Barabara mpya ya Morogoro (STRABAG) inavunjwa

weka picha..maana wanaoishi Kimara Mwisho, wanasema hakuna barabara inayovunjwa! Sijui wewe umeona wapi hilo zoezi likiendelea...

Aliyekwambia hivyo kama alikuadanganya yupo dar basi kakuingiza cha kike
 

asante mkuu nimekuelewa vema
 
Kama ipo chini ya kiwango na inarudiwa, mnaolalamika mnalalamika nini?
 
Kwa hizo barabara za strabag ziliishakabidhiwa au tunabwabwaja tu
 
Barabara ni finyu sana wamepunguza mita moja kila upande wa barabara ndio maana utakuta malori yakikata kona yakwangua barabara na wakati mwingine magari kugonga kingo za barabara na nguzo za taa. Yaani barabara imeshachakaa hata kabla haiajakabidhiwa. Bora hata ilivyokuwa zamani.
 
heri mkuu umejionea
 
Total Demolition?Labda ukomo wake wa kutumika umefika - Decommissioning ina muda sasa tangu ijengwa hivyo labda wanapisha ujenzi wa flyovers. Mambo ya kihandisi haya
Kwahiyo jiji halina master plan? ukibuniwa mradi mpya inabidi mradi wa zamani uvunjwe?
 


Tupia picha !
Je ndiyo ile tetesi ya upana wa Barabara kuchakachuliwa inayoendelea nini?
 
Chanzo cha kubomolewa hiyo barabara ni kwamba Mabasi yaliyokuja kutumika kwa ajili hiyo milango yake ipo upande wa barabara nyingine, lakini acha tuisome namba, tumeipenda wenyewe...!!!
 
Kwahiyo jiji halina master plan? ukibuniwa mradi mpya inabidi mradi wa zamani uvunjwe?

Barabara iliyokuwepo ilijengwa na serikali ya Dernmak ?? miaka 1990s enzi za Mh Keenja watu wakavunjiwa, sasa kabla umri wake au lifetime kwisha ikavunywa ikajengwa Rapid Transport. Nayo hii haijaisha pamebuniwa barabara ingine ya Dar -Chalinze Toll (PPP); hii labda ina njia nane hatujui? na hasa itaanzia wapi?. Pamoja naohii kuna project mpya ya Dar fly overs . lazima nayo ivunje kidogo Mandela? , Nujoma na Morogoro Rd. Kazi ipo. Hivyo jua kila barabara auproject mpya inakula ya zamani bila kujali imefikia lifespan yake. Mambo ya maendeleo . However , Mlipaji ni mi na we. God save
 
Hawa starbag wamejenga barabara nzuri sana kwenda iringa huenda hao dar siyo wenyewe ni feki

Wale ni aarsleef-interbeton jv wala sio Strabag na ndio wanaofanya extension ya terminal 3 airport
 
But lakini chonga utanigambirajeee....?Hivi Zaidi ya kiswanglish wahandisi hamna lugha nyingine?Mimi nimekuelewa hofu kwa wezangu

Hahaha mkuu kawaida sana tunaweka msisitizo kwenye kingereza😝😝😝
 
Kwa kweli wenzetu Nairobi barabara wamejitahidi Sana,na watu wana discipline haswa na barabara,huwezi kuta bodaboda anapitia njia ya waenda kwa miguu....lkn Ss ni usanii kuanzia ujenzi mpk matumizi.labda tunaridhika tukijipima na Kampala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…