Barabara ya Kilwa bomu?

Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,728
2,256
Barabara ya Kilwa ni Bomu kabisa!!!!

(From Michuzi)
Barabara hii iliyozinduliwa hivi majuzi ina kila aina ya ubovu wa kitaalam.
Barabara hii imeanza kubonyea sehemu mbali mbali.
Barabara haina mabango ya kuonyesha alama za barabarani.
Katika picha hii jamaa mwenye lori kakatiza katikati ya mduara wa kuongozea magari. Hii ni kutokana na mapungufu makubwa katika usanifu na ujenzi wa barabara hii.
Tunajiuliza hivi Miundo mbinu na taasisi zake zilikuwa wapi wakati ujenzi wa barabara hii yenye mapungufu makubwa ukifanyika?
Ukilinganisha barabara hii na nyingine zilizojengwa na kampuni ya KONOIKE zaidi ya 10 hadi 15 iliyopita utajua kinachoongelewa hapa.
Barabara hii haina hata miaka mitau kukamilika na ina matatizo ya kukatisha tamaa.Itadumu miaka mingine 10?
 
Si unajua tena kama barabara ina lami yenye unene wa nchi 8, ukichukua idadi ya vigogo wanaohusika inakuwa ishu? manake wanaweza kuwepo mathalani vigogo 4 kila mmoja baada ya tenda anakubali apewe tu nusu nchi ya hiyo lami, jumla kwa hao wanne ni nchi 2 tayari, ukijumlisha na wengine 20 wa 0.05inch unabakiwa na inchi 5, bado hawajaiba kokoto mafuta n.k. Halafu tunataka barabara idumu miaka 20, labda ya kuchonga!
 
tanzania ni moja ya nchi zinazofuatilia sana ubora wa procurement zake kwa hiyo barabara ni nzuri ila tu nyie mnataka quality za ulaya ...poleni
 
Inasikitisha, kiwango cha barabara hii ni duni mnooo

Pamoja na mapungufu ya hii barabara kitu kingine kinachonisikitisha ni kwamba hawa jamaa walijenga bila mifereji ya maji ambayo inajengwa na Kampuni nyingine. Enzi za mwalimu anayejenga barabara ndiye aliyekuwa anajenga na mifereji kwani barabara bila mifereji haikalimiki. Cha ajabu enzi hizi za KIFISADI NA USANII ULIOKITHIRI kazi zinafanywa tofauti. Kwangu mimi hili linafanywa kuongeza tu mianya ya chakula cha wakubwa.Kwani hapo contractors watakuwa wengi na process ya kuwapata itakuwa ndefu so grease kulainisha mitambo ya process yao itatumika zaidi. Anyway huenda tutafika thought doubt yangu ni kubwa sana kwa style hii ya maigizo kila kona.,
 
Barabara ya Kilwa ni Bomu kabisa!!!!

(From Michuzi)
Barabara hii iliyozinduliwa hivi majuzi ina kila aina ya ubovu wa kitaalam.
Barabara hii imeanza kubonyea sehemu mbali mbali.
Barabara haina mabango ya kuonyesha alama za barabarani.
Katika picha hii jamaa mwenye lori kakatiza katikati ya mduara wa kuongozea magari. Hii ni kutokana na mapungufu makubwa katika usanifu na ujenzi wa barabara hii.
Tunajiuliza hivi Miundo mbinu na taasisi zake zilikuwa wapi wakati ujenzi wa barabara hii yenye mapungufu makubwa ukifanyika?
Ukilinganisha barabara hii na nyingine zilizojengwa na kampuni ya KONOIKE zaidi ya 10 hadi 15 iliyopita utajua kinachoongelewa hapa.
Barabara hii haina hata miaka mitau kukamilika na ina matatizo ya kukatisha tamaa.Itadumu miaka mingine 10?

Nadhani ungezungumzia uzembe na kukosa umakini kwa madereva wetu. Dereva wa roli hilo yeye alikuja kasi ya ajabu, akashindwa ku-round then akaishia kukatiza kwenye round about hiyo. Huo ni uzembe wa dereva na wala sio ubovu wa barabara ingawa barabara nayo ni mbovu
 
tanzania ni moja ya nchi zinazofuatilia sana ubora wa procurement zake kwa hiyo barabara ni nzuri ila tu nyie mnataka quality za ulaya ...poleni
Hivi ili Lori inayofanya pulling iweze kuzunguka round about, round about hiyo inatakiwa iwe na diameter kiasi gani?
Kama diameter ya round about ni ndogo, Vitz inaweza kuzunguka lakini siyo lori na hilo ni suala la ubora bila mjadala mreefu.
Unless wewe ndio muhandis wa hiyo barabara una data zote za kitaalamu vinginevyo ni vizuri kufanya utafiti kabla ya kujipa pole mwenyewe.
 
Umefika wakati wa kuwashauri TBS wafatilie na kupitisha viwango vya barabara zetu. Sio soda na bia tu.
 
ile barabara ni mbovuu, eneo tajwa ambalo ajali imetokea nadhani ni pale jirani na JWTZ Twalipo camp, jirani na Viwanja vya sabasaba na chuo cha Uhasibu , kwa wakazi wa barabara hiyo nafikiri sijakosea, nimewahi kuipita hiyo njia mara kadhaa, inatechnical problems, mfano mzingo kwenye vipita shpto ni mdogo sana kulinga nisha na ukubwa wa magari yapitayo hapo, barabara ina bumps sana ambazo ni matokeo ya kutokushindiliwa vyema, ama uzito wa magari kuzidi, barabara imechakaa ndani ya muda mfupi...kifupi tumeibiwa tu.
 
Huo ni msaada tu wewe unalalamika nini? wakati pesa yenyewe mnakula wenyewe huko BOT mnakopeshana. Mh. Kikwete ataijenga upya akipita kwenye uchanguzi usijali unajua kukarabati si ghali ghali ni kuplani. watu piiiipooooo.bye
 
Wajanja waliunda KONOIKE ya kibongo wakajitwalia tenda wakapata wakatengeneza hiyo barabara bomu, sasa inaonekana imeanza kuwaumbua
 
Waumini nawakumbusha kutoa fungu la kumi na kutoa sadaka Kila uingiapo Kanisani. Karibuni wote kwenye kanisa lenu la Upako Ubungo. Yesu kristo akulinde na akutangulie kuzuia kila jambo baya.....na akupe kheri kila nukta wakati woote ukiwa unavuta pumzi ...emen
Hii imekaa vizuri original pastor.
 
Hilo lori nililipita jana asubuhi wakati naelekea kibaruani. Kuna mawili hapo, hiyo round about inawezekana ina design problems na pia dereva wa lori ni mzembe. Ukiangalia magari yanayotaka Kilwa yanapitiliza sana na kuingia mfereji(upande wa kushoto) kona imekaa kidogo si sawa. Hasa ukija spidi kali, be careful. Lakini lori lilikuja na spidi gani? kwanza ilikuwa ni giza, huenda halikuwa na taa au jamaa njwiii.Kwa hiyvyo, lazima ulambe kitu pale. Kuna siku nilikuwa nalamba kitu pale kilwa road pub, jamaa alikuwa spiiidi akitokea Kilwa (au sema mbagala), badala ya kukunja alienda straight mtaroni..puuuuuu! bia yangu ilimwagika!. Hiyo round about si nzuri sana, na madereva tuwe macho.
Jamani hiyo barabara iacheni tuuuu...ni mkombozi wa kusinim a.k.a Mbagala, sasa tunateleza kuliko sehemu yeyote ile, japo kwa muda mfupi. Tungengoja ya kiwango, ingepatikana lini? Nani hakuona bango lillilobandikwa pale kurasini ; "BARABARA HII INAJENGWA KWA MSAADA WA FEDHA ZA WALIPA KODI WA JAPANI" . Yaani unaweza kuuliza msaada uliopewa uwe na TBS?! Zawadi ni zawdi chuuukua.... Tutakapoacha kuendekeza misaada ndio tutakapozingatia viwango. Tangu nije hapa dar kila mwaka naona barabara ya mandela iko kwenye ukarabati tu! Labda yale yale....ngoja wa kusini tutanue kwa muda

Ooops! do I call myself TzPride.....of course yes...wahenga bwana!...ati nyumbani ni nyumbani hata kama ni shimoni..yeah.
 
Kuna haja ya kuchunguza usanifu na ujenzi wa hii barabara....kuna kitu hakiko sawa mahala fulani.
 
Si unajua tena kama barabara ina lami yenye unene wa nchi 8, ukichukua idadi ya vigogo wanaohusika inakuwa ishu? manake wanaweza kuwepo mathalani vigogo 4 kila mmoja baada ya tenda anakubali apewe tu nusu nchi ya hiyo lami, jumla kwa hao wanne ni nchi 2 tayari, ukijumlisha na wengine 20 wa 0.05inch unabakiwa na inchi 5, bado hawajaiba kokoto mafuta n.k. Halafu tunataka barabara idumu miaka 20, labda ya kuchonga!
Kuna haja barabara hii kufanyiwa Technical Audit kuthibitisha viwango vyake!!
 
Labda Konoike iliyojenga hiyo barabara ni ya kichina.
we acha kudandia treni kwa mbele soma mada vizuri ndo uchangie na kama hujui kaakimya kwanza unajua ile barabara ilijengwa na mkandarasi Gani? ok nirudi kwenye mada tatizo lililopo hapa ni watoa msaada wanatoa msaada lkn pesa yote inabakia kwao,kajima wamejenga kulingana na pesa walio pewa,tanroad walipaswa kukaa chini na mkandarasi na kutia upya ngharama za ujenzi na kupunguza urefu ili ijengwe kwa kiwango, kwa sababu cost za kurepair ni kubwa sana
 
Wajanja waliunda KONOIKE ya kibongo wakajitwalia tenda wakapata wakatengeneza hiyo barabara bomu, sasa inaonekana imeanza kuwaumbua
we ulitimuliwa konoike nini, kajima tangu lini ikawa konoike?au wewe kila kampuni ya ujenzi ni konoike
 
Back
Top Bottom