Barabara ya kifo - World's most dangerous road - Bolivia

most dengerous
death%20road%2011.jpg

Nilikuwa nimekaa juu ya stool, kuangalia hii picha tu nikala mweleka nilikuwa napata mdadi wa kuliokoa hilo gari lisianguke!
 
Ni kweli ukiangalia uumbaji wa Mwenyezi Mungu hauna mfano. ndio maana tunaambiwa tusiache kuomba na kumshukuru Mungu kwa kila jambo maana ukiangalia hizo barabara huwezi amini lakini ndio maisha waishiyo watu kila kukicha wengine huzipita. Je siku milima ikikasirika kama tuonavyo bahari zinavyokasirika hivi sasa, watu wa huko watafanyeje?

Hapo ndiyo ujue hakuna aliiye kama YEYE aliye juu aliyeumba ulimwengu na vyote vilivyomo akawapa uwezo hao wanadamu wakaijenga hiyo bababara hatujui ni wangapi walisalimika katika ujenzi huo maana ukikosea ukaporomoka chini ndio kwa heri nahisi muda wote walikuwa wamefungwa nira (kamba au kitanzi na maparachuti) wakiporomoka waweze kujiokoa.
 
Kutazama picha tu moyo unaenda mbio! je ikiwa ndio live lazima upite sijui inakuwaje! Inataka kufanana kwa mbali na kitonga!

Maybe hiyo kitonga unaisikia tu. ile barabara jike kabisa. huo mziki wa bolivia is another aisee..
 
kweli bolivia hiyo ni barabar ya kifo nawavulia kofia, hapa kwetu zilikuwepo mpaka sasa kutoka kiwira mbeya hadi mbalizi kupitia igogwe hospital bado ipo, makongorosi chunya bado ipo, morning site morogoro sehemu bado ipo kuelekea bondwa kileleni mlima wa morogogo. Sehemu moja upareni-ugweno ipo lakini wa tz hakuna anaefikiria jinsi ya kuiboresha mpaka sasa miaka 50 ya uhuru. Milima ya bolivia ni ya bonde la ufa katika milima ya andes. Mbinu mya wanatoboa milima. Kama ilivyo china, switzaland ,nk
mkuu hiyo mi road of death ni nouma
 
Kutoka kwasadala kupita njia ya uswaa kuna mto mmoja unaitwa. Marire hapo ni sehemu hatari kama unavyoona hizo za Bolivia
 
Last edited by a moderator:
Barabara zingine ukipita Mara ya kwanza lazima uwe umevaa pampas la sivyo MTU mzima unaumbuka!
 
Back
Top Bottom