Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 491
- 781
Ni takribani miaka mitatu tangu kuanza kwa utekelezaji wa Mradi wa Awamu ya Nne wa Barabara ya Mabasi Yaendayo Haraka (Mwendokasi) katika kipande cha Mwenge hadi Tegeta (DAWASA). Hata hivyo, kasi ya utekelezaji wa mradi huo hairidhishi, hasa ikizingatiwa kuwa mkandarasi ameshavuka muda wa awali aliopewa wa kati ya miezi 18 hadi 24 wa kuukamilisha.
Barabara hiyo ya Mwenge hadi Tegeta ina urefu wa kilomita 15.6 na inatekelezwa na mkandarasi M/s Shandong Group Co. Ltd. Kwa mujibu wa TANROADS, ambao ndio wasimamizi wa mradi huo, ilitarajiwa ukamilike mwaka 2025.
Pia soma ~ Barabara ya Mwendokasi kutoka Maktaba hadi Tegeta kuanza kujengwa, Ubungo Kimara kufumuliwa
Hata hivyo, sasa tupo mwezi Juni 2026 na hakuna dalili za mradi huo kukamilika katika kipindi cha karibu. Hata kama mkandarasi ameongezewa muda wa utekelezaji, kasi ya kazi bado ni ndogo kutokana na sababu kadhaa nilizozibaini tangu mradi ulipoanza. Miongoni mwa sababu hizo ni uhaba wa wafanyakazi ukilinganishwa na ukubwa wa majukumu yaliyopo, pamoja na upungufu wa vifaa vya ujenzi.
Hali hii imechangia kuchelewa kwa ukamilishaji wa mradi huo, mbali na changamoto za mvua na joto kali ambazo upande wa mkandarasi uliwahi kuzitaja wakati wa moja ya ziara zilizofanywa na viongozi wa Serikali.
Wananchi waliambiwa kuwa shughuli za ujenzi zingefanyika mchana na usiku ili kuongeza kasi ya utekelezaji na kuhakikisha mradi unakamilika ndani ya muda uliopangwa. Hata hivyo, hali inayoonekana kwa sasa haiendani na ahadi hiyo, kwani kasi ya ujenzi bado ni ndogo licha ya Serikali kuweka wazi kuwa malipo kwa mkandarasi huyo yameshafanyika.
Nilichobaini ni kwamba kumekuwepo na changamoto za usimamizi ambazo zinaweza kuwa zinakwamisha utekelezaji wa mradi huu kwenda kwa kasi inayostahili. Ni wito wangu kwa TANROADS na Wizara ya Ujenzi kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa mradi huu; vinginevyo, kuna uwezekano wa kufika mwaka 2027 bila kukamilika.
Ni muhimu pia kutambua kuwa miradi ya aina hii imekuwa ikigharamiwa kwa fedha za mikopo. Hivyo, kuchelewa kukamilika na kuanza kutumika kwake kunasababisha ongezeko la gharama kwa Serikali, jambo ambalo baadaye linaweza kuongeza mzigo kwa wananchi katika ulipaji wa mikopo hiyo.
Pia soma ~ TANROADS: Ni kweli Mkandarasi wa Mradi wa Mwendokasi Mwenge - Tegeta anasuasua, Serikali itachukua hatua kali
=============================