Nyati
JF-Expert Member
- Mar 6, 2009
- 2,489
- 1,814
Wakuu, hadi sasa hivi, Saa tano na nusu usiku saa za Africa Mashariki, Moro Road hakuna movement yeyote ile. Hasa kati ya Ubungo na Mbezi. Tatizo TANROAD WANAJENGA MATUTA maeneo ya Stop over na Temboni. Sijui kama wana strategic Plan hawa, badala ya kujenga usiku wa manane wao wajenga sasa. Hivyo mimi nipo kwenye gari naperuzi mtandao. Kazi hii wameanza asubuhi hadi sasa. Sina uhakika na hili kwani habari tunapewa na waendesha piki piki ambao wamepata BINGO ya hali ya juu leo. Ubungo - Kimara wanachaji 5,000/= kama huna wasema tambaa.