. Ila kuna tuta moja Nyololo (Mufindi) pale ni kubwa kupitiliza tunaharibu magari
 
Vipande vya barabara kuu ambavyo ni bora kibongobongo ni Chalinze- Morogoro(NCC Arshleef), Iyovi/Ruaha Mbuyuni- Mafinaga( NCC Arsheleef), Nangurukuru- Lindi(Karafi), Kurasini- Ubungo( Maltauro), Ndundu- Somanga( Karafi),angalau Ubungo- Mwenge( Mchina) wengine ongezeeni. Kwa maana hiyo nje ya hapo barabara nyingi zina mashimo, Mawimbi nk
 
Hii nchi imefika sehemu kuwa hata shetani anatushangaa na Mungu anahuzunika kutokana na tunavyofanya mambo yetu, Ni aibu kubwa mtu kujiita mtu mzima then tunajisifia na hivi vichochoro tunaita barabara kuu, miaka hamsini ya uhuru mvua za kawaida tu za msimu zinasomba barabara na madaraja aibu kubwa.
 
Vipande vya barabara kuu ambavyo ni bora kibongobongo ni Chalinze- Morogoro(NCC Arshleef), Iyovi/Ruaha Mbuyuni- Mafinaga( NCC Arsheleef), Nangurukuru- Lindi(Karafi), Kurasini- Ubungo( Maltauro), Ndundu- Somanga( Karafi),angalau Ubungo- Mwenge( Mchina) wengine ongezeeni. Kwa maana hiyo nje ya hapo barabara nyingi zina mashimo, Mawimbi nk
makuyuni mpaka katatu nadhani konoike
 
Back
Top Bottom