Barabara ya Morocco Tegeta Wazo kujengwa kuanzia mwenge!!!!

Kisoda2

JF-Expert Member
May 30, 2008
2,475
745
Kuna tetesi juu ya ujenzi wa hii barabara kwamba hautaanzia Morocco kama ilivyoelezwa hapo awali badala yake utaanzia Mwenge hadi Tegeta Wazo kwa kiwango cha njia mbili.
Sababu eti kutoka Morocco hadi Mwenge kuna NYUMBA zimejengwa BARABARANI,hivyo kipande hicho kitaendelea kubaki kama kilivyo.

Wadau hii kweli yaweza kuwa sababu ama kiini macho??
 
Ni kweli ujenzi utaanza hivi karibuni toka Mwenge hadi Tegeta kwa ufadhili wa serikaliya Japan japo study ilifanyika toka Morocco hadi Tegeta. Kwa upande wa Japan kilakitu kiko tayari kwani wao wanatengeneza Barabara na Serikali ya Tanzania wanatakiwa kulipa fidia. Sasa ikaonekana shida ni serikali ya Tanzania kushindwa kwenda na wakati hivyo Serikali ya Japan under JICA wakaomba waanze first phase that side. Ila nailaumu serikali kwani hebu fikiria pale Victoria wameruhusu ujenzi wa hotel na apartiment wakati wanajua kuna ujenzi utaanza na study ilishafanyika bado wanatoa vibali. pili kuna bomba la DAWASCO hivi karibuni limejengwa na litatakiwa kuhamishwa.
 
kama UJAMAA ulivyohujumiwa na watendaji wabovu kuonekana haufai .....vivyo hivyo watendaji walewale ama watoto wao wanaifanyia hivyo serikali ili ionekani haaifai kumbe ni mtu mmoja-mmoja
 
Kama issue ni kwenda Bagamoyo serikali ingefanya mipango ya kujenga nyingine ambayo itakuwa parallel na Ally Hassan Mwinyi na kukutana na hiyo bagamoyo road mbele kwa mbele. Kwani lazima wafike Mwenge? Halafu hiyo barabara ina njia tatu, Wakati wa kuweka njia tatu walitakiwa kufanya mchakato wa kuongeza ya nne kinyume na hiyo tumeona new developments nyingi sana maeneo hayo.
 
Je, unaweza toa mfano wapi ipite hiyo nyingine parallel ambapo hakuna malipo ya fidia?
waziri mwenye dhamana anatakiwa atoe tamko na maelezo ya kina ilikuwaje kukawepo na development hizo wakati ujenzi wa hii barabara ulitakiwa ufanyike toka enzi ya utawala wa mkapa na kikwazo kilikuja Lugalo jeshi lilipogoma ispite hapo.na pesa yake kuamishiwa kwenye mirdi mingine.huku tayari kulishawekwa alama za X kuashiria no develepment.ama ndo mambo ya Kilonda londa hayo????
 
basi watengeneze barabara za katikati zinazoingia na kutoka kipande cha Morroco/Mwenge ili zipunguze msongamano eneo hilo na zitumike kupokea magari yanayoungana na Mwenge/Tegeta. Hili linawezekana kabisa. Vipo vinjia vingi tu vingeweza kukutana na barabara ya Coke-Cola/ Sam Nujoma bila msongamano mkubwa. Hata hivyo huku ndiko kutoangalia mbele ...kuruhusu ujenzi kando ya barabara hii wakati ilionekana wazi haja ya kuipanua. Ila mashaka yangu makubwa zaidi ni wamiliki wake...na nguvu zao. Kama ni katika kuharakisha maendeleo nani anashindwa kuhamishika? Au ndio muda mbaya...Kampeni?
 
Je, unaweza toa mfano wapi ipite hiyo nyingine parallel ambapo hakuna malipo ya fidia?
waziri mwenye dhamana anatakiwa atoe tamko na maelezo ya kina ilikuwaje kukawepo na development hizo wakati ujenzi wa hii barabara ulitakiwa ufanyike toka enzi ya utawala wa mkapa na kikwazo kilikuja Lugalo jeshi lilipogoma ispite hapo.na pesa yake kuamishiwa kwenye mirdi mingine.huku tayari kulishawekwa alama za X kuashiria no develepment.ama ndo mambo ya Kilonda londa hayo????

Kunduchi(Mbuyuni) - Goba - Morogoro Road. Kunduch(Mbuyuni) panakutana na Bagamoyo road kwenda Tegeta. Hii itapunguza msongamano kwa wanaotoka ukonga,temeke,ubungo, kwenda Tegeta-------population ya watu imeongezeka sana kwenda Bagamoyo road.
 
hiyo option mbona ipo mbali sana?hao wa morogoro rd wao ndo wanaitaka foleni?
angalia zengwe liko wapi kabla ya kurukia mjadala.
 
Back
Top Bottom