Barabara ya njia nne Arusha Inufaishe waendesha vyombo vya moto pia

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,591
4,279
Kwa wale wageni Arusha,

Kuna barabara nzuri sana kutokea Sakina hadi Tengeru na kuna mpango wa kuindeleza ifike Namanaga na Holili kwa upande wa pili
Pamoja na kupendezesha mji kwa kiasi kikubwa kwa mtazamo wangu kuna changamoto inayotakiwa kufanyiwa kazi.

Hii barabara pamoja na kuwa na njia nne inatakiwa madereva wote waendeshe KM 50 kwa saa tokea sakina hadi tengeru kitu ambacho kimekuwa ni kero kwa madereva.

Yaani asubuhi na jioni utakuta jam kuuubwa barabarani inayo sababishwa na madereva kuendesha kms 50 na magari yale ambayo hayasomi kms ndio kabisa yanatembea kms 30 hivi.

Huwa najiuliza, wakati ikiwa barabara moja ilikuwa klm 50 kwa saa, zikawa mbili kms 50 kwa saa, na sasa zipo barabara 4 kms 50 kwa saa; sasa hiyo barabara inatoa urahisi gani kwa waendesha vyombo vya moto kama sio kuwa kero kwa kupigwa faini za tochi kila siku?

Nafikiri ipo haja pia ya kuangalia vibao wa kms 50 kutoka Arusha hadi Njiapanda na kuvipunguza badala yake waweke tu matuta maana tunako elekea itakuwa ni kuendesha kms 50 kutoka Arusha hadi same au pengine Dar.

Hii ni kwa sababu kanda ya kaskazini miji inakua kwa kasi sana hivyo lisipo angaliwa vizuri na kutafutiwa utatuzi naona kutakuwa na tatizo kubwa miaka sio mingi ijayo
 
Hiyo bara bara wamejaa nyuki hadi kero kutoka Tengeru mpaka Mianzini wapo zaidi ya sita...
 
Huwa najiuliza sana kwanini imekuwa njia nne ilhali inapoteza muda wa wadau!!
 
Back
Top Bottom